Kuna makubaliano yaliyo na sifa zinazokaribiana miongoni mwa wataalam wa uchaguzi ambapo uamuzi muhimu katika uwezo wa mfumo wa uchaguzi wa kufasili kura zilizopigwa kuwa viti vilivyoshindwa kwa usawa ni ukubwa wa wilaya, ambao ni idadi ya wanachama watakaochaguliwa katika kila wilaya ya uchaguzi.
Chini ya mfumo kama ule wa FPTP, AV au Two Round System, huwa kuna ukubwa wa wilaya moja; wapigaji kura wanachagua mwakilishi mmoja. Kwa kulinganua mifumo yote ya PR, baadhi ya wafuasi wengi kama vile Block Vote na PBV pamoja na baadhi ya mifumo mingine kama vile Limited Vote na SNTV, huhitaji wilaya za uchaguzi ambazo huchagua zaidi ya mwanachama mmoja chini ya mfumo uliosawazishwa, idadi ya wanachama watakaochaguliwa kutoka kila wilaya huamua, kwa kiwango fulani, kiasi cha usawazishaji matokeo ya uchaguzi yatakavyokuwa.
Mifumo ambayo hupata kiwango cha juu cha usawazishaji, hutumia wilaya kubwa kabisa kwa sababu wilaya kama hizi huweza kuhakikisha kuwa hata vyama vidogo kabisa huwakilishwa katika bunge. Katika baadhi ya wilaya, kiwango chenye ufuasi huwa cha juu Kwa mfano katika wilaya ambapo kuna wanachama watatu peke watakaochaguliwa, chama kinastahili kupata kiasi cha asilimia 25 + 1 ya kura ili kuhakikishiwa kuwa kimepata kiti cha ushindi. Chama ambacho huwa na ufuasi wa asilimia 10 pekee ya wapigaji kura huweza kushinda kiti, na kura za wafuasi wa chama hiki huweza basi kuchukuliwa kuwa zimeharibika. Katika wilaya ya viti sita, kwa kulinganua, asilimia 10+1 ya kura huhakikisha kuwa chama hushinda, kulingana na ukubwa wake wa kijiografia pia - ili uhusiano kati ya mwanachama aliyechukuliwa na eneo bunge lake huendelea kuwa dhaifu.
Hili linaweza kuwa na athari kubwa katika jamii ambapo masiala ya kitaifa huwa na jukumu imara katika siasa au pale ambapo wapigaji kura hutarajia wanachama wao kuweka mahusiano imara pamoja na wanaochaguliwa na kuwa kama ‘mjumbe ’katika bunge.
Kutokana na haya, pamekuwa na mjadala halisi kuhusu ukubwa bora wa wilaya. Wasomi wengi hukubali kama kanuni ya kijumla, kuwa ukubwa wa wilaya wa kati ya viti vitatu au saba huonekana kufanya kazi vizuri, na imependekezwa kuwa nambari tasa kama tatu, tano na saba hufanya kazi katika uhalisi kuliko nambari shufwa, hasa katika mfano wa vyama viwili. Hata hivyo, huu ni mwongozo tu wa muda, na huwa kuna hali nyingi ambapo idadi kubwa huweza kuwa ya kupendeza au muhimu ili kuhakikisha uwakilishaji wa kutosha na uliosawazishwa. Katika nchi nyingi, wilaya za uchaguzi hufuata migao ya utawala iliyopo, labda mipaka ya kitaifa au ya wilaya yaani panaweza kuwa na tofauti kubwa katika ukubwa wake. Hata hivyo, mtazamo huu huondoa umuhimu wa kuchora mipaka mipya ya uchaguzi na huwezesha wilaya za uchaguzi kwenye jamii zilizotambuliwa na kukubalika.
Nambari katika upande wa juu au wa chini wa mpangilio fulani huonekana kutoa matokeo mapana zaidi katika upande mmoja wa mpangilio, nchi nzima huweza kuunda wilaya moja ya uchaguzi ambayo kwa kawaida humaanisha kuwa idadi ya wapigaji kura waliohitajika katika uchaguzi, ambayo kwa kawaida humaanisha kuwa idadi ya wapigaji kura waliohitajika katika uchaguzi ni ya chini kabisa na hata vyaa vidogo kabisa huweza kushinda uchaguzi. Huko Israel, kwa mfano, nchi yote huunda wilaya moja ya wanachama 120 ambayo humaanisha kuwa matokeo ya uchaguzi huwa na usawazishaji wa juu lakini pia humaanisha kwamba vyama vyenye migao michache ya kura huweza kupata uwakilishaji na kuwa uhusiano kati ya mwanachama aliyechaguliwa na eneo lolote la kijiografia huwa hafifu zaidi.
Katika upande huo mwingine wa mpangilio, mifumo ya PR huweza kutumiwa katika hali ambayo kuna ukubwa wa wilaya mbili tu. Kwa mfano, mfumo wa List PR unaotumiwa katika wilaya za uanachama wa aina mbili huko Chile. Hili hutoa matokeo ambayo hukosa usawazishaji kwa sababu hakuna zaidi ya vyama viwili ambavyo huweza kushinda uwakilishaji katika kila wilaya. Hili limeelekea kupuuza umuhimu wa PR katika uwakilishaji na uhalali.
Mifano hii, kutoka pande zote mbili za spektra, yote hueleza umuhimu mkubwa wa ukubwa wa wilaya katika mfumo wowote wa uchaguzi wa PR. Ndio mfumo mmoja muhimu kabisa katika idadi fulani ya mifumo isiyo ya PR. Mfumo wa SingleNon-Transferable Vote, kwa mfano huonekana kutoa matokeo yaliyosawazishwa kwa kiasi hata kama huwa hauna fomula ya usawazishaji, kwa sababu hutumiwa katika wilaya zenye uanachama zaidi ya mmoja. Hali kadhalika, mfumo wa Single Transferable Vote, unapotumika katika wilaya ya uanachama mmoja huwa mfumo wa Alternative Vote ambao hubakisha baadhi ya umuhimu wa STV lakini sio usawazishaji wake. Katika mifumo ya Party Block Vote na Block Vote , wakati ukubwa wa wilaya unapoongezeka, usawazishaji pia huweza kupunguka. Kwa kumalizia, wakati wa kupanga mfumo wa uchaguzi, ukubwa wa wilaya huwa kwa njia nyingi jambo la kimsingi katika kuamua jinsi mfumo unavyofanya kazi katika uhalisi, uwezo wa uhusiano kati ya wapigaji kura na wanachama waliochaguliwa, na matokeo ya jumla ya uchaguzi yaliyosawazishwa.
Kutokana na mtazamo unaohusiana , ukubwa wa chama (idadi ya wastani ya wagombeaji walioshinda kutoka chama kimoja kutoka wilaya moja ya uchaguzi) huwa jambo muhimu katika kuamua ni nani atakayechaguliwa. Ikiwa mgombeaji mmoja atachaguliwa katika wilaya, mgombeaji huyo huweza kuwa mwanaume na mwanachama wa vikundi vya wengi vya kikabila au vya kijamii katika wilaya. Ikiwa wawili au zaidi wanachaguliwa, tiketi sawa huweza kuwa na athari zaidi, huku pakiwa na uwezekano wa kuwa na wanawake zaidi na wagombeaji zaidi kutoka kwa wachache watakuwa washindi. Wilaya kubwa (viti saba au zaidi kwa ukubwa) na idadi ndogo kiasi ya vyama itaongeza ukubwa wa chama.

