Umuhimu wa Mifumo ya Uchaguzi
Taasisi za kisiasa huweka sheria za jinsi demokrasia itakavyoendelezwa, na hujadiliwa kila wakati kuwa miongoni mwa taasisi nyingine za kisisa mfumo wa uchaguzi ndio njia iliyo rahisi zaidi kubadilisha, ili kuleta matokeo bora au mabaya. Wakati wa kufasiri kura zilizopigwa katika uchaguzi kuwa viti vya uwakilishi bunge, uteuzi wa mfumo wa uchaguzi huweza kuamua kwa ufanisi ni nani aliyechaguliwa na ni chama kipi kitakachokuwa mamlakani. Huku vipengele vingi vya vya muundo wa kisiasa wa nchi vikiwa vimeelezewa katika katiba na huweza kuwa vigumu kuvifanyia marekebisho, uteuzi wa mfumo wa uchaguzi huhusisha tu sheria mpya na huweza tu kubadilishwa na wafidhuli walio wengi. Hata pale ambapo kila mpigaji kura atakapopiga kura moja na kukiwemo na kura zinazolingana kwa kila chama, mfumo mmoja wa uchaguzi huweza kupelekea kuwepo kwa serikali ya mseto au serikali inayoongozwa na wachache huku mfumo mwingine ukiruhusu chama kimoja kikichukua uongozi kwa wingi.
Mifumo ya Uchaguzi na Mifumo ya Vyama
Matokeo kadhaa ya mifumo ya uchaguzi huwa ni zaidi ya athari hizi za kimsingi. Baadhi ya mifumo hushawishi, au hata kulazimisha, uundaji wa vyama vya kisiasa; mingine hutambua tu wagombeaji binafsi. Mfumo wa vyama ambao hukuzwa, hasa idadi na ukubwa wa vyama vya kisiasa vilivyosajiliwa, hushawishiwa kwa kiasi kikubwa na mfumo wa uchaguzi. Hali hii pia huathiri mshikamano wa ndani na nidhamu ya vyama: mifumo mingine huweza kuhimiza uwepo wa ugomvi ndani ya vikundi tofauti vya chama kimoja, pale ambapo makundi ya chama hicho kimoja yana ugomvi kila wakati, huku mifumo mingine ikihimiza vyama kuzungumza kwa sauti moja na kuondoa tofauti zao. Mifumo ya uchaguzi pia huweza kuathiri jinsi ambavyo vyama hufanya kampeni zao na jinsi ambavyo wanasiasa waliosoma hujitokeza, hivyo basi kusaidia katika kuamua hali ya kisiasa kwa mapana na marefu; wanaweza kuhimiza, au kudidimiza, maendelo ya miungano miongono mwa vyama; na wanaweza kutoa motisha kwa vyama na vikundi kuwa na mawazo pana na wenye kukubali wengine, au kujiweka katika hali finyu yenye miungano ya kikabila na kijamaa.
Mifumo ya uchaguzi na Udhibiti wa Migogoro
Athari hizi tofautitofauti huangaza jukumu muhimu linalotekelezwa na mifumo ya uchaguzi katika udhibiti wa migogoro. Ni wazi kwamba mifumo tofauti ya uchaguzi huweza kuzidisha au kupunguza hali ya wasiwasi pamoja na migogoro katika jamii. Kwa kiwango kimojawapo, wasiwasi huweza kuwepo kati ya mifumo ambayo huweka ushawishi kwenye uwakilishaji wa walio wachache na wale ambao huhimiza uwepo wa serikali inayotawaliwa na chama kimoja. Katika kiwango kingine, ikiwa mfumo wa uchaguzi hauonekani kuwa wa haki na muundo wa kisiasa hauruhusu upinzani kuhisi kuwa wana nafasi ya kushinda katika uchaguzi utakaofuata, walioshindwa wanaweza kulazimika kutafuta uongozi kupitia njia zisizo halali, kwa kutumia njia zisizofuata demokrasia, kuanzisha makabiliano na hata harakati za kivita. Mwishowe, kwa sababu uteuzi wa mfumo wa uchaguzi utaamua urahisi au ugumu wa upigaji kura, utaweza kuathiri makundi ya walio wachache na waliotengwa kimaendeleo. Hili huwa muhimu kila wakati, lakini umuhimu wake huonekana pale ambapo kuna idadi ndogo ya wapigaji kura wasio na ujuzi au wasio na elimu katika jamii.
