Huku MMP ikiweka  faida  za  usawazishaji  za mifumo ya PR, pia huhakikisha kwamaba waliochaguliwa  wameunganishwa  na  wilaya  kijiografia. Hata hivyo, pale ambapo wapigaji  kura  wana kura mbili - moja ya chama  na  moja ya  mwakilishi wa eneo lao - huwa  haieleweki kila wakati kuwa kura ya uwakilishaji wa eneo lao huwa haina  umuhimu kuliko kura ya   chama katika  kuamua  utoaji wa  kijumla  wa viti bungeni.  Zaidi  ya hayo, MMP huweza  kutoa  makundi  mawili ya  wanabunge  kundi  moja  likiwajibikia  eneo  bunge  na  lingine  kutokana  na orodha  ya chama  cha  kitaifa  bila  mahusiano ya  kijiografia  na kushughulikia  chama. Hili linaweza  kuwa  na  athari  katika  mshikamano wa  makundi  ya wawakilishaji wa vyama  waliochaguliwa.
Katika  kufasiri kura kuwa  viti, MMP huweza  kuwa  na  usawazishaji wa  mfumo wa uchaguzi kama  ilivyo List PR iliyo safi, na  hivyo, sababu moja  ya kwa nini MMP wakati mwingine huchukuliwa  kama usiopendelewa  ikilinganishwa  na List PR  uliowekwa  sawa ni kwamba  unaweza kutoa  matokeo  yasiyo ya  kawaida  yanayotiwa  ‘upigaji kura wenye mikakati’. Huko New Zealand  mwaka wa 1996,  katika eneo bunge  la  Wellington Central, baadhi ya  mikakati  ya  National Party  iliwahimiza  wapigaji  kura  kutopigia  kura  mgombeaji  wa National Party kwa sababu walikuwa  wamepiga  hesabu   kwamba  chini ya  MMP, uchaguzi wake  haungepatia  National Party  kiti kingine  lakini  kumbadilisha mwanabunge  ambaye  angechaguliwa  kutokana  na orodha  yao  ya chama. Basi ilikuwa  afadhali kwa National Party  kumuona  mgombeaji  akichaguliwa  kutokana na chama  kingine  ikiwa mgombeaji  huyo  alikuwa ana  upendeleo  wa maoni na  imani za  National Party kuliko  kwenye  kura ‘zitakazo haribika’ ili kumuunga mkono mgombeaji wao.
 
