Umuhimu wa AV
Umuhimu mmoja wa kuhamisha karatasi za kura ni kuwa huwezesha kura za wagombeaji wengi kukusanywa, ili kuwezesha mitazamo anuwai na inayohusiana kuwekwa pamoja ili kushinda uwakilishaji. AV pia huwezesha wafuasi wa wagombeaji ambao wana matumaini ya chini ya kuchaguliwa kutoa ushawishi wa kupata nafasi ya pili , kupitia uteuzi wao wa pili, na kutokana na uchaguzi wa mgombeaji mwenye ufuasi mkubwa. Kwa sababu hii inadaiwa kuwa AV ndio mfumo bora zaidi katika kuhimiza siasa za mwanasiasa mwenye uchaguzi wa kati, kwa kuwa unaweza kuwalazimisha wagombeaji kutafuta sio kura tu kutoka kwa wafuasi wao bali pia za watakaowafuata katika upendeleo. Tajriba ya AV huko Australia huunga mkono madai haya; vyama vikuu kwa mfano hujaribu kusawazisha majadiliano na vyama vidogo vichukue nafasi ya pili kutoka kwa wafuasi wao kabla ya uchaguzi – mchakato unaojulikana kama ‘kubadilisha upendeleo’. Zaidi ya haya, wanachama huweza kuimarisha mitazamo yao kihalali.
Matumizi ya AV huko Papua New Guinea na Australia hupendekeza kwamba unaweza kutoa vichocheo halisi vya siasa zenye makubaliano na ushirikiano. Katika miaka ya hivi karibuni, AV au mfumo ulio kinyume chake, Supplementary Vote, umechukuliwa na kutumika katika uchaguzi wa uraisi na umeya huko Bosnia, London na San Francisco.
Udhaifu wa AV
Hata hivyo, AV ina udhaifu wake. Kwanza panahitajika kiwango fulani cha uwezo wa kusoma na kuhesabu ili utumike kwa ufanisi, na kwa sababu unafanya kazi katika wilaya zenye uanachama mmoja unaweza kutoa matokeo ambayo hayana ulinganifu ikilinganishwa na mifumo ya PR - au hata katika hali zingine ulinganishwe na FPTP . Pia uwezo wa AV wa kuinua matokeo ya kati hutegemea sana hali zilizopo za kijamii na idadi ya watu: huku kwa ufanisi ukihimiza kuwashughulikia makabila yote hoko Papua New Guinea katika miaka ya 1960 na 1970, umetolewa lawama katika nchi ya Pacific, Fiji, kwa sababu ulitumika huko mwaka wa 1997. Zaidi ya hayo kama ilivyotambuliwa ulipotumiwa katika Australian Senate kati ya miaka ya 1919 hadi 1946, AV haufanyi vizuri unapotumiwa katika wilaya kubwa na zenye uanachama zaidi ya mmoja.


Alternative Vote
Stop messing with a proven system.