Katika mwaka halisi au muhula kamili wa uchaguzi, halmashauri ya kusimamia uchaguzi inaweza kuwa na nafasi ndogo ya kuwasiliana moja kwa moja na wapigakura kwa manufaa ya elimu kwa wapigakura. Katika shughuli ya usajili hata hivyo, halmashauri hiyo italazimika kuwasiliana kuhusu ukweli na ujumbe fulani kwa wapigakura, na hili huipa halmashauri hiyo nafasi ya kuongeza kipengele cha elimu kwa wapigakura kwenye shughuli hiyo. Hatua ya kwanza ni kuwasilisha taarifa ya kismingi kuhusu usajili wa wapigakura – nani anayestahili kujisajili kupiga kura, jinsi ya kujisajili na kadhalika – lakini ni bora zaidi kuongeza jumbe kuhusu umuhimu wa kupiga kura. Jumbe hizo zinaweza kulenga makundi fulani ya wapigakura kama vile vijana, wanawake, jumuia za makabila fulani au watu wasio na makazi.
Mambo Yanayoathiri Mipango ya Elimu
Fomu ya usajili wa wapigakura inayotumika itafafanua lengo la jumbe za elimu kwa wapigakura. Ikiwa usajili unafanywa kwa njia ya kutoka nyumba hadi nyingine, msisitizo utakuwa kuhusu kueleza sababu kwa nini hilo linalifanyika na kinachohusishwa. Jumbe zitawaeleza watu kwamba maofisa wa kusimamia uchaguzi au usajili watawatembelea katika maboma yao, kwamba maofisa hao wataonyesha vitambulisho vyao, na kwamba wasajili hawa wa kuhesabu watakusanya taarifa inayohitajika ili kuongeza wakazi wastahifu wa kila boma kwenye orodha ya wapigakura.
Lengo huwa tofauti katika mfumo unaotumia vituo vya usajili. Jumbe zitawaeleza wapigakura kuhusu mahitaji ya usajili, na utawaambia lini na mahali pa kupigia kura. Katika wilaya inayohudumiwa na kitengo cha kuhamishwa cha usajili, jumbe hizo zitawaarifu wapigakura kuhus tarehe ambazo vituo vitaanza kufanya kazi katika mazingira yao.
Hesabu
Ikiwa hesabu ndiyo mbinu iliyoteuliwa kwa usajili wa wapigakura, mpango wa elimu unapaswa kueneza tarehe na saa ambapo shughuli hiyo itafanyika – hasa kwa kuwa wakati ambapo wasajili watazunguka huwa mfupi kiasi. Sura nyingine ya elimu kwa wapigakura ni kadi ambazo wasajili wa kuhesabu wataacha katika makazi ambayo hawapata mtu yeyote nyumbani. Kadi hiyo inaweza kueleza zaidi hatua za kusajili wapigakura katika makazi hayo; kwa mfano, inaweza kutoa tarehe ambayo wasajili hao watarudi tena, au nambari ya simu ya kupiga ili kuulizia taarifa zaidi.
Usalama pia ni jambo la muhimu katika hesabu. Kwa kuwa wapigakura huombwa kufungua milango ili wasajili waweze kuingia, mtu bandia anaweza kutaka kuingia katika boma hilo bila idhini. Mpango wa elimu kwa wapigakura unapaswa kueleza jinsi ya kutambua wasajili halisi na vitambulisho ambavyo maofisa hawa watabeba.
Kingine cha muhimu ni kutoa usalama kwa wasajili. Kinga ya kawaida ni mahitaji kwamba wafanye kazi katika jozi. Hili linaweza kuzidisha gharama na kusababisha juhudi za kupata wasajili watakaoweza kufanya kazi pamoja kwa ushirikiano, lakini manufaa ya usalama ni muhimu. Vielelezo vya usajili vyenyewe vinaweza kuhitaji kwamba wasajili wawili wafanyie kazi pamoja, huku kila mmoja wao akiwakilisha haja tofauti ya kisiasa na/au kuteuliwa na chama tofauti cha kisiasa.
