Orodha ya kwanza ya wapigakura ikishatayarishwa na kupewa wapigakura na vyama vya kisiasa, hatua ya pili itakuwa kuikusanya mabadiliko kwenye orodha hiyo. Sababu mbalimbali zinaweza kuchochea haja ya kudurusu orodha ya kwanza:
- Wapigakura wengine stahifu hutaka majina yao yaongezwe kwa sababu walikosekana katika usajili wa mwanzo au hawakuweza kujipeleka kwenye kituo cha usajili katika kipindi cha usajili.
- Wapigakura wengine wamehama tangu kusasaishwa kwa orodha hizo na makao yao mapya yamenakiliwa.
- Wapigakura wengine wamefikisha umri wa kupiga kura, wamekuwa raia au pengine wameafiki mahitaji ya uistahifu, na mabadiliko katika taarifa hizo zao hayajanakiliwa.
- Wapigakura wengine wanataka kusahihisha taarifa iliyonakiliwa au kuandikwa vibaya (k.m. maendelezo mabaya ya jina na makao)
- Wengine wanaweza kutaka kuondolewa kutoka kwenye orodha.
Kwa ufupi, kuna sababu nyingi zinazoweza kuchangia orodha ya kwanza ya wapigakura kukosa usasa, kukosa ulinganifu na kutokamilika. Kipindi cha masahihisho hutoa nafasi nzuri ya kuimarisha ubora wa orodha hiyo.
Kutoa Majina kwenye Orodha ya Kwanza ya Wapigakura
Mtu anaweza kuondolewa kwenye orodha ya kwanza ya wapigakura ikiwa kuna ushahidi kwamba mtu huyo hatimizi mahitaji ya uraia na ukazi, au amepoteza haki yake ya kupiga kura kwa sababu ya kutatizika kiakili au kutuhumiwa kwa kosa la jinai. Kwa kawaida, jina hilo hufutwa baada ya mchakato kamili au nusu yake wa kisheria ili kuzuia kuondolewa kwa njia za hila.
Maofisa wa usajili wanapaswa kuondoa jina la mtu yeyote aliyewekwa kwenye orodha hiyo japo tangu wakati huo ameshafariki. Mara nyingi, hutaka ushahidi wa stakabadhi za kuthibitisha kifo hicho ili kuondoa jina hilo; mpango wa utumizi deta kwa ushirikianopamoja na takwimu muhimu ambazo ofisi hiyo vinaweza kutoa taarifa muhimu na ushahidi kwa halmashauri ya kusimamia uchaguzi.
Kwa kawaida, mpigakura hawezi kuomba kuondolewa kwa jina mtu mwingine kutoka kwenye orodha ya wapigakura. Hii ni kinga thabiti ya kuwakomesha wafuasi wa chama kimoja dhidi ya kuondoa majina ya wapinzani wao.
Madai na Vipingamizi
Kadiri inavyowezekana, uongezaji wa majina au usahihishaji wa taarifa iliyoko kwenye orodha ya kwanza vinapaswa kusalia kuwa shughuli ya kiusimamizi badala ya jukumu la kisheria au nusu-sheria. Hata hivyo, hatua kabambe zinapswa kufuatwa katika kuondoa majina kutoka kwenye orodha. Mara nyingi mahakama ya urejelezi, au shirika dogo la kisheria, ina jukumu la kusikiliza mashtaka yanyohusu orodha ya wapigakura; ina mamlaka, wakati mwinginw kwa pamoja na ofisa mkuu wa kusimamia uchaguzi, kubadilisha orodha hiyo baada ya kusikizwa.
Maeneo mengi ya kiusimamizi huchukulia zoezi la kusikiliza mashtaka kama jukumu la kiusimamizi badala ya kuwa jukumu la mahakama. Ofisa mkuu wa kusimamia huhakikisha kwamba kila mtu anayestahili kupiga kura anahimizwa na kuarifiwa kuhusu tarehe na mahali pa kusikilizwa kwa mashtaka sawa na yafanywavyo makundi yanayowasilisha mashtaka hayo. Wote wana haki ya kuwepo na kutoa nyenzo au taarifa kwa mahakama hiyo ya urejelezi. Mahakama hii ndiyo mwamuzi wa mwisho kwenye mashtaka yanayohusu orodha ya kwanza ya wapigakura.
Hoja mbili zinapaswa kuzingatiwa:
- Ikiwa wapigakura wanaweza kusajiliwa siku ya uchaguzi, hatua hii haiwezi kutekelezeka kwa kuwa usikizwaji wa kesi hiyo utafanyika baada ya uchaguzi,
- Ikiwa orodha ya kwanza haina ubora wa kuridhisha, usikizwaji wa kesi hiyo unaweza kuwa kikwazo kikubwa na unaweza kuhitaji kuharakishwa.