Demokrasia mbalimbali zina mielekeo tofauti tofauti kuhusu jinsi ya kulikabali suala hili la iwapo zinapaswa kuruhusu wapigakura kujisajili siku ya uchaguzi. Katika mfumo unaotumia orodha ya muda, ambao hutayarisha orodha mpya ya wapigakura katika kila uchaguzi, majina yanweza kuachwa nje ya orodha ya mwanzo au ya mwisho kwa sababu mbalimbali: wapigakura wanaweza kusahau kujisajili. Huenda ikawa kwamba hawakujua kama walipaswa kujisajili au kwamba usajili unaendelea. Huenda wakawa wagonjwa au safarini katika kipindi cha usajili. Sababu nyingine hutokea katika mfumo unaotumia rejista endelevu: mpigakura anaweza kuwa kwamba amehama juzi juzi tu na mpango wa halmashauri ya kusimamia uchaguzi wa kutumia deta kwa ushirikiano na mashirika mengine haukunasa mabadiliko hayo ya taarifa kuhusu makao au pengine mpigakura hakusahihisha taarifa hiyo wakati wa kipindi cha masahihisho. Wapigakura pia wanaweza kuwa kwamba wametimiza mahitaji ya ustahi japo hawakuchukua hatua kuingizwa kwenye rejsta ya wapigakura.
Kwa kawaida, mwelekeo wa kukabiliana na suala hili hutolewa katika sheria za uchaguzi katika nchi bali sio kwa kuzingatia ufaafu wa kesi hiyo. Ikiwa sheria inaruhusu usajili kwenye siku ya uchaguzi, ni lazima kuwe na vigezo wazi vya kutekeleza kipengele hicho. Kwa mfano, je, usajili wa wapigakura kwenye siku ya uchaguzi kuruhusiwa tu katika hali maalumu? Halmashauri nyingine za kusimamia uchaguzi huruhusu mtu yeyote stahifu anayewasilisha vitambulisho vinavyotakikana kujisajili na kupiga kura; hili halifanyiki katika mifumo mingine.
Isitoshe, je, halmashauri ya kusimamia uchaguzi ihifadhi orodha ya watu wanaojisajili siku ya uchaguzi kando na ile ya jumla ya wapigakura? Je, ihifadhi pia nakala ya stakabadhi zinazoonyoshwa na wapigakura wanaojisajili siku ya uchaguzi, kama vile leseni ya udereva zilizo na picha au fomu ya usajili wa wapigakura ikiwa na sahihi ya mpigakura huyo? Ikifanya hivi, halmashauri ya kusimamia uchaguzi inalazimika kupangia hifadhi salama ya nyenzo zilizo kwenye kituo cha uchaguzi. Inaweza pia kuhitajika kutoa taarifa kuhusu wapigakura waliojisajili siku ya uchaguzi, na kufafanua wakati na mahali pa vyama vya kisiasa kukagua orodha ya wapigakura hawa.
Punguza hatari ya Udanganyifu wa Wapigakura
Usajili kwenye siku ya uchaguzi unaweza kuzidisha pakubwa hatari ya kuwa na udanganyifu wa wapigakura. Kuna njia nyingi za kupunguza hatari hiyo:
- Utambulisho. Wapigakura lazima waonyeshe utambulisho ulio na picha ili asili yako na kuthibitisha kwamba wanastahi. (Hatari za udanganyifu wa wapigakura ni chache katika nchi ambazo raia wake wote au takribani wote wanabeba vitambulisho hasa vilivyo na picha.)
- Kupigia kura katika eneo la makazi. Wapigakura hutengewa nafasi katika kituo fulani cha upigaji kura katika jumuia zao, na ni lazima waonyeshe au kuthibitisha kwamba wao ni wakazi kwenye jumuia hiyo.
- Kujulikana kibinafsi. Maafisa wa kusimamia uchaguzi katika eneo la upigaji kura hutoka katika eneo la hapo karibu na huenda wakawa wanajuana na watu wanaopaswa kupiga kura katika kituo cha upigaji kura. Bila shaka, hili haliwezekani katika maeneo ya miji.
- Kutambua watu ambao tayari washapiga kura. Ni lazima wapigakura waweke kidole chao katika wino usiofutika haraka ili kuonesha kwamba washapiga kura. Aidha, ya kieneo na uraia.