Vituo vya Usajili
Katika mfumo unaotumia vituo vya usajili, elimu kwa wapigakura husisitiza umuhimu wa kujisajili, na itaeleza tarehe na nyakati za usajili na maeneo ya vituo vya usajili. Jumbe nyingine zinaweza kuwaeleza aina ya stakabadhi, ikiwa zipo, wanapaswa kuleta kwenye kituo cha usajili (k.m. thibitisho la utambulisho, anwani na uraia), ikiwa wanaweza kusajili watu wa familia na vilevile wenyewe, au cha kufanya ikiwa hawawezi kufika kwenye vituo vya usajili katika saa zilizotangazwa za utendakazi.
Wadau katika Elimu kwa Wapigakura
Mipango ya elimu kwa wapigakura inapaswa kulenga kuhusisha vyombo vikuu vya habari katika kueneza taarifa muhimu, kupitia kwa matangazo ya kibiashara au huduma za matangazo ya taarifa zinazolenga umma. Katika nchi ambako vyombo vikuu vya habari vinaendeshwa na serikali, ni kuwa changamoto ya kiasi fulani kuhakikisha kwamba hakuna mapendeleo ya kisiasa. Ikiwa hiyo ndiyo hali, mashirika ya kijumuia, mashirika yasiyo ya kiserikali na vyama vya kisiasa vyenyewe vinaweza kusaidia kueneza umuhimu wa kujisajili kama mpiga na jinsi ya kujisajili.
Katika demokrasia changa, mashirika ya kigeni yasiyo ya kiserikali yanaweza kutoa usaidizi kwa elimu kwa wapigakura. Katika visa hivi (na vilevile visa vingi), ujumbe mkuu unaweza kuwa kuwa “Ni lazima ujisajili ili kupiga kura.”
Rejista Endelevu na Sajili ya Raia
Katika ujenzi wa mwanzoni wa orodha endelevu, mahitaji ya elimu kwa wapigakura yanafanana na yale kutengeneza orodha ya muda. Tofauti ni kwamba orodha ya muda hutumiwa tu kwa tukio moja la uchaguzi, na iwapo mtu ameorodheshwa au la, hakuna athari yoyote zaidi ya tukio hilo. Kinyume cha haya, kufaulu kwa shughuli ya usajili wa mwanzo kwa orodha endelevu husaidia kutambua kufaulu kwa muda kwa sajili hiyo na hivyo basi mchakato mzima wa demokrasia. Juhudi za elimu zinapaswa kuwasilisha mtazamo huu kwa wapigakura watarajiwa ili waelewe kwa ukamilifu athari ya kuteua kutojisajili.
Elimu kwa raia kuhusu usajili ina wajibu pia katika nchi inayotumia mfumo wa sajili ya raia. Kwa kuwa ushiriki katika sajili hiyo mara nyingi huwa wa lazima, jumbe zinapaswa kuwaarifu wananchi kuhusu mahitaji yoyote mapya na adhabu ya kutozingatia hayo. Raia pia wanapaswa kujua kuhusu jinsi kuzingatia au kukiuka kunavyoathiri haki zao za raia na/au za kidemokrasia. Kwa mfano, wakikosa kujisajili kufikia tarehe ya mwisho iliyotangazwa kabla ya uchaguzi, wanaweza kulazimika kulipa faini na huenda wakakosa njia ya kustahili kupiga kura katika tukio hilo.
Viwango vya juhudi za Elimu
Viwango vya mpango wa elimu kwa wapigakura hutegemea tajriba ya hapo awali ya nchi hiyo na kukusanya taarifa kuhusu raia wake na kufanya chaguzi za kidemokrasia. Ikiwa kuna mazoea ya kutunza rekodi za raia na kuandaa chaguzi huru na za haki, uhamasisho wa wapigakura unaweza kujengwa na mpango wa elimu utakuwa wa wastani. Juhudi kubwa zinahitajika ikiwa mfumo huo umeimarishwa katika siku za hivyo karibuni, au ikiwa nchi hiyo ina tajriba ndogo ya na usajili au chaguzi za kidemokrasia.