Muhtasari
Elimu inayosaidia uendeleza mchakato wa upigaji kura imekuja kujulikan kuwa “elimu kwa mpiga kura” ambapo mlengwa mkuu ni mpiga kura. Kuna sehemu zingine kadha za elimu zinazohitajika ili uchaguzi uweze kufaulu, lakini hizi zinaweza kutekelezwa na vyama vya kisiasa na maafisa wakusimamia uchaguzi. Kwa upande mwingine elimu kwa mpiga kura, inachukuliwa kuwa shughuli tofauti na ya kipekee. Huwa inatambuliwa kama shughuli ya wasimamizi wa uchaguzi na mara chache huwa inatolewa kama zabuni kwa kampuni za kibinafsi na mashirika ya kupigania haki za kijamii. Pia huwa inaendelezwa na mashirika spesheli ya umma na ambayo ni huru kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi.
Elimu kwa Wapigakura ni nini?
Kwa undani wake, elimu kwa mpiga kura ni shughuli ambayo imedhamiriwa kuhakikisha Wapigakura wako tayari, wanakubali, na wana uwezo wa kushiriki katika siasa za uchaguzi. Imechukuliwa kuwa shughuli hii inahusisha elimu ya uchaguzi na imani kuwa mchakato wa uchaguzi unafaa katika kuchagua serikali na kuimarisha sera ambazo zitafaa mpiga kura kibinafsi.
Je, Elimu kwa Wapigakura inatosha kueleza Demokrasia?
Kama ilivyoelezewa kwingineko katika eneo hili la mada, elimu kwa mpiga kura in muhimu katika kuhakikisha kuwa Wapigakura wanaweza kutumia haki zao za kupiga kura vilivyo na kudhihirisha matamanio yao ya kisiasa kupitia kwa mchakato wa uchaguzi. Kama Wapigakura hawako tayari au hawana motisha ya kushiriki katika uchaguzi, maswali yataanza kujitokeza kuhusu uhalali, uwakilishaji, na uajibikaji wa viongozi na taasisi zilizochaguliwa. Wakati huo huo, elimu kwa mpiga kura ni shughuli inayohitaji umakinifu. Inawalenga Wapigakura ambao wamehitimu na ushughulikia matukio mahususi ya uchaguzi na vilevile mchakato wa uchaguzi kwa ujumla. Ingawa elimu kwa mpiga kura ni sehemu muhimu ya mchakato ya uchaguzi wa kidemokrasia, hautoshelezi demokrasia.
Elimu kwa mpiga kura inafaa kutiliwa nguvu na juhudi endelevu za elimu kwa raia ili kufanikisha utamaduni wa kidemokrasia unaotokana na chaguzi za mara kwa mara. Elimu kwa raia inahusisha mtazamo mkubwa kuliko elimu kwa mpiga kura. Elimu kwa raia inahusika na wananchi, na wala si Wapigakura tu, na inasisitiza uhusiano baina ya wananchi wenye bidii na jamii ya kidemokrasia. Inaeleweka kuwa wananchi wanafaa kuhusika katika mchakato wa kisiasa mara kwa mara, sio tu wakati wa uchaguzi (Tazama Elimu kwa Raia).
Bila shaka, kushiriki katika chaguzi na hali ya mpiga kura ina uzito katika nchi zinazotekeleza mabadiliko na ambazo zinafanya chaguzi zao kwa mara ya kwanza na pale ambapo haki ya kupiga kura imepatikana kupitia mvutano wa kijamii. Wakati ambapo ulimwengu wa kidemokrasia unaelekea kukubalia haki kamili ya uraia kwa kila mtu, hata hivyo, upigaji kura unatazamwa kama mojawapo ya njia nyingi ambazo wananchi wanashiriki katika kuunga mkono demokrasia.