Athari za Kisaikolojia na Kiufundi
Mifumo ya uchaguzi huchukuliwa kuwa na athari za ‘kisaikolojia’ na ‘kiufundi’. Athari za kiufundi hujitokeza zaidi kupitia jinsi ambavyo mifumo mbalimbali ya uchaguzi inapojaribu kuhimiza uwepo wa mifumo tofauti tofauti ya vyama. Mifumo inayotawaliwa na wengi kwa kawaida huonekana kuwa na athari zenye kuwashurutisha wanachama kwa kuwa wagombeaji au mgombeaji wa hadhi ya juu au vyama katika kila wilaya ya uchaguzi ndio watakaochaguliwa, huku mifumo iliyosawazishwa ikisalia kuwa ‘huru’, matokeo yakiwa vyama vingi vyenye mitazamo tofauti. Athari za kisaikolojia kwenye mifumo ya uchaguzi huimarisha athari hizi za kiufundi: chini ya kanuni za ‘First Past The Post’ (FPTP), wapigaji kura ambao wameamua kufuata chama chenye wafuasi wachache hukumbana na mtanziko wa jinsi ya kuepukana na ‘kupoteza’ kura zao, kwa kuwa mgombeaji mmoja tu ndiye huchaguliwa kutoka kwa kila wilaya. Matokeo ya mtanziko huu ni kwamba wapigaji kura wengi huenda wakakosa kuonyesha uteuzi wao wa ukweli lakini huishia kupigia kura mgombeaji mwingine (kawaida anayetoka kwenye chama kinachoungwa mkono na wengi) ambaye wanaamini ana nafasi kubwa ya kushinda. Athari ya jumla ni kuimarisha vyama vyenye kuungwa mkono na wengi huku vyama vinavyoungwa mkono na wachache vikizidi kudhoofika. Mifumo iliyosawazishwa au mifumo inayoruhusu uteuzi wa kura kwa wingi, ikilinganuliwa, huweza kufanikisha ushindani wa vyama vinavyoungwa mkono na wachache, na hapo kupunguza misukumo ya kupiga kura kwa mpango.
Umuhimu wa Muktadha
Ni muhimu kutambua kwamba mfumo wowote wa uchaguzi hauwezi kufanya kazi kwa njia inayolingana katika nchi mbalimbali. Hata kama kunaweza kuwepo na tajriba zinazolingana katika maeneo mbalimbali ulimwenguni, athari za kila mojawapo ya mfumo wa uchaguzi hutegemea kwa kiwango kikubwa muktadha wa kijamii na kisiasa ambapo unatumika. Kwa mfano, hata pale ambapo makubaliano ya mifumo inayoungwa mkono na wengi inaposalia na kuonekana ikiwekea vikwazo uwakilishaji mpana wa wawakilishaji na mifumo ya Uwakilishaji Uliosawazishwa inapoihimiza, kaida na wazo kuwa walio wengi ndio ambao hutawala husababisha mfumo wa vyama viwili pamoja na Uwakilishaji Uliosawazishwa wa mfumo wa vyama vingi unaoendana na wakati. Katika miaka ya hivi karibuni, FPTP haijawezesha mkusanyiko wa mfumo wa vyama katika demokrasia zinazoendelea kama vile Canada na India, au kupelekea kuwepo kwa uundaji wa vyama imara na vya kudumu kama katika Papua New Guinea. Uwakilishaji Uliosawazishwa umepelekea kuwepo vipindi vya uchaguzi wa chama kimoja kinachotawala huko Namibia, South Africa na kwingineko. Kwa upana zaidi, athari za uteuzi wa mfumo wa uchaguzi hutegemea masiala kama vile jamii ilivyoundwa kwa mujibu wa imani, dini, asili, maeneo, rangi, lugha au migao ya kitabaka; ama kuna mfumo wa chama unaotumika, au vyama ambavyo havijaundwa, na idadi ya vyama vinavyotambulikana, na ikiwa wafuasi wa chama fulani wanatoka katika maeneo yanayofanana kijiogrofia au wametawanyika katika maeneo mapana.
