Misisitizo ambayo kila mfumo wa uchaguzi huwekewa kuhusiana na uwezo wa kiutawala wa nchi kimsingi huamuliwa na historia, muktadha, tajriba na rasilimali, lakini kwa mtazamo wa haraka kuhusu gharama tofauti na mambo ya kiutawala hutoa dalili/ishara kuhusu gharama inayowezekana kuhusu mifumo tofauti. Mifumo ya orodha ya PR hasa mifumo ya orodha funge ya kitaifa huwa na alama za juu ikitazamwa kulingana na gharama ya chini na huhitaji rasilimali kidogo ya kiutawala, vivyo hivyo katika PBV. Hufuata mifumo ya SNTV na LV, kisha BV na FPTP na chini zaidi mifumo ya AV, STV, Sambamba, Borda Count na MMP. Mfumo ambao una uwezekano mkubwa wa kuwa na msukumo mkubwa kwenye uongozi wa nchi yoyote ni mfumo wa Awamu-mbili.
Jedwali 8: Gharama Inayowezekana na Athari za Uongozi za Mifumo 12 ya Uchaguzi

