Mifumo mingi ya uchaguzi, ile yenye ufuasi wa wengi na iliyosawazishwa, huwa na safu moja ya uwakilishaji: kila mpigaji kura nchini hupiga kura mara moja na huwa kuna seti moja ya wawakilishaji waliochaguliwa. Katika mifumo ya safu moja ya List PR, orodha huwa katika kiwango cha kitaifa, au kimaeneo, kama ilivyo huko Finland na Switzerland.
Katika mifumo iliyochanganywa, huwa kuna safu mbili za uwakilishaji, ile ya wale waliochaguliwa chini ya mfumo wenye ufuasi wa wengi na ile ya wale waliochaguliwa chini ya mfumo uliosawazishwa. Huko Hungary, hata hivyo, huwa na safu tatu: wawakilishaji kutoka mfumo wenye ufuasi wa wengi kutoka wilaya zenye uanachama mmoja waliochaguliwa kwa kutumia TRS; pamoja na wawakilishaji katika kiwango cha kieneo na kiwango cha kitaifa waliochaguliwa kwa kutumia List PR.
Pia inawezekana kuwa mfumo wa uchaguzi kuwa na safu mbili bila kuwa na sifa za kuwa umechanganywa. Mifumo ya usawazishwaji yenye safu mbili huweza kuwa na orodha ya kitaifa na kieneo (kama huko Afrika Kusini) au orodha ya kieneo pekee (kama huko Denmark). Katika mfumo wa safu mbili wenye wafuasi wengi katika British Virgin Islands, huwa na wawakilishaji waliochaguliwa kutoka wilaya zenye uanachama mmoja huku wakitumia mfumo wa FPTP na wawakilishaji waliochaguliwa kutoka Visiwani kwa ujumla kwa kutumia mfumo wa Block Vote.
Jedwali la 6: Tofauti katika Uwakilishaji Uliosawazishwa

Mifumo ya uchaguzi yenye safu mbili au zaidi huhitaji kubainishwa kutokana na mifumo zalishwa ambapo sehemu moja ya nchi huchagua wawakilishaji wake kwa kutumia mfumo mmoja wa uchaguzi, na sehemu nyingine ya nchi huchagua uwakilishaji kwa kutumia mfumo tofauti. Huko Panama, kiasi cha thuluthi tatu za wawakilishaji huchaguliwa kutokana na wilaya zenye uanachama mmoja kwa kutumia FPTP bila mwingiliano wa aina mbili za wilaya.
Jedwali la 7 hutoa muhtasari wa umuhimu na udhaifu wa mifumo mikuu ya uchaguzi. Ni muhimu kukumbuka kwamba umuhimu na udhaifu uliotolewa hapa huweza kuwa tofauti kutoka hali moja hadi nyingine na hutegemea maswala mengi yaliyo tofauti. Kwa mfano, utokeaji wake huweza kuwa wa juu chini ya mfumo wa FPTP, na mfumo wa List PR huweza kutoa ufuasi wa uwakilishaji ulio imara kwa uraisi. Pia, kile ambacho huonekana kama muhimu katika muktadha mmoja au na chama kimoja huweza kuonekana kuwa kinyume katika muktadha au chama kingine.
Jedwali la 7: Teuzi Tano za Mifumo ya Uchaguzi: Umuhimu na Udhaifu


