Mifumo yote ya uchaguzi huwa na viwango vya juu vya uwakilishi, yaani kiwango cha chini cha ufuasi ambacho chama huhitaji kupata uwakilishi. Viwango vya juu huweza kuwekwa kisheria (viwango rasmi) au viwepo kama mali ya hisabati ya mfumo wa uchaguzi (viwango asilia au vinavyofaa).
Viwango rasmi huandikwa kwenye matoleo ya katiba au sheria ambayo hueleza mfumo wa PR katika mifumo iliyochanganyika huko Ujerumani, New Zealand, Russia kwa mfano, kuna asilimia 5 ya viwango katika sehemu ya PR: vyama ambavyo hukosa kupata asilimia 5 ya kura kote nchini huwa havistahili kupewa viti kutokana na orodha za PR. Dhana hii ina misingi yake katika umuhimu wa kuwekea vikwazo uchaguzi wa makundi yaliyozidi huko Ujerumani, na umepangwa ili kuzuia vyama vidogo kabisa kupata uwakilishaji.
Hata hivyo huko Ujerumani na New Zealand kuna njia za ‘mlango wa nyuma’ za kuwezesha chama kupata viti kutokana na orodha; kama ilivyokuwa New Zealand chama lazima kishinde angalau kiti kimoja cha bunge na katika Ujerumani viti vitatu, ili kupata viwango vinavyohitajika. Huko Russia katika mwaka wa 1995, hakukuwa na njia za mlango wa nyuma na karibu nusu ya kura kwenye orodha ya vyama zilikuwa zimeharibika. Kwingineko, viwango vya kisheria huwa kati ya asilimia 0.67 huko Netherlands hadi asilimia 10 huko Turkey. Vyama ambavyo hupata chini ya asilimia hizi ya kura hutolewa katika orodha. Mfano mzuri ni wa uchaguzi wa Turkey mwaka wa 2002 ambapo vyama vingine vilishindwa kufikia asilimia 10 ya kiwango na asilimia 46 ya kura ziliharibika. Katika hali hizi zote, uwepo wa viwango rasmi huelekea kuongeza kiwango cha jumla cha ukosefu wa usawazishaji kwa sababu kura za vyama hivi ambavyo vingetumiwa kupata uwakilishaji huharibika. Huko Poland mwaka wa 1993, hata baada ya kutumia viwango vya chini vya asilimia 5 kwa vyama na asilimia 34 ya kura zilipigiwa vyama na miungano ambayo haikuipita.
Kiwango kinachofaa, kilichofichika, au asilia huundwa kama tokeo la hisabati, kikiwa na sifa za mifumo ya uchaguzi, ambapo ukubwa wa wilaya ndio muhimu zaidi. Kwa mfano, katika wilaya yenye viti vinne chini ya mfumo wa PR, kama ilivyo kwa kila mgombeaji aliye na zaidi ya asilimia 20 ya kura atakayochaguliwa, mgombeaji yeyote aliye na chini ya karibu asilimia10 (idadi kamili huwa tofauti kutegemea mipangilio ya chini ya chama, wagombeaji, na kura) hana uwezekano wa kuchaguliwa.

