Upatikanaji wa bidhaa na huduma huhitaji:
- ujenzi wa mahitaji
- ombi la kupewa bidhaa
- kupata msururu wa vidondozi au kuweka mahitaji hayo kwa mkataba,
- mchakato wa kufanya uamuzi kuhusiana na tathmini ya kibinafsi ya mtoa huduma mwafaka.
Mashirika na serikali huelekea kuwa na taratibu na viwango kuhusu bidhaa zinazonunuliwa: nyenzo, machapisho, samani, tarakilishi na vifaa vya kutoa sauti na picha. Hivi ni pamoja na kugawa taratibu hizi kutegemea gharama, pamoja na viwango vinavyoongezeka vya uidhinishaji na urasmi. Wanaweza pia kuwa na orodha ya watoa huduma waliokubali (tazama hapo chini). Kunaweza pia kuwa na mazingatio maalumu ambayo waelimishaji wanaweza kuzingatia na sehemu hii inarejelea haya hasa.
Maendeleo na Hatua ya Uthibitisho
Katika baadhi ya nchi, kunaweza kuwa na njia zaidi zilizopangwa kuendeleza maendeleo ya nchi. Kwa mfano, ununuzi unaweza kuwa na mapendeleo ya kuegemea makampuni na mashirika ya maeneo hayo, au makampuni madogo, au makampuni ambayo wengi wa wamiliki wake ni wanawake au makundi yaliyotengwa. Pale ambapo hapana sheria kuhusiana na hili, halmashauri ya kusimamia uchaguzi inaweza kuamua hatua yake na katika njia hii kuhimiza au kukuza usawazishaji wa mamlaka na utajiri, ambamo demokrasia inapatikana kwa urahisi.
Taratibu za Kijumla
Katika visa vingine, kanuni za kuongoza ununuzi hufanya kazi kwa watoa bidhaa na huduma za viwango vya juu ofisini.
Kunaweza kuwa na utohakika kuhusu utoaji wa huduma za kitaalamu ikiwa mbinu hafifu za utiifu zinatumiwa kuharakisha michakato hiyo, au kushinda vikwamizi vinavyodhaniwa kuwepo katika idadi hiyo na ubora wa watu waliopo.
Hata ikiwa bidhaa au huduma hizo zinanunuliwa kutoka nje, kuna mipangilio ya kuongoza utoaji tenda (ushindani katika maombi ya tenda) inayoweza kutumiwa ili kuhakikisha kwamba mtoa huduma bora anapatikana kwa bei mwafaka na bila shirika hilo kuonekana kukosa haki au kupendelea wale wanaoweza kuwa na nafasi kubwa kwa sababu ya mahusiano ya kifamilia au kisiasa.
Mielekeo Inayowezekana
Hatua mojawapo inayoweza kuharakisha mchakato wa ununuzi huku ikiifanya shughuli hiyo kuwa na haki ni kuweka mbinu Fulani ya kijumla mapema na kuhakikisha kwamba orodha ya watoa huduma watarajiwa imejengwa. Orodha hiyo ikiwepo, maombi ya tenda yatafunguliwa na kutolewa kwa wale walio kwenye orodha hii na uteuzi kufanywa kutoka kwenye orodha hiyo.
Kuingia katika orodha hiyo kunaweza kumhitaji mtoa huduma kuonyesha umulisi wake, kupitia mahitaji Fulani ya kimsingi, ambayo yanaweza kujumuisha kuzuru eneo la kazi hiyo, kutoa habari kuhusu kampuni, na pengine alivyofanya kazi au kutoa huduma katika siku zilizopita.
- Taarifa za kabla ya Kutuma maombi.
Ikipendelewa kufungua ushindani uwe mkubwa iwezekavyo, na si kutenga wale ambao huenda pale awali walishindwa kushiriki katika shughuli zinazoibuka, au katika nchi zinazowazuia watu wengine kuunda makampuni au mashirika inawezekana kusawazisha kinyanyiro hicho kwa kuomba watoa huduma wote wanaoweza kuwa na nia kuhudhuria vikao vya kupewa taarifa ambapo habari hutolewa kwa wote na maswali yanaweza kuulizwa.
Tenda hutolewa tu baada ya kupewa taarifa hizi, na masharti yatakayozingatiwa katika kutathmini tenda hizo kueleweka na watu wote.
- Watoa huduma Wanaotambulika.
Kwa sababu mbalimbali, kunaweza kuwa na shughuli Fulani maalumu na mahusiano ya kibiashara ya muda mrefu ambayo huishia katika mashirika kuweka orodha ya watoa huduma wanaotambulika. Ikiwa orodha kama hiyo itajengw, kunapaswa kuwa na mabadiliko ya mara kwa mara katika bei, tathmini ya ubora, na nafasi ya watoa huduma wapya kuingia katika orodha hiyo.
Orodha hiyo inaweza kufunguliwa kwa sehemu Fulani na mkakati ufuatao, japo kunaweza kuwa na kidhibiti kuhusu muda ambao kampuni hiyo inapaswa kuendelea kuwa kwenye orodha hiyo.
Kutenga Bidhaa na Huduma
Wale wanaowajibikia ununuzi wanaweza kuyavunja maombi yao katika mafungu madogo madogo ili makampuni na mashirika mengi yaweze kushirikishwa. Kunaweza kuwa jaribio la kupeana kandarasi moja kubwa na kuliacha suala la kutafuta watoa huduma kwa mshindi huyu ambaye anaweza ama hataweza kutumia wapewa kandarasi wadogo.
Kugawa tenda kunaweza kuyawezesha mashirika madogo, yakiwemo mashirika yasiyo ya serikali na makundi yasiyofanya biashara kwa manufaa ya kupata faida, kutuma maombi na kufaulu. Mkakati kama huo ni muhimu hasa katika kupata huduma za kitaalamu kutoka kwa watu mablimbali bila watu hawa kuingia katika mashirika yasiyofaa. Aidha, hutoa nafasi kwa biashara ndogo ndogo kuweza kufikia shughuli hizi, hasa ikiwa utengaji huo unafanywa kwa misingi ya majukumu au maeneo ya kijiografia.
Mbinu ya Kuteua
Bei nzuri si kigezo cha kipekee cha kiuchumi. Hata wale wanaochukua bidhaa na huduma kwa misingi hii huchunguza ubora, uwezo wa kufanya kazi hiyo, kuaminika miongoni mwa mengine.
Wale wanaotayarisha ununuzi kwa kiwango cha taifa wanaweza kuchagua kuongeza mbinu inayohimiza mashirika Fulani kutuma maombi na kuyapa nafasi nzuri ya kushinda tenda. Kando na mikakati ya wazi ya kuthibitisha, ambayo huenda ikayazawadi makundi tengwa na kushiriki kwa wanawake, kunaweza kuwa na kigezo cha lugha, au ufahamu wa hali za maeneo hayo, au uwezo wa kufanya kazi na kuvutia idadi kubwa ya wafanyakazi wa kujitolea. Katika haya yote dhana inafanywa kuwa vigezo hivi vitasaidia utoaji huduma na kukubalika kwake katika jamii; na kwamba utoa huduma kwa kiwango kikubwa una wajibu wa kuongeza usawa.