Mifumo ya uchaguzi yenye usawazishaji katika uwakilishaji huhitaji kwa kiwango kikubwa kuliko mifumo mingine huhitaji kuwa mpangaji pia azingatie masuala fulani pamoja na uteuzi wa aina ya mfumo wa uchaguzi. Masuala haya yataathiri matokeo ya uchaguzi katika mipango yake na kupitia athari za kisaikolojia kwa kubadilisha vichocheo vya wapigaji kura pamoja na vyama vya kisiasa. Kawaida, athari hizi huonekana kuwa ndogo na hili huweza kuwa kweli katika utendakazi wake. Hata hivyo tofauti yoyote kidogo katika matokeo huweza wakati mwingine kuwa na athari kubwa kwenye upangaji wa uwakilishaji bunge pamoja na uundaji wa serikali na pengine cha muhimu zaidi - utambuzi wa uhalali wa uchaguzi na matokeo yake. Pia, hata kama nyingi ya baadhi ya teuzi hizi huweza tu kuathiri matokeo kwa kiasi kidogo, zingine – kama uteuzi wa ukubwa wa wilaya ya uchaguzi - itakuwa na athari za kutosha katika jinsi ya kufasiri kura kuwa viti, na hivyo huweza kuwa swala kubwa la kisiasa. Hivyo, mpangaji hushauriwa kuzingatia masuala haya yote mapema zaidi kabla ya uchaguzi na kuwa na ufahamu wa utawala unaowezekana pamoja na athari za kisiasa zitakazokuwepo kwenye chaguzi tofauti.

