Mifumo sambamba pia hutumia vipengele vya mifumo ya PR na vya mifumo yenye wafuasi wengi, lakini tofauti na mifumo ya MMP, kipengele tofauti cha PR cha mfumo sambamba hakiwezi kufidia ukosefu wowote wa usawazishaji ndani ya mfumo wa wafuasi wengi.(Huwa na uwezekano wa kipengele kisichokuwa cha PR cha mfumo sambamba kutoka kwenye familia ya mifumo ‘mingine’ kama ilivyokuwa huko Taiwan ambapo SNTV hutumiwa).

Katika Mfumo Sambamba, kama katika MMP, kila mpigaji kura huweza kupokea karatasi moja ya kura ambayo hutumiwa kupigia kura mgombeaji pamoja na chama chake kama ilivyo huko South Korea (Jamhuri ya Korea), au karatasi mbili za kura, moja ya kiti chenye wafuasi wengi na moja ya viti vya PR kama ilivyo huko Japan, Lithuana na Thailand. Mifumo Sambamba imekuwa matokeo ya mpango wa mfumo wa uchaguzi kwa zaidi ya mwongo mmoja na nusu- labda kwa sababu huonekana kujumlisha pamoja umuhimu wa orodha ya PR na ile yenye uwakilishi wa wafuasi wa wengi (au nyingine).