Muundo Mpana wa Kidemokrasia
Ni muhimu pia kuepuka hali ambapo kuna mfumo wa uchaguzi uliojitenga. Mipango na athari zake huwa na umuhimu kwenye miundo mingine ndani na nje ya katiba. Mifumo ya uchaguzi huwa sehemu moja tu ya mifumo mingi ya serikali inayohusiana, sheria na njia ya kupata uongozi. Mfumo wa uchaguzi uliofanikiwa hutokana na kutazama miundo ya taasisi za kisiasa kwa ujumla: kufanyia mabadiliko sehemu moja ya muundo huu huweza kuleta mabadiliko yatakayoathiri jinsi taasisi nyingine ndani yake zinavyofanya kazi. Kwa mfano, ni kwa njia gani mfumo wa uchaguzi ulioteuliwa unavyoendesha au kuhimiza mapatano kutokana na migogoro kati ya viongozi wa vyama na wanaharakati mashinani? Viongozi wa vyama wana udhibiti kiasi gani kwa viongozi walioteuliwa kuwakilisha vyama hivyo? Kuna nafasi ya kikatiba ya kuwepo kwa kura ya maoni, uwezo wa wananchi wa kutoa maoni au ‘demokrasia ya moja kwa moja’ ambayo inaweza kufidia taasisi zenye uwakilishi wa kidemokrasia? Yaliyomo kuhusu mfumo wa uchaguzi yameelezewa katika katiba, kama ratiba ya kiambatisho cha katiba, au kwenye sheria za kawaida? Hili litaamua kiasi cha udhabiti wa mfumo au uwezo wake wa kubadilishwa na wengi wa waliochaguliwa. Kuna masuala mawili ya aina hii ambayo yanahitaji kushughulikiwa zaidi. Kwanza ni kiwango cha mfumo wa mamlaka kutoka sehemu moja. Mfumo wa uongozi wa aina hii ni wa muungano au ni mmoja, ikiwa ni wa muungano, viungo vyake ni linganifu kiutawala au havina ulinganifu? La pili ni uteuzi kati ya uanabunge na uraisi. Mifumo yote miwili ina wakili wake, na tamaduni za kila nchi huweza kuathiri mfumo uliochaguliwa au kutawala mjadala; lakini mahusiano yanayotofutiana kati ya taasisi ya utungaji sheria na ya serikali huwa na athari kubwa kwenye mpango wa mfumo wa uchaguzi. Mijadala ya kila wakati kuhusu uchaguzi wa moja kwa moja wa mameya na viongozi wa serikali nchini hujumlisha maswala yote mawili. Katika baadhi ya serikali zenye mifumo ya bunge mbili na mifumo ya muungano, baraza zote mbili huchaguliwa kwa kuzingatia njia tofauti (au zisizolingana). Hili hudhihirisha sababu mbili muhimu zinazohusiana na nadharia ya kuimarisha muungano. Kwanza, chumba cha pili (au cha juu) cha utungaji sheria cha muungano kiko ili kuwakilisha mikoa au maeneo ya nchi, na kila sehemu kila wakati hupokea uwakilishaji unaolingana bila kuzingatia ukubwa wa idadi ya wananchi au wa kimaeneo (kwa mfano US Senate or South Africa’s National Council of Provinces).
