Kura ya maoni ya mwaka wa 1993 huko Italy, iliyopelekea kuwepo kwa mabadiliko yaliyosababisha mfumo uliosawazishwa wa wanachama mchanganyo (mixed members proportional system -MMP) ambao ungetumika katika uchaguzi duniani kote. Katika nyingi ya hali kama hizi, mabadiliko yamefanywa kandokando, ikiwemo fomula ya ugawanyaji wa viti, idadi mpya ya wilaya za uwakilishaji, au uwepo wa idadi zaidi ndogo za wanachama walioteuliwa katika bunge lakini nchi nyingi pia zimepitia mchakato wa marekebisho na wamebadilisha mfumo wao wa uchaguzi kabisa .
Kutokana na jedwali 1, mkondo uko wazi. Nchi nyingi ambazo zimebadilisha mifumo ya uchaguzi wamefanya hivyo kwa kufuata mwelekeo wa usawazishaji zaidi, ama kwa kuongeza kipengele cha PR kwenye mfumo wa wengi (na kuufanya uwe sambamba au uwe mfumo wa MWP) au kwa kuubadilisha kabisa na nafasi yake kuchukuliwa na mfumo wa awali wenye orodha ya PR. Badiliko la kawaida kabisa limekuwa kutoka kwa mfumo wa wengi hadi kwenye mfumo wa mchanganyiko, na hakuna hata mfumo mmoja wa mabadiliko katika upande mwingine. Mifumo mipya ya wengi yote ilitokana na familia moja isipokuwa tu nchini Madagascar ambapo walihama kutoka mfumo wa orodha ya PR, sio kuelekea kwenye mfumo kamili wa wengi, lakini kwenye mfumo wa mchanganyo kati ya asilimia kubwa ya FPTP na asilimia ndogo ya orodha ya PR.
Jedwali la 1: Mabadiliko ya Hivi Karibuni Kwenye Mifumo ya Uchaguzi.


