Kuna tofauti kadha muhimu kati ya shughuli za habari kwa mpiga kura, elimu kwa mpiga kura na elimu kwa raia, ilhali wakati huo huo aina moja ya elimu inaweza kuingiliana vizuri na nyingine na, katika hali nyingi, inaweza kuwa sehemu ya juhudi pana.
Wakati huo huo, kuna sifa fulani ambazo ni za kawaida kwa habari kwa mpiga kura na elimu kwa mpiga kura kwa pamoja. Zote zinafaa kuhusisha toleo lao la kalenda na ratiba ya uchaguzi. Zote zinaweza kutumia washika dau mbalimbali, vikiwemo vyama vya kisiasa (Tazama Vyama vya Kisiasa katika Elimu kwa Mpiga kura), maafisa wa uchaguzi (Tazama Maafisa wa Uchaguzi katika Elimu kwa Mpiga kura), na au sekta ya mshirika ya kijamii ili kuongeza ueneaji wa Mpango na kuimarisha ubora wake. Wote watajiusisha na sio tu upigaji kura katika siku ya uchaguzi, bali pia Usajili wa Wapigakura. Na hatimaye, wote watafaa kuzingatia njia ambazo Maeneo ya Kupigia kura yanaweza kutumiwa kupunguza gharama na kuboresha ufanisi wa Mpango.
Kutokana na mwingiliano huu, sehemu hii ya mada inashughulikia habari kwa mpigakura na elimu kwa mpiga kura kwa ushanjari isipokuwa pale ambapo itaelezwa tofauti. Elimu kwa raia si swala kimsingi linaloangaziwa katika eneo hili la mada lakini inachukua sehemu yake kubwa pekee. Kwa kuwa habari kwa mpiga kura na elimu kwa mpiga kura mara nyingi huwa ni sehemu muhimu ya mipango ya elimu kwa raia, baadhi ya mambo yanayotokana na elimu kwa raia yamehusishwa katika sehemu inayoonyesha vifaa (vya kimaandishi) vinavyotumika kama mifano.