Uchaguzi haufanyiki tu katika vitabu lakini katika uhalisia, na kwa sababu hii uteuzi wa mfumo wa uchaguzi, kwa kiwango fulani, hutegemea gharama na uwezo wa utawala wa nchi inayohusika. Hata kama nchi zinazotoa ufadhili hutoa pesa za kutosha kufadhili uchaguzi wa kwanza na hata wa pili, uchaguzi katika nchi ni njia inayoleta demokrasia, jambo ambalo halitawezekana kwa muda hata kama ilihatajika hivyo.
Muundo wa kisiasa wa kudumu huzingatia rasilimali ya nchi kwa kutazama uwepo wa watu wenye stadi za kufanya kazi kama viongozi katika uchaguzi na kwa kuzingatia mahitaji ya fedha kwenye makadirio ya pesa za taifa
Kwa mfano, nchi maskini haitaweza kugharamia uchaguzi ambao hutokea zaidi ya mara moja chini ya Mfumo wa Two-Round au kuweza kutekeleza kwa ufanisi hesabu ya kura kutokana na uchaguzi wa upendeleo ulio changamano.
Hata hivyo, usahili kwa ufupi hautakuwa wa gharama ya chini. Mfumo wa uchaguzi unaweza kukosa kutumia fedha nyingi na uwe rahisi kutekeleza lakini unaweza kukosa kutimiza mahitaji muhimu ya nchi – na wakati mfumo wa uchaguzi unapokubwa na utata kutokana na mahitaji ya nchi matokeo yanaweza kuwa mabaya.
Kwa upande mwingine, mfumo ambao huonekana mwanzoni kuwa wa gharama ya juu kutekeleza na changamano zaidi kufahamu huweza kusaidia kuhakikisha udhabiti wa nchi kwenye mwelekeo chanya wa demokrasia iliyoimarishwa.