Ulinganisho wa Kimataifa
Upeo wa juhudi za elimu kwa mpiga kura zinazohitajika katika nchi yoyote ile utategemea mambo mbalimbali. Je, nchi inahistoria ndefu ya chaguzi za kidemokrasia, au huu ni uchaguzi wa kwanza au wa mpito? Je, usajili wa Wapigakura ni wa lazima au wa hiari? Ni nani aliye na jukumu la kuwasajili Wapigakura? Je, upigaji kura umepanuliwa ili kuhusisha makundi mapya ya Wapigakura? Je, kumekuwepo na mabadiliko yoyote kwa mfumo wa uwakilishi au mchakato wa upigaji kura? Je, watu wana imani katika mchakato wa upigaji kura na taasisi za kisiasa? Je, kampeni ya uchaguzi ni wazi na ya kushindaniwa? Je, juhudi za kuwaelimisha Wapigakura zimefanywa wakati uliopita? Je, kuna juhudi za kuelimisha raia zinazoendelea? Majibu kwa maswali haya na mengine yataathiri hali ya Mpango wa elimu kwa Wapigakura na umbali ambao Mpango huu utafika.
Ujumbe na Mbinu
Kuwasaidia wananchi kuelewa kushiriki katika uchaguzi, sio tu kama mgombezi au mfuasi wa mgombezi kunahitaji kumakinikia mambo kadha. Haya yanaonekana kuwa na umuhimu fulani kote ulimwenguni, ingawa kila uchaguzi unaweza kuwa na sifa zake maalum.
Waelimishaji pia watazingatia masuala ya kimethodolojia na haya yameelezewa katika Sifa Muhimu za kuzingatiwa katika Mpango. Sifa mbalimbali za Mpango zinaweza kuafiki kwa kutegemea malighafi yaliyopo na malengo yaliyowekwa na shirika linalotoa elimu, au shirika linalofadhili Mpango. Tofauti za kimethodolojia zilizopo zinaashiria kuwaelimu kwa mpiga kura inajikita kati ya dhana mbili “Habari kwa Mpiga kura” na “Elimu kwa Raia”.
Je, ni Wajibu wa nani?
Ingawa habari kwa mpiga kura ni jukumu la wasimamizi wa uchaguzi, elimu kwa Wapigakura inaweza kutazamwa kama jukumu la wasimamizi wa uchaguzi na vilevile na mashirika ya kijamii. Mawakala mbalimbali wa serikali vilevile yanaweza kuwa na jukumu katika kuwafahamisha na kuwaelimisha wananchi. Kazi ya wasimamizi wa uchaguzi au mawakala wengine wa serikali inaweza ikaamuliwa kupitia kwa sharia, wakati ambapo mashirika ya kupigania haki za kijamii yanaweza kumakinikia uelimishaji wa Wapigakura na ushiriki katika siasa.
Kwamba kuna haja ya kuwaelimisha watu ili kushiriki katika uchaguzi si suala. Kwa kutegemea ikiwa watu hawa ni watoto au watu wazima, kuna mahitaji mengi ya kielimu ambayo yanahusiana na maadili ya uchaguzi. Lakini pia kuna mahitaji yanayohusiana na kushiriki kwa bidii katika siasa za ushindani. Shughuli moja ya kielimu inahusisha matumizi ya chaguzi wa majaribio au sambamba. Katika nchi ya Chile, kwa mfano, watoto huandamana na wazazi wao katika vituo vya kupigia kura katika siku ya uchaguzi na kupiga kura katika uchaguzi sambamba. Katika hali zingine, shughuli za chaguzi za majaribio zinaweza kwa ufinyu kuangazia suala la mienendo ya upigaji kura au kuhusisha shughuli nzima ya kampeni ya uchaguzi. Kuwapa nafasi watoto kugombea chaguzi au kuwapigia kampeni wengine kunatoa mafunzo muhimu ambayo hayawezi kufunzwa kupitia kwa njia ambazo zinatilia mkazo shughuli za siku ya uchaguzi.
