Usajili wa wapigaji kura ni hatua changamano zaidi na yenye ubishi na kawaida yenye ufanisi wa chini katika uendeshaji wa shughuli za uchaguzi. Kutokana na shughuli zinazohusika, unahusu ukusanyaji wa habari maalum kwa njia iliyosawazishwa kutoka kwa idadi kubwa ya wapigaji kura na baadaye kupanga na kusambaza data hiyo katika hali inayoweza kutumiwa wakati wa uchaguzi zaidi katika njia ambayo huhakikisha kuwa wapigaji kura halali pekee hushiriki katika mchakato wa upigaji kura na kuzuia dhidi ya upigaji kura zaidi ya mara moja, kutumia watu wengine wasiosajiliwa kupiga kura n.k. Jambo lenye kuibua hisia za kisiasa kuhusu masuala haya na hali ya ugumu wa kazi yenyewe humaanisha kuwa usajili wa wapigaji kura kwa kawaida ni mojawapo ya hatua ya gharama ya juu, yenye kuchukua muda mwingi na yenye utata katika mchakato mzima wa uchaguzi.
Mahitaji ya usajili wa wapigaji kura huathiriwa na muundo wa mfumo wa uchaguzi. Mfumo ambao hutumia wilaya za uanachama mmoja kawaida huhitaji kila mpigaji kura awe amesajiliwa katika eneo lenye mipaka ya wilaya maalum. Hii humaanisha kwamba mifumo ya FPTP, AV, TRS na BC (wakati inapotumia wilaya za uanachama mmoja) huwa ya gharama ya juu zaidi na yenye kuchukua muda mwingi kuendesha wakati wa usajili wa wapigaji kura, pamoja na mifumo ya MMP ambayo huwa na wilaya za uanachama mmoja. Wilaya chache zenye uanachama zaidi ya mmoja zenye mifumo ya BV, PBV, SNTV na STV hufanya mchakato huu kuwa rahisi kidogo, huku mifumo ya PR yenye wilaya kubwa huwa na uchangamano mdogo.
Mipango ya usajili kwa upigaji kura nje ya nchi huweza kuwa si rahisi. Usahili wa mfumo wa orodha ya PR. Katika muktadha huu umekuwa ukichangia katika matumizi yake katika baadhi ya uchaguzi mkuu wa kuleta mabadiliko kama vile katika uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia huko Afrika Kusini mwaka wa 1994, inastahili kusisitizwa, hata hivyo, kwamba tofauti kati ya mifumo ya uchaguzi huwa tu na athari ndogo kwenye gharama ya juu zaidi ya usajili wa wapigaji kura.

