Kila mfano wa wilaya ya uanachama mmoja huhitaji mchakato unaochukua muda na ambao ni wa gharama ya juu katika uwekaji mipaka ya maeneo madogo ya uwakilishi bunge. Jinsi ambavyo maeneo hayo hugawanywa hutegemea masuala kama vile idadi ya wananchi, mshikamano wake, njia za usafiri na mfumo wa mawasiliano, mapendeleo ya wanajamii, na ujirani Zaidi ya hayo hili si zoezi la siku moja kwa sababu mipaka inastahili kubadilishwa kila wakati ili kuzingatia mabadiliko ya idadi ya watu. Mifumo ya FPTP, AV na STV pia huhitaji wilaya za uchaguzi kugawanywa lakini huwa rahisi kuongoza kwa sababu hutumia wilaya za wanachama zaidi ya mmoja ambazo zitakuwa chache kiidadi na kubwa. Uwekaji wa mipaka ya mifumo yenye mchanganyo ya elementi ya walio wengi huwa na changamoto zinazofanana.
Wakati wilaya zenye wanachama zaidi ya mmoja zinapotumiwa, inawezekana kuepuka uhitaji wa kubadilisha mipaka badala ya kubadilisha idadi ya wawakilishi waliochaguliwa kutoka kwa kila wilaya ya uchaguzi - njia ya hadhi fulani wakati sehemu kama vile mikoa hutumiwa kama wilaya za uchaguzi. Mifumo ya orodha ya PR kwa kawaida huwa ya gharama ya chini kutekeleza kwa sababu huwa wanatumia ama eneo bunge moja la kitaifa, kumaanisha kwamba hakuna mipaka ambayo inahitaji kuwekwa kamwe, au wilaya kubwa za uanachama zaidi ya mmoja ambazo (dovetail) hushikana na mipaka iliyokuwepo ya taifa au ya mikoa. Uchaguzi ambao ulifadhiliwa na umoja wa mataifa huko Sierra Leone mwaka wa 1996, Liberia mwaka wa 1997 na Kosovo mwaka wa 2001 ulifanyika chini ya mfumo wa Orodha ya PR ya kitaifa, kwa sababu kwa kiasi uhamishaji wa watu na ukosefu wa data halisi ya idadi ya watu nchini ilimaanisha kwamba viongozi wa uchaguzi hawakuwa na data ya idadi ya watu iliyohitajika katika uwekaji mipaka ya wilaya ndogo.

