Halmashauri
za kusimamia uchaguzi zina uwezo wa kutoa amri zinazonuiwa kudhibiti masuala ya
uchaguzi. Mapatano ya kimataifa kati ya viongozi wa uchaguzi (ya utawala ama
kisheria) ya nchi tofauti yamekuwa muhimu sana katika kuleta muungano wa kimataifa
na miradi ya pamoja ya kiakademia, uchapishaji ama utafiti, zote ambazo
zimefanywa kupitia kongamano muhimu semina, mabaraza, warsha na machapisho
kuhusu mada za uchaguzi.
Makubaliano
ya kimataifa yaliyopigwa sahihi na viongozi wa uchaguzi hayana hadhi sawa ya
kisheria na hukumu za kimahakama. Licha ya hayo ni muhimu kwa kuwa yanayafunga
nchi zilizotia sahihi kwa njia rasmi. Pindi mapatano ya uchaguzi yanapoafikiwa,
majukumu na haki hupatikana na bidii inafaa kufanywa ili kuafikia malengo ya
mapatano. Mapatano ya kimataifa (na mapatano yasiyo ya uchaguzi) yanaweza
kutazamwa kama njia maalumu ya kuibua sheria za uchaguzi katika taratibu za
kijumla zinazolazimu suluhisho za kiulimwengu kwa matatizo ya kiulimwengu.
Mapatano ya
kimataifa lazima yapigwe sahihi na viongozi wenye mamlaka ya kufanya hivyo.
Lazima yaambatane na kanuni zilizoko. Mapatano yasiyo ya kikatiba ama yasiyo
halali ni bure. Makubaliano yanayokiuka kanuni zilizowekwa katika mikataba
mingine lazima zibatilishwe vilevile.
Katika
mifumo ya majimbo, mkubaliano kuhusu uchaguzi hufikiwa na viongozi wa viwango
tofauti (muungano, viongozi wa serikali na manispaa) na wamekuwa muhimu katika
kutatua masuala ya uchaguzi yanayowahusu (hasa masuala ya uatawala) kwa njia ya
kuungana. Mapatano kama hayo yamewafaidi wapigakura wenye maarifa na matumizi
kuhusu masuala yafuatayo: utawala, masuala ya katika uchaguzi na matumizi ya
kawaida ya orodha ya wapiga kura na vitambulisho vya kupiga kura (zote ambazo
ni ghali, kubwa za masuala changamano ya kiteknolojia yanabuniwa na
wakala za muungano za uchguzi na kusambazwa kwa wakala za mitaa zinazowahusu
katika uchaguzi wa mtaa.