Chini ya party Block Vote, tofauti na FPTP, kuna wilaya zenye wanachama zaidi ya moja. Wapiga kura huwa na kura moja, na huchagua kati ya orodha za vyama vya wagombeaji kuliko kati ya watu binafsi.Chama ambacho hushinda kura nyingi huchukuwa viti vyote katika wilaya hiyo na orodha yote ya wagombeaji huwa imechaguliwa. Kama katika FPTP, hakuna mahitaji ya mshindi kuwa na ufuasi kamili wa wengi kutokana na ufuasi na kura. Kufikia mwaka wa 2004, PBV ulitumika kama mfumo wa pekee au kipengele kikuu cha mfumo katika nchi nne - Cameroon, Chad, Djibouti na Singapore.

