STV umetetewa kwa muda mrefu na wanasayansi wa kisiasa kama mojawapo ya mifumo ya uchaguzi iliyo bora, lakini matumizi yake katika uchaguzi wa uanabunge umekuwa ukitumia katika hali chache – Jamhuri ya Ireland tangu 1921, Malta tangu 1947 na mara moja Estonia mwaka wa 1990. Hutumika pia katika uchaguzi kwenye Australian Federal Senate na katika baadhi ya mataifa ya Australia na katika uchaguzi wa kitaifa Scotland na katika baadhi ya mamlaka huko new Zealand. Ulichaguliwa kama pendekezo la bunge la wananchi la British Columbia.
Kanuni za kimsingi za mfumo huu ziliweka kama njia huru katika karne ya 19 na Thomas Hare huko Britain na Carl Andrae huko Denmark. STV hutumia wilaya zenye uanachama zaidi ya mmoja na wapigaji kura hupanga wagombeaji kulingana na upendeleo wao kwenye karatasi ya kura kama ilivyo chini ya Alternative Vote System katika hali nyingi , uchaguzi huu wa upendeleo huwa wa hiari na wapigaji kura hawahitajiki kupanga wagombeaji wote; wakipenda, wanaweza kutaja tu mmoja.
Baada ya kujumlisha idadi ya kura ya chaguo la kwanza, hesabu basi huanza kuweka quota ya kura zinazohitajika ili kuchagua mgombeaji mmoja. Quota inayotumika huwa ni Droop quata, inayohesabiwa hivi.
Quota = [Kura/(viti +1)] +1
Matokeo huamuliwa kupitia hesabu ya kwanza, idadi yote ya kura za chaguo la kwanza kutoka kwa kila mgombeaji huhakikishiwa. Mgombeaji yeyote ambaye ana idadi ya chaguo la kwanza zaidi au inayolingana na quota huchaguliwa .
Katika hesabu ya pili na inayofuata, kura zinazosalia za wagombeaji waliochaguliwa (yaani kura zilizo juu ya quota) hugawanywa kulingana na chaguo la pili kwenye karatasi za kura. Ili kuonyesha haki, karatasi za kura za wagombeaji wote huweza kugawanywa, lakini kila mojawapo kulingana na asilimia fulani ya kura moja ili idadi ya jumla na masalio ya kila mgombeaji (Jamhuri ya Ireland ilitumia sampuli iliyopimwa badala ya kugawa asilimia) ikiwa mgombeaji alikuwa na kura 100, kwa mfano, na kura za ziadi zilikuwa tano, basi kila karatasi ya kura ingegawanywa kulingana na chaguo la pili katika kiwango cha moja kwa ishirini (1/20) cha kura. Baada ya kila hesabu ikiwa hakuna mgombeaji aliye na kura za zaidi ya quota, mgombeaji aliye na idadi ya chini ya kura huondolewa. Kura zake hugawanywa katika hesabu inayofuata kati ya wagombeaji na chaguo la pili na la chini lilipo. Mchakato wa hesabu unaofuatana, baada ya kugawa kila moja wapo ya kura za zaidi au baada ya kuondolewa kwa kwa mgombeaji, huendelea hadi, ama viti vyote vya katika wilaya ya uchaguzi vimejazwa na wagombeaji ambao wamepokea quota au idadi ya wagombeaji waliosalia kwenye hesabu ni moja tu zaidi ya idadi ya viti vitakavyojazwa, ambapo wagombeaji waliosalia huzuia mmoja kuchaguliwa bila kupata quota kamili.

