Waelimishaji wa wapigakura wanapaswa kuwa na uwezo wa kufikia nyenzo zilizotayarishwa kwa shughuli za kuelimisha wapigakura hapo awali ama katika nchi yao au katika mazingira mengine. Wanaweza pia kuwa waliomba watoa huduma katika shughuli hizo kuwapa nyenzo za kutathminiwa au ili waweze kutoa na kusambaza baadaye.
Kuna shughuli za kijumla kuhusu tathmini ya mitaala zinazopaswa kufanywa na vilevile shughuli za kukubali kutumia mpango huo, ambazo zinapaswa kufanywa kabla ya kutekeleza shughuli za mafunzo au uelimishaji.
Tathmini ya nyenzo haiwezi kufanyika hadi pale ambapo malengo ya mpango huo na malengo ya vipengele mbalimbali vya mpango huo yameelezwa wazi. Haya yakikosekana, hakutakuwa na lengo la kismingi la kufanyiwa tathmini.
Malengo haya yakiwepo, inawezekana kutathmini nyenzo kwa misingi ya mambo yafuatayo:
- ufaafu wake katika kuafiki malengo hayo kwa hadhira lengwa haswa
- gharama yake kwa misingi ya gharama ya kutayarisha nyenzo maalumu na mpya
- uwezo wa waelimishaji waliopo kutumia nyenzo hizo
- uwezo wa kuingiana na hali za maeneo hayo
Uwezo wa kuingiana na hali za maeneo hayo unaweza kujumuisha kutafsiri nyenzo hizo, kubadilisha michoro inayoelekea kuonyesha picha Ulaya na kuweka michoro ya eneo hilo, kulazimika kusahilisha lugha, au kulazimika kubadilisha nyenzo hizo ili ziafiki hali za maeneo hayo, ikiwa ni pamoja na tofauti katika mazingira ya kisiasa.
Ikiwa nyenzo hizo zitatumiwa katika mazingira ya warsha na wafundishaji wa maeneo hayo, inawezekana kuchukua sehemu Fulani, pengine kwa kuipa hadhira na vifaa vinavyoweza kutazamwa. Ikiwa nyenzo hizo lazima zitumwe nje kwa misingi ya matumizi ya kibinafsi au kuonyeshwa, sehemu yake Fulani inaweza kuchukuliwa na inaweza kuwa nyenzo zilizotolewa zinamatumizi tu kama mwongozo wa kuongoza utoaji wa kibinafsi.
Bila shaka, nyenzo ambazo ziko karibu na nyumbani zinaweza kuwa muhimu na rahisi kuchukuliwa. Zile zilizotolewa katika chaguzi za awali katika nchi hiyo zinaweza kuchukuliwa kuwa bora kabisa, japo uzingatifu unapaswa kuchukuliwa kwamba tathmini ya shughuli za kutathmini mipango hiyo na kupanga malengo yanafanya hata kabla ya kuzingatia nyenzo hizi. Nyakati hubadilika, wakati mwingine vilivyo.
Inaweza pia kuwa na faida kuona tathmini yoyote iliyofanywa kuhusiana na nyenzo hizo baada ya kutumiwa mara ya kwanza.
Kuidhinisha Nyenzo za Kutumiwa kwa Shughuli Maalumu
Waelimishaji wengi wanapaswa kuchukua nyenzo zilizotayarishwa kwa jumla na kisha wakapewa ili wazitumie. Hii inarejelea mpango wa kitaifa uliotayarishwa kulingana na mpango uliotengenezwa taratibu. Kwa sababu hii, mafundisho ya waelimishaji yanapaswa kujumuisha habari kuhusu kuidhinisha sehemu hii katika eneo hilo.