Malengo ya Elimu ya kidesturi kwa Wapigakura
Elimu ya kidesturi kwa Wapigakura inalenga kutayarisha hali ya ufahamu ili kuwawezesha Wapigakura watarajiwa kushiriki katika uchaguzi ujao. Pia inalenga kuwawezesha Wapigakura watarajiwa kupiga kura zao kwa matumaini.
Malengo haya yanaweza pia kufikiwa kupitia kwa mbinu zingine, na waelimishaji watataka kuazisha mipango ambayo inafanya kazi pamoja na mbinu ambazo zinashughulikia masuala kama vile usalama wa mpiga kura, taratibu za kimsingi za kupiga kura, vituo vya kupiga kura vinavyo weza kufikiwa na kampeni changamfu lakini zisizokuwa na vurugu na za kutisha kwa upande wa wagombezi.
Kusawazisha mipango ya elimu kwa Wapigakura dhidi ya mbinu hizi zingine ni muhimu katika uhakikishaji kuwa bajeti hazifanywi kuwa za juu. Gharama za mipango ya elimu kwa Wapigakura zinaweza na zinafaa kufanywa katika misingi ya gharama kwa kila mpiga kura.Tunaweza kudai kuwa na vilevile imedaiwa kuwa chaguzi hata ziwe ghali namna gani ni nafuu kuliko vita au vita vya kijamii visivyokoma. Huu ni ukweli, lakini nia ya chaguzi za kidemokrasia ni kuhakikisha kuwa chaguzi za mara kwa mara zinaendelea, na hii haiwezikufanyika kwa ubadhirifu milele. Gharama zinafaa kuchunguzwa kwa makini na mipango kuundwa ambayo inapunguza gharama. Wakati mwingine hii inaweza kuhitaji kupunguza malengo ambayo yanafaa kuafikiwa na Mpango ili kuwa na uchaguzi unaopendeza au unaofaa.
Wakati wa kutoa Habari
Wakati wa kutoa habari kwa Wapigakura unaweza kuwa au kutokuwa sawa na ule waMpango wa habari kwa Wapigakura. Ingawa inaweza kutekelezwa kwa wakati huo huo katika viwango fulani. Kihalisi, wakati wa Mpango wa elimu kwa Wapigakura unaweza kutegemea muda wa Mpango, taasisi inayoshughulikia Mpango, kazi ya taasisi, vigezo vya Mpango, aina ya vifaa vya maagizo vinavyo undwa na mahitaji ya kundi lengwa.
Katika mazingira ambapo hakuna wasimamizi wa uchaguzi wa kudumu na pale ambapo vifaa ni pungufu, Mpango wa elimu kwa Wapigakura unaweza tu kuendeshwa wakati huo huo wa uchaguzi na pamoja na juhudi zingine za utoaji habari kwa mpiga kura. Katika hali zingine, elimu kwa Wapigakura inaweza kuanzishwa mapema kidogo kuliko habari kwa mpiga kura, hasa ikiwa mabadiliko makubwa yanafanywa kwa mfumo wanchi wa uwakilishi na mipaka ya kisheria ya chaguzi, pale ambapo upigaji kura unapanuliwa, na pale ambapo mabadiliko muhimu yanafanywa kwa mchakato wa kisiasa na uchaguzi. Hata hivyo, katika nchi ambapo demokrasia imekuwepo kwa muda mrefu na pale ambapo panatume ya kudumu ya kusimamia uchaguzi na vifaa vya kutosha, eimu kwa Wapigakura inaweza kuwa shughuli ambayo inaendelea wakati wote. Kwa kutegemea kazi ya wasimamizi wa uchaguzi na lengo la shirika fulani la kupigania haki za kijamii, elimu kwa Wapigakura inaweza kushughulikiwa kwa kupitia kwa Mpango mpana wa elimu kwa raia kama sehemu yake.
