Umuhimu na Udhaifu wa Two Round System (TRS) —
تخطى إلى المحتوى
|
Skip to navigation
البحث في الموقع
Advanced Search…
English
Español
Русский
العربية
Français
Swahili
الرّئيسة
الموســـوعة
بيانـــات المقارنـــة
مواد انتخابية
المشـــورة والدعـم
الأقاليم والبلدان
حول شبكة المعرفة الانتخابية أيــس
الأدوات الشخصية
تسجيل الدّخول
شبكة الممارسين الانتخابية
الرئيسة:
الرّئيسة
»
Encyclopaedia
»
Mada
»
Mifumo ya Uchaguzi
»
Mifumo na Athari Zake
»
Mifumo Yenye Wafuasