Uchaguzi chini ya alternative vote hufanyika katika wilaya za uanachama mmoja, kama katika uchaguzi wa FPTP. Hata hivyo, mfumo wa AV hupatia wapigaji kura nafasi zaidi kuliko FPTP wakati wa kuweka alama kwenye karatasi za uchaguzi. Mbali na kuwekea alama wagombeaji wanaowapenda, wapiga kura chini ya AV huwapanga wagombeaji kulingana na uteuzi wao, kwa kutumia ishara ‘1’ kwa mgombeaji wa kwanza, ishara ‘2’ kwa mgombeaji wa pili, ishara ‘3’ kwa watu n.k. Mfumo huu hivyo huwawezesha wapigaji kura kudhihirisha upendeleo wao kati ya wagombeaji mbali na kuteua tu mgombeaji wa kwanza. Kwa sababu hii, mfumo huu hujulikana kama ‘uchaguzi wa upendeleo’ katika nchi zinazoutumia (mifumo mingine ya aina hii ni ‘The Borda Count, STV na Supplementary Vote’.)
AV pia hutofautiana na FPTP kutokana na jinsi kura zinahesabiwa. Kama FPTP au TRS, mgombeaji ambaye ameshinda kura kwa wingi kati ya zote (asilimia 50 na zaidi) huchaguliwa mara moja. Hata hivyo, ikiwa hakuna mgombeaji aliye na idadi kubwa ya wengi, chini ya AV mgombeaji aliye na idadi ya chini ya nafasi ya kwanza huondolewa wakati wa hesabu ya kura, na karatasi zake za uchaguzi kukaguliwa ili kutafuta nafasi ya pili. Kila karatasi baadaye huhamishwa kwa mgombeaji yeyote anayebakia na ambaye ana nafasi ya juu zaidi katika orodha kama ilivyowekewa alama kwenye karatasi ya kura. Mchakato huu hurudiwa hadi mgombeaji mmoja aliye na kura za wengi apatikane na kutangazwa mshindi. Hivyo mfumo wa AV ni mfumo wa kuchaguliwa na walio wengi.
Inawezekana lakini si muhimu katika mifumo ya upendeleo kama vile AV kuwataka wapigaji kura kuorodhesha wagombeaji wote au karibu wote kwenye karatasi ya kura. Hili husaidia kuepukana na uharibifu wa kura katika siku za baadaye wakati wa kuhesabu kwa sababu hazina upendeleo zaidi. Hata hivyo, unaweza kusababisha ongezeko la kura zisizohalali, na huweza wakati mwingine kuonyesha umuhimu wa upendeleo kati ya wagombeaji ambao mpigaji kura hapendi au hana uhakika nao.

Karatasi ya kura ya AV huko Australia