Ikiwa itatekelezwa katika mfumo mzima wa shule, kozi fupi ya elimu kwa Wapigakura inaweza pia kuhusishwa kama sehemu ya mpangilio mpana wa elimu kwa raia. Kozi hii inaweza kutolewa kwa watoto wa miaka mbalimbali, au tu kwa wale ambao wanakaribia kutimiza umri wa kupiga kura. Muda wa jumla unaotumika kwa elimu kwa Wapigakura katika hali hii unaweza vilevile kutegemea upana na kina cha kozi inayohusika. Uigizaji, kampeni na chaguzi za majaribio, na mazoezi ya kutoa mafunzo darasani na nje ya darasa yanaweza kuhusishwa. Shughuli zinaweza kutengewa darasa mahususi au kuhusisha madarasa yote na viwango mbalimbali. Pia kunaweza kuwa na mashindano baina ya shule. Kadri kozi ilivyo changamano na toshelevu, ndivyo itakavyohitaji muda zaidi. Maelezo zaidi kuhusu maigizo yanaweza pia kupatikana chini ya Maigizo.
Ujumbe Wastani kwa Wapigakura
Waelimishaji wa Wapigakura hutumia ujumbe fulani wastani. Kufanya ujumbe kuwa wastani kunamaanisha mambo mawili:
- Sifa fulani muhimu za ujumbe lazima zielezwe / zifafanuliwe
- Nyaraka iliyo na ujumbe inaweza kutolewa tena au kutolewa nakala kama ilivyo au yaweza ikabadilishwa upya kwa usambazaji zaidi.
Kuna ujumbe wa aina nne za kijumla ambazo mipango yote ya elimu kwa Wapigakura itaeleza. Hii itahitaji kuwa waelimishaji wafanye kazi na wataalamu walio na ujuzi na maarifa ili kuhakikisha kuwa ujumbe unajadiliwa katika njia ambazo zina umuhimu kwa nchi mahususi ambayo demokrasia inatengenezwa. Kila nchi ina historia yake, na historia hii inatoa masuala ya kuzingatiwa na maelezo kuhusu asili ya demokrasia na vilevile masuala madogo ya kimpangilio na kimaadili ambayo yatahitaji kushughulikiwa kwa njia tofauti kutoka kwa yale yaliyoundwa hata katika nchi jirani. Hata hivyo, ni jambo linalowezekana kuelezea masuala ambayo yanatarajiwa kuzungumziwa katika kila sehemu.
- Chaguzi na Demokrasia. Ni vigumu kuwaziakuwepo kwa demokrasia katika shirika kubwa na la kisasa au jamii bila ya mfumo unaoimarisha mashirika makubwa ya wananchi kupitia kwa taratibu za upigaji kura. Chaguzi ni mojawapo ya matukio muhimu yanayotambulisha demokrasia za kisasa, na pamoja na chaguzi za mara kwa mara na za haki, kunamaanisha kuongezeka kwa mahitaji kuwa wananchi watakuwa na nafasi ya kuchagua kati ya watu binafsi, vyama, na sera. Pia watakuwa na uhuru wa kuchagua bila ya vitisho visivyotarajiwa, na watakuwa na haki ya kujiweka wao wenyewe au watu wengine mbele kwa uchaguzi wa ofisi mbalimbali. Hatimaye, watakuwa na uhuru unaohitajika kujadili masuala ya sera na kuunda mashirika ambayo yatashindana katika uchaguzi, yataunga mkono wagombezi au vyama fulani, na / au kuwapa habari na mijadala wanayohitaji ili kufanya uamuzi wao wanapopiga kura. Pia watakuwa na uhuru wa kutembea kila mahali wakifanya kampeni kwa niaba ya mgombezi wao kote nchini.
