Kuna njia nyingine nyingi za kuwezesha uwakilishaji wa wachache na makundi ya kijamii. Pia, mifumo ya uchaguzi ambayo huwa na ukubwa wa kutosha huvitia moyo vyama katika kuteua wagombeaji kutokana na makundi ya wachache katika misingi ya kwamba tikiti zilizosawazishwa zitatumika kuongeza nafasi zao za kuchaguliwa. Kiwango kidogo kabisa cha kupimia, au uondoaji kamili wa kiwango hiki, katika mifumo ya PR huweza pia kuwezesha uwakilishaji wa makundi ambayo yamewakilishwa kwa uchache au hayajawakilishwa kwa kuhimiza uundaji wa vyama vya kisiasa ambavyo vitawawakilisha wao wenyewe. Katika mifumo yenye ufuasi wa wengi hasa, viti, wakati mwingine vinavyotengewa makundi ya wachache na ya makundi ya kijamii bungeni.
Viti vilivyotengwa huweza kutumiwa kuhakikisha uwakilishaji wa makundi fulani ya wacache bungeni. Viti hutengwewa makundi ya wachache ya kiasili au ya kidini nchini kama ilivyo huko Colombia (‘jamii za watu weusi’), huko Croatia ( jamii za wachache kutoka Hungarian, Italian, Czech, Slovakia, Ruthenian, Ukranian, Ujerumani, na Australia), India ( makabila na tabaka zilizoratibiwa), Jordan ( Wakristo na Circassians), Niger (Tuareg), New Zealand (Maori), Pakistan (Makundi ya wachache wasio Waislamu), Palestine (Wakristo na Wasamaria), Samoa (makundi ya wachache wasio wa asili ya huko), Slovenia (Hungarians na Italians), na Taiwan (jamii ya ‘aboriginal’). Wawakilishaji kutoka katika viti vilivyotengwa huchaguliwa kwa njia inayolingana na ile ya wawakilishaji wengine lakini wakati mwingine huchaguliwa na wanachama kutoka kwa jamii ya walio wachache kama ilivyo katika sheria za uchaguzi. Hili huhitaji orodha moja ya jumla (orodha ya wapigaji kura kutokana na hali kwamba wanatokana na chama hicho na wamehitimu kupiga kura katika uchaguzi huo). Huku ikichukuliwa kama kaida nzuri ya kuwakilisha jamii ndogo pia inadaiwa kuwa huu ni mkakati bora wa kupanga miundo ambayo hutoa uwakilishaji bungeni bila kutumia vibaya sheria za uchaguzi au jukumu la kisheria, na kuwa viti vya quota huweza kuzalisha uhasama kutoka kwa jamii za walio wengi na kuzidisha ukosefu wa uaminifu kati ya makundi ya kijamii.
Bali na viti vilivyotengwa kirasmi, maeneo yanaweza kuwa yamewakilishwa kuliko ilivyo kawaida ili kuwezesha ongezeko la uwakilishaji wa makundi yaliyo katika maeneo finyu kijiografia. Huko UK, Scotland na Wales huwa na Wanabunge wengi katika British House of Commons kuliko inavyotakikana ikiwa kiwango cha idadi ya wanachi pekee kilikuwa kigezo pekee cha kuzingatia. Hali kama hii huwa kweli katika maeneo ya milimani ya Nepal.
Uwezekano mwingine ni mfumo wa mgombeaji aliyeshindwa kabisa unaotumiwa huko Mauritius, pale ambapo wagombeaji ambao wanapoteza na waliokuwa na kura za juu kutokana na kundi fulani la kikabila hutuzwa viti bungeni ili kusawazisha uwakilishaji wa kikabila kwa ujumla.
Mipaka ya uchaguzi huweza pia kubadilishwa ili kuimarisha uwakilishaji wa makundi fulani. Sheria za Haki ya Kupiga Kura huko United States hapo awali zimeruhusu serikali kuweka mipaka ya wilaya yenye maumbo yasiyo ya kawaida huku wakiwa na lengo la kuunda wilaya za wengi wa Watu Weusi, Walatino, au za Asian- American; jambo lilalorejelewa kama ‘ufanyaji hila unaokubalika wakati wa uchaguzi ili kupendelea kundi fulani’ Hata hivyo mabadiliko yenye upendeleo ya mfumo wowote wa uchaguzi ili kuinua au kulinda wawakilishaji wachache huwa kwa kawaida si yenye ubishani.

