Manufaa ya PBV
PBV ni mfumo rahisi kutumia, huhimiza vyama imara na kuruhusu vyama kuweka makundi mchanganyo ya wagombeaji ili kuwezesha uwakilishaji wa wachache. Huweza kutumika katika kusaidia kuhakikisha uwakilishaji uliosawazishwa wa kikabila, kwa sababu huviwezesha vyama kutoa orodha ya wagombeaji iliyo anuwai kikabila wakati wa uchaguzi na huweza kwa hakika kupangwa ili iwawezeshe kufanya hivyo.
Udhaifu wa PBV
Hata hivyo, mfumo wa party Block Vote huathirika pia kutokana na baadhi ya udhaifu wa FPTP na huweza kutoa matokeo yasiyokuwa na ulinganifu kabisa pale ambapo chama kimoja hushinda viti karibu vyote ikiwemo ufuasi wa wengi wa kura hizo. Katika uchaguzi wa Djibouti mwaka wa 1997, chama tawala cha Union cha muungano wa Presidential Majority kilishinda kila kiti, huku vyama viwili vya upinzani vikiachwa bila uwakilishi wowote bungeni.