Uimarishaji wa mawazo haya ni muhimu, kwa sababu kuna uwezekano kuwa kutakuwa na wale ambao watafikiria kuwa uchaguzi unaweza kuendelezwa bila ya kuwepo masharti kama hayo. Nchini India, lazima wasimamizi wa uchaguzi watathmini iwapo masharti kama hayo yapo kukubali uchaguzi kuendelea. Lakini kumekuwepo na wakati mwingine, katika sehemu zingine, ambapo uchaguzi umetumiwa kuendeleza uaminifu na uhalali wa serikaliambayo haina nia ya kuakikisha kuwepo kwa haki muhimu za kidemokrasia wakati wa kipindi cha uchaguzi.
- Jukumu, wajibu na haki za mpiga kura. Sehemu ya pili ya ujumbe inatoa motisha kwa wananchi kushiriki katika chaguzi. Wananchi wanapata kujifunza jinsi ushiriki katika uchaguzi na watu binafsi kunavyoweza kuchangia katika uundaji wa serikali ya uwakilishi na kuhakikisha uajibikaji wa wale wanaochaguliwa.
Hata hivyo, haitoshi tu kumakinikia majukumu na wajibu. Lazima waelimishaji wazingatie haki za watu kwa uchaguzi huru na wa haki. Kuwasaidia Wapigakura kuelewa haki hizi kunachangia katika kufuatilia kwa uchaguzi na wananchi wote na sio tu makundi maalumu. Inahakikisha uangalizi wa wagombezi na wasimamizi wa uchaguzi.
- Kura yako ni muhimu. Ingawa mifumo yote inaelezea kanuni kila kura ni muhimu, kuna tofauti chache katika ujumbe kwa kutegemea iwapo mifumo ya uwakilishi ya kwanza iliyopita au sawazishi inatumika. Katika mifumo ya kwanza, kufana au kufeli kwa shughuli ya uchaguzi kunaweza kuamuliwa na idadi ndogo ya kura ambapo kutakuwa na mshindi aliyeshinda kwa kura chache na mshindwa. Katika mifumo ambayo inatumia vipimo, kila kura ni muhimu katika kuongezea ukubwa wa kiwango cha uwakilishi wa mgombezi anayependelewa na mpiga kura.
Mbali na idadi ya kura, Wapigakura wanafaa kufahamishwa kuwa kila kura ina uzito katika kuamua haki walizo nazo juu ya chama kilichochaguliwa au mwakilishi baada ya kushinda au kushindwa katika uchaguzi. Ikiwa uhusiano wa wawakilishaji hauwezi kutengenezwa kati ya wananchi na maafisa waliochaguliwa, wananchi wanaweza kuanza kuhisi kuwa kura yao haina umuhimu mkubwa.
- Kura yako ni siri. Kuna hali nyingi ambapo ni muhimu kuwa Wapigakura walindwe dhidi ya vitisho na woga unaotokana na athari za kisiasa na kibinafsi. Katika hali kama hizi, ujumbe kuwa kura ni siri unafaa kuelezwa na, kwa kiwango ambacho kinaweza kuthibitishwa. Usiri una vidokezo chanya na hasi, na katika jamii ambazo zinathamini umoja wa kijamii, usiri unaweza kushukiwa. Au kunaweza kuwa na jamii ambazo zinachukulia usiri kuwa jambo ambalo haliwezekani, labda kutokana na utawala uliofeli au miundo ya kiimani iliyopo.
Katika hali hizi, mifano ya mambo ambayo ni siri, au yale ambayo hayawezi kujulikana, yanaonyesha waelimishaji sitari zinazoweza kuibuka katika mchakato wa kupiga kura. Na kunaweza na mitazamo badala. Labda mtazamo wenye nguvu zaidi ni wakati ambapo chaguzi zinarudiwa na hakuna athari zozote hatari zinazowapata Wapigakura. Lakini sharia za uchaguzi zitahitajika kuupa nguvu ujumbe kwa kuzingatia kwa umakini jinsi kuhesabiwa kwa kura kutafanyika na matokeo kutangazwa. Kura ya mtu binafsi inaweza kuwa siri, lakini mapendeleo ya jamii huenda yasiwe, na ii inaweza vilevile kuwa na athari muhimu.
