Sifa ya kimsingi ya mfumo wa Two - Round ni kama jina linavyodokeza. Sio uchaguzi mmoja lakini ni uchaguzi unaofanyika kwa awamu mbili zikitenganishwa na kipindi kifupi cha wakati. Awamu ya kwanza hutekelezwa kwa njia inayolingana na ya awamu moja ya uchaguzi wenye wafuasi wengi. Katika hali nyingi za TRS, uchaguzi hufanywa kwa kutumia FPTP. Pia inawezekana kufanya TRS katika wilaya za uanachama zaidi ya mmoja kwa kutumia Block Vote (kama katika Kiribati) au Party Block Vote (kama katika Mali). Mgombeaji au chama kinachopokea kipimo fulani cha kura huchaguliwa papo hapo bila kutegemea karatasi ya pili ya kura. Kipimo hiki huwa idadi kubwa ya kura halali zilizopigwa, hata kama baadhi ya nchi hutumia idadi tofauti wanapotumia TRS kuchagua rais. Ikiwa hakuna mgombeaji au chama kitakachopokea idadi kubwa, basi awamu ya pili ya uchaguzi hufanywa na mshindi wa awamu hii hutangazwa mshindi.
Maelezo ya jinsi awamu ya pili hutekelezwa huwa tofauti kulingana na hali moja hadi nyingine. Njia inayotumika zaidi ni kinyang’anyiro cha moja kwa moja kati ya washindi wawili wakuu kutokana na awamu ya kwanza ambayo huitwa uchaguzi wa kufuatana wa TRS. Hutoa matokeo ambayo yana idhibati ya kuchaguliwa na wengi hivi kwamba mmoja wa washiriki atapata kura nyingi zaidi na kutangazwa mshindi. Njia ya pili, TRS ya walio wengi hutuniwa kuchagua wanabunge huko France, nchi ambayo hunasibishwa na Two Round System. Katika chaguzi hizi, mgombeaji yeyote ambaye amepokea kura zaidi ya asilimia 12.5 ya wapigaji kura waliosajiliwa katika awamu ya pili basi hutangazwa mshindi, hata, kama wameshinda idadi kubwa au hajashinda.Tofauti na kuchagulia wa pili na idadi kubwa, mfumo huu hauna sifa ya walio wengi, kwa kuwa kunaweza kuwa na wagombeaji watano au sita wakishindania awamu ya pili ya uchaguzi.