Pili, kuna haja ndogo ya kuunda vyumba viwili vya utungaji sheria isipokuwa pale ambapo kuna viwango tofauti kati ya majukumu na pengine kutokana na uwezo wa vyumba viwili, huku pakiwa na matumizi ya mfumo wa uchaguzi ulio sawa kwa wote huweza kujirudia na kuimarisha nguvu za wengi ambao wanadhibiti chemba cha chini – hasa ikiwa uchaguzi wa vyumba vyote viwili utafanywa wakati mmoja. Vyumba vya juu hutoa nafasi kwa kiwango fulani cha uvumbuzi wa wapigaji kura ili kujumuisha jamii husika ambayo huweza kuwa hawajawakilishwa katika uchaguzi wa kitaifa katika chemba cha chini. Lakini wakati uchaguzi unapofanyika katika viwango vitatu au zaidi, kwa wale walio katika chemba cha juu cha utungaji sheria, chemba cha chini cha utungaji sheria, na taasisi za serikali katika kiwango cha kimaeneo, ni muhimu kuwa mifumo iliyotumika izingatiwe kwa pamoja. Kwa mfano, inawezekana kuimarisha uwakilishaji wa wachache katika kiwango cha kimaeneno huku ikipinga au kuizuia katika kiwango cha taifa. Hili likiwa la kupendeza au la kutopendeza husalia kuwa mjadala na uteuzi wa kisiasa.
Ni kufikia miaka ya hivi karibuni ambapo pamekuwa na mifano michache ya demokrasia za kudumu zinazotumia mifumo ya uraisi. Hata hivyo, uwajibikaji kwa mfumo wa uraisi kwa mfano katika Latin Amerika na baadhi ya sehemu za South – East Asia huzua swali ambalo linauilizwa sasa: Ni mikabala ipi ya mipango ya kitaasisi itakayofanya mifumo ya uraisi kufaulu? Kuna ushahidi kutokana na uzoevu wa Latin Amerika kwamba uimara huweza kuwa changamoto kubwa katika nchi zenye katiba zenye mifumo ya urais na mifumo iliyotengana ya vyama, na kuwa kuna wasiwasi kati ya serikali iliyogawika na wanabunge hawafanyi maamuzi kwa pamoja. Hata hivyo, inaonekana wakati wa mfumo wa uchaguzi wa uraisi una matawi mawili muhimu kwa awamu mbili, mfumo wa utungaji sheria ni List PR, na uchaguzi wa kuchukua mfumo wa uchaguzi unaooonyesha uwezekano kuwa chama au muungano unaounga mkono raisi aliyechaguliwa una wafuasi wa kutosha, hata kama sio lazima uwe na wafuasi wengi, wa wawakilishi bunge waliochaguliwa. Uchaguzi wa wengi wa uraisi na uchaguzi wa pamoja wa uraisi na wa uanabunge huonekana kuwa wenye umuhimu katika kuelekeza mfumo wa chama wa wagombeaji wachache wa uongozi. Hata hivyo, panaweza kuwa hatari kubwa wakati wa kuweka pamoja uwezo mkubwa uliowekewa raisi aliyechaguliwa ambaye ndiye kiongozi wa serikali kwa kutumia mbinu ya walio wengi katika nchi iliyogawanyika kikabila na ambapo hakuna hata kundi moja lililo na wengi wanaotambulikana. Matokeo yanaweza kuwa mabaya na yasiyo halali au hata katika kufanikisha mchakato wa amani. Mfumo wa uchaguzi wa uraisi huweza kufidia mfumo wa muungano kwa kumtaka mgombeaji atakayefanikiwa kupata kura ya ushindi sio tu nchini kote bali pia asilimia kubwa ya kura kutokana na idadi ndogo ya maeneo ya muungano.