Jumbe Nyingine
Vilevile, kila uchaguzi utakuwa na nyongeza ya seti ya ujumbe wastani ambao unafaa kwa uchaguzi mahsusi. Katika hali nyingi, ujumbe huu utahusisha kauli ya kunata ambayo itatumika katika taarifa fupi kama vile vibandiko, mabango, na mavazi. Ujumbe huu unafaa kuandaliwa na waelimishaji katika mtindo ambao unaweza kutumika kwa wingi. Wanaweza pia kuunda sehemu ya hifadhi ya data kwenye faksi ili waelimishaji ambao wanaweza kufikia vifaa vifaavyo vya simu na faksi wanaweza kubonyeza na kupata nakala za ujumbe kwa matumizi zaidi na usambazaji. Nchi zilizo na uwezo wa kutumia wavuti na barua pepe zinaweza kufanya usambazaji kupitia njia hizi.
Pamoja na ujumbe huu wastani, kuna kifaa cha ujumbe wastani kingine ambacho kimepata umaarufu zaidi na hata kinaweza kuwa kilicho muhimu zaidi na nyaraka ambayo imesambazwa zaidi na Mpango wa elimu. Hii ni Makala yenye Maswali Yanayoulizwa mara kwa mara.
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara
Kuanzia mwanzoni mwa shughuli ya uchaguzi, waelimishaji wataanza kukusanya orodha ya maswali yanayoulizwa katika warsha, kupitia kwa simu zinazo pigwa, na maafisa wa uchaguzi wakati wanaposajiliwa na kupewa mafunzo. Maswali haya yanafaa kuorodheshwa na kupangwa katika kategori mbalimbali.Wakati ambapo kuna orodha ya kwanza ya maswali karibu kumi, majibu mwafaka yanafaa kuandaliwa na nyaraka yenye swali likifuatiwa na jibu itolewe katika njia nyingi zaidi iwezekanavyo.
Orodha hii ya maswali ambayo yanaulizwa mara kwa mara inaweza kufanyiwa marekebisho mara nyingi wakati wa uchaguzi. Maswali zaidi yataongezwa, na habari zaidi zitatolewa ambazo zinaweza kubadilisha majibu yaliyopo au kuyaongezea. Mtu mwingine anafaa kupewa kazi ya kuakikisha kuwa orodha ni sahihi na kuisambaza.
Kwa sababu itabadilika mara kwa mara, na inaweza kutumwa kwa njia ya faksi, au barua pepe au ya kusambazwa katika warsha za mafunzo, ni muhimu kuwa kila toleo lipewe nambari, tarehe, na kuhakikisha kuwa inatolewa kwa wakati ufaao katika siku za mwisho katika kila uchaguzi. Ikiwa maswali yanayoulizwa mara kwa mara yanaandaliwa na shirika au na wasimamizi wa uchaguzi, inafaa kuwa na jalada ambalo linatoa maelezo yote ya kina kuhusu shirika ambalo liliyaandaa na kuyasambaza, pamoja na njia za kuweza kuwasiliana nao moja kwa moja kwa habari zaidi.
Kunaweza kuwa na maswali yanayoulizwa mara kwa mara tofauti na yanayowalenga wasimamizi wa uchaguzi na waelimishaji. Ni muhimu kuelewa kuwa watu tofauti wana maswali tofauti. Bila kujali hai, mukhtasari huu wa maoni mbalimbali ambayo watu wako nayo kuhusu uchaguzi na maswali majibu mafupi itakuwa kifaa ambacho kina weza kuwa na athari ambayo itakuwa na umuhimu zaidi ya kuhalalisha gharama za kuundwa kwake.