Mara nyingi, sheria za uchaguzi za kuimarisha mifumo ya kidemokrasia zina uwili na hali ya kutotegemewa
- Kwa upande mmoja zinahusika katika mijadala ya kisiasa na kijamii inayosababisha upungufu wao kuzingatiwa zaidi kuliko ubora wao. Mara kwa mara hali kama hii huleta utata ambao unaweza kuelezewa kwa swali lifuatalo:
- Ni vipi mfumo wa uwiano unatuhumiwa ilhali utengano kati ya wapigakura na wagombeaji umependekezwa?
- Utafiti wa mfumo ulioimarishwa wa kisiasa unatoa wazo muhimu; mfumo wa uchaguzi unawezeshwa na kiwango muhimu cha uendelezo. Kanuni ya kimataifa inaweza kuwekwa kama ifuatavyo: Mifumo ya uchaguzi huimarisha misingi yao lakini inaweza kuimarishwa iwapo mfuno wa kisiasa unafikia upeo wa mgogoro
Hali kama hii inaafikiana na mabadiliko ya kiufundi, madogo na ya kitaratibu yanayoathiri sheria za uchaguzi. Miongoni mwa sababu zinazowezesha uendelezo wa kimsingi wa mifumo ya uchaguzi zinaweza kutajwa kama ifuatavyo:
- Kwanza, hakuna yeyote anayekuwa na hamu ya kubadilisha anachokijua ili achukue asichokijua.Wakala wowote wa mfumo wa uchaguzi wana hakika na utendakazi wa mfumo wao. Hakika kama hiyo haiwakatazi wananchi ama vyama vya kisiasa kuwa na maoni tofauti kuhusu mfumo huo.
- Pili, wale ambao wana uwezo wa kubadili sheria za uchaguzi ndio washindi wa uchaguzi.Wale ambao wamenufaika na mfumo uliopo ndio wanapaswa kupendekeza marekebisho yoyote.
- Mbali na hayo kuna ukweli wa kihistoria unaofanya marekebisho yawe magumu mno.Wananchi kwa kawaida huwa na mvuto kwa mifumo yao ya uchaguzi ya kijadi ambayo kwa maoni yao ndiyo inayowakilisha demokrasia.kadiri mfumo ulivyo mkongwe ndivyo ulivyo na mvuto kwa wananchi. Tamaduni huwalazimisha viongozi kuidhinisha vipengele vya kitamaduni ambavyo huonekana kuwa vya kijadi mahali kwingineko.
- Hatimaye kuna changamoto zinazotokana na kurekebisha sheria za uchaguzi. Kanuni muhimu za uchaguzi huwekwa na katiba na kuidhinishwa. Kutokana na ulinzi huu, sheria za uchaguzi zinaweza kurekebishwa tu na zaidi ya nusu ya watu. Ukweli kama huu unalazimu vyama vya kisiasa kufikia uelewano mpana na dhahiri kuhusu mada.
Licha ya hayo, marekebisho madogo kwa sheria za uchaguzi hufanywa mara nyingi. Sheria za uchaguzi katika demokrasia mpya na mifumo ya kidemokrasia iliyoimarishwa hurekebishwa mara kwa mara na kubadilishwa.