Uchaguzi, uwe ni wa kuchagua wawakilishaji katika taifa, baraza la mawaziri, bungeni, taifa nzima, au taasisi za kimaeneo, si lazima, kwa kawaida, ufanyike kwa siku moja (au siku mahsusi) lakini unaweza kutawanywa. Sababu za kutenganisha uchaguzi kwa kipindi fulani cha wakati huweza kuwa za kiutendaji au za kisiasa. Kutawanywa kwa uchaguzi kawaida hutokea pale ambapo kuna maandalizi mengi yanayohitajika (kwa mfano uchaguzi wa kuchagua wawakilishi katika chemba cha chini huko India, Lok Sabha, huchukua muda wa siku nne kwa kipindi cha majuma kadhaa kutokana na uhitaji kura) au pale ambapo pana haja ya kuweka usalama zaidi. Mahitaji ya kiutawala na kiusalama humaanisha kwamba huwa rahisi zaidi kwa Tume ya uchaguzi ya India kuratibu utekelezaji wa kura za uanabunge kwa kuzingatia wakati na mataifa yaliyopo. Ugumu unaokumbana na uchaguzi unaotenganishwa hujumlisha usalama wa karatasi za kura; ili kuhakikisha kuwa maeneo ambayo yanapiga kura baadaye hayaathiriwi na maeneo ambayo tayari yamepiga kura, karatasi za kura huhitaji kuchungwa katika maeneo moja maalum hadi upigaji kura wote kumalizika ambapo kura zote zitaweza kuhesabiwa pamoja.
Njia inayotumika zaidi ni ule utenganishaji wa wakati fulani katika uchaguzi wa uraisi, uanabunge na wa serikali za ushirikisho. Kuna idhibati ya kutoa maoni kuwa utekelezaji wa uchaguzi wa uraisi na wa uanabunge siku moja huweza kuwa wa kupendelea chama ambapo raisi ni mwanachama na bunge na mawaziri kukosa mtawanyiko na hivyo kuifanya serikali kuwa na mshikamano zaidi hasa katika demokrasia changa. Hata hivyo, ikiwa kuna matamanio ya kukaza ugawanyaji wa uongozi au kuna uwezekano wa mipango ya kuzingatiwa, basi inaweza kuwa muhimu au busara kutenga uchaguzi wa urahisi na ule wa uanabunge.

