Umuhimu wa Mifumo Sambamba
Kwa kuzingatia ukosefu wa usawazishaji, Mifumo Sambamba hutoa matokeo ambayo huwa kati ya ile ya ufuasi wa wengi iliyo safi na ile ya PR iliyo safi. Umuhimu wa kwanza ni kuwa panapokuwa na viti vya PR vya kutosha, vyama vidogo vyenye ufuasi mdogo ambavyo havijakuwa vikifanikiwa kwenye uchaguzi wa ufuasi wa wengi huweza pia kuzawadiwa kwa sababu ya kura kwa kushinda viti katika utoaji uliosawazishwa. Pia, Mfumo Sambamba unastahili, kinadharia, kuvunja mfumo wa chama kwa kiasi kidogo kuliko mfumo sawa wa uchaguzi wa PR.
Udhaifu wa Mifumo Sambamb
a
Kama ilivyo MMP, haiwezekani kwamba makundi mawili ya uwakilishaji yanaweza kuundwa Pia, mifumo sambamba haitoi uhakika wa jumla wa usawazishaji na vyama vingine huweza pia kufungiwa nje ya uwakilishaji hata kama vimeshinda idadi Fulani ya kura. Mifumo sambamba pia huwa changamano kwa kiasi na huweza kuwafanya wapigaji kura kukanganyikika kuhusu hali na utekelezaji wa mfumo wa uchaguzi.

