Baada ya kutoa orodha ya kwanza ya wapigakura, halmashauri ya kusimamia ucahguzi inapaswa kuwatengea wapigakura na makundi mengine husika wakati wa kuiangalia kabla ya kutoa orodha ya mwisho. Katika wakati huu kesi za rufani zinaweza kushtakiwa zikitaka majina mengine yaongezwe au kuondolewa kutoka kwenye orodha hiyo.
Kufikia hivi majuzi ilikuwa kawaida kwa mamlaka ya majaji au nusu ya mamlaka hiyo kusikiliza rufaa za usajili wa wapigakura. Hivi sasa hii si desturi tena. Katika demokrasia zilizokomaa mchakato wa kukata rufani umekuwa jukumu la kiusimamizi na maofisa wa uchaguzi wenyewe huamua kesi hizo.
Bila shaka, si madai yote kuhusu mabadiliko kwenye orodha ya wapigakura huhitaji kushughulikiwa kama rufani. Mara nyingi huwa maswala mepesi nay a moja kwa moja ya kiusimamizi. Wapigakura wastahifu wanaweza kuwa walitupwa nje ya orodha ya kwanza kwa mfano, japo huenda walitamani kabisa kusajiliwa. Mchakato fulani wa kichunguzi unaoaminiwa kukabiliana na malalamishi ambayo huenda mtu asiyefaa kuwa kwenye orodha au aliyekufa. Katika hali hii, ama stakabadhi rasmi inahitajika au mfumo rasmi zaidi wa malalamishi unaweza kuwekwa.
Kwa kawaida anayetaka rufaa hii anapaswa kufika mwenyewe kabla ya mahakama za rufaa au masahihisho, au halmashauri ya kusimamia uchaguzi. Kunapaswa kuwa na nafasi za kutosha za kuhudhria kikao bila kulazimika kusafiri miendo mirefu au kutumia pesa nyingi. Mahakama au mahakama maalumu zinapaswa kudumisha haki, na zinapaswa kuonekana kuwa na haki. Mamlaka yoyote inayobuniwa kushughulikia rufaa hizo, maamuzi ya bodi hiyo yanapaswa kuwa na uwezo wa kurejelewa, hasa kupitia kwa mfumo wa majaji.