Ilivyopendekezwa katika sehemu za utangulizi za sehemu ya mada hii, utofautishaji unafaa kufanywa baina ya habari kwa mpiga kura, elimu kwa mpiga kura, na elimu kwa raia. Bila shaka, kila mmoja wepo inapatikana katika mwendeleo wa shughuli mbalimbali zinazo saidia katika shughuli za uchaguzi na demokrasia na zinatoshelezana. Na pia itakuwa ukweli kuchukulia kwamba elimu kwa mpiga kura, kwa mfano, inafaa kuwa sehemu ya Mpango mpana wa elimu kwa raia.
Hata hivyo, dhana hizi si lazima zitumike kiutoano na zinahusisha tofauti ndogo katika malengo, hadhira, ujumbe, mwelekeo, wakati, na / au wajibu wa kitaasisi. Kwa ufupi:
Taarifa za kimsingi kwa wapigakura inarejelea habari za kimsingi zinazo mwezesha mwana nchi aliyehitimu kupiga kura. Taarifa hizi ni pamoja na tarehe, wakati, na mahali pa kupigia kura, aina ya uchagusi, utambulishaji unaofaa kubainisha kuhitimu kwa mpiga kura, usajili unaohitajika na njia za kupiga kura. Haya yanajumuisha mambo ya kimsingi kuhusu uchaguzi huo na hayaitaji maelezo ya dhana. Ujumbe utundwa kwa kila uchaguzi. Shughuli hizi zinaweza kutekelezwa haraka (ingawa upangaji unaofaa bado unahitajika). Wenye mamlaka ya kusimamia uchaguzi wanaitajika kutoa habari za aina hii, ingawa wanaowania katika uchaguzi huo na miungano ya mashirika ya kijamii vile vile yatafanya hivyo.
Elimu ya kimsingi kwa Wapigakura hasa inazungumzia motisha walionayo Wapigakura na namna walivyojiandaa kushiriki kikamilifu katika chaguzi. Elimu inahusu habari changamano kuhusu upigaji kura na mchakato wa upigaji kura na inahusiana na dhana kama vile uhusiano uliopo paina ya haki za kibinadamu na haki za kupiga kura; kazi, wajibu na haki za Wapigakura; uhusiano baina ya chaguzi na demokrasia na masharti yanayofaa kwa chaguzi za kidemkrasia; usiri wa kura; sababu zinazomfanya kilampiga kura kuwa muhimu na athari zake kwa uajibikaji kwa umma; na namna kura zinavyo changia katika kushinda kiti. Dhana kama hizi zinahusisha maelezo, na wala sio kutaja kwa mambo tu. Elimu kwa mpiga kura inahitaji muda zaidi unaotangulia utekelezaji kuliko habari kwa mpiga kura na inafaa kuendeshwa katika hali ya kuendelea (bila kukatizwa). Aina hii ya habari mara nyingi hutolewa na wasimamizi uchaguzi na miungano ya mashirika ya kijamii.
Elimu ya kimsingi kwa raia huhusika na dhana pana zinazojenga jamii ya kidemokrasia kama vile majukumu mahususi na wajibu wa wananchi, serikali, makundi spesheli na ya kisiasa, vyombo vya habari, na sekta za kibiashara na zisizo za kibiashara na vilevile umuhimu wa chaguzi za mara kwa mara na zenye ushindani mkuu. Elimu hii inasisitiza sio tu uhamasishaji wa wananchi lakini pia kushiriki kwa wananchi katika maswala yote ya jamii ya kidemokrasia. Elimu kwa raia ni mchakato unaoendelea na ambao haujafungwa kwa kalenda ya uchaguzi. Hata hivyo habari kwa mpiga kura na elimu kwa mpiga kura zinaweza kuwa sehemu ya shughuli pana ya elimu kwa raia. Elimu kwa raia inaweza kuendeshwa kupitia kwa mfumo wa shule na chuo kikuu, kupitia kwa mashirika ya kutetea haki ya kijamii, na labda kupita kwa mashirika fulani ya kiserikali, ingawa sio lazima yawe ni mamlaka ya kusimamia uchaguzi.
Kuna baadhi ya sifa za habari na za kielimu ambazo ni za kawaida. Sifa hizi zinajadiliwa katika Sifa za Kawaida za Habari na Elimu kwa Wapigakura.