THii ni njia inayotumia upigaji kura wa waliowengi katika wilaya zenye uanachama zaidi ya mmoja. Wapigaji kura huwa na idadi kubwa ya kura kama vilivyo viti vinavyojazwa katika wilaya hiyo, na kawaida huwa huru kupigia kura wagombeaji binafsi pasi na kuzingatia vyama vyao. Katika mifumo mingi ya BV, wanaweza kutumia idadi kubwa kabisa au ndogo ya kura zao kama wanavyotaka. Mfumo huu ulitumika huko Jordan mwaka wa 1989, Mongolia mwaka wa 1992 , Philippines na Thailand mwaka wa 1997, lakini ulibadilishwa katika nchi hizi zote kutokana na kutoaminika kwa matokeo yaliyopatikana.

