Kuna uhusiano uliopo kati ya kiwango cha utokeaji katika kupiga kura na mfumo wa uchaguzi uliochaguliwa. Mifumo ya PR huwa kwa kawaida imenasibishwa na ujitokeaji wa hali ya juu. Katika mifumo yenye ufuasi wa wengi, ujitokeaji huonekana kuwa wa juu wakati ambapo chama kimoja kinauhakika wa kushinda, na pia huwa wa juu katika wilaya binafsi ambapo matokeo hutarajiwa kukaribiana.
Kama njia ya kuinua kiwango cha uhalali wa uchaguzi, baadhi ya nchi, hasa baadhi ya zile jamhuri zilizojitenga na ukomunisti wa USSR, walianzisha viwango vya chini vya ujitokezaji vya lazima. Ikiwa ujitokeaji katika wilaya ya uchaguzi haukufika, kwa mfano, asilimia 50, uchaguzi hivyo basi haukuchukuliwa kama halali. Hata hivyo, matumizi ya viwango vya ujitokeaji vya lazima huweza kusababisha mtafaruku wa kiutawala ikiwa uchaguzi uloirudiwa ukakosa kupita kila wakati ili kupata viwango vya utokeaji wa lazima baada ya uchaguzi wa 1998 baada ya uwepo wa kurudiwa rudiwa kwa uchaguzi ambao haukupita ili kufikisha ujitokeaji uliohitajika mwaka wa 1994.
Nchi nyingi hushughulikia suala hili la uhusika kwa kutumia upigaji kura wa lazima, zikiwa ni pamoja na Australia, Belgium, Greece na nchi nyingi, hata hivyo, hakataa upigaji kura wa lazima kutokana na misimamo yao. Huku ukiwa na uwezekano wa usawa unaolingana pamoja na mfumo wowote wa uchaguzi, matumizi yake huweza kuzingatiwa pamoja na masuala mengine yanayohusiana na ujitokeaji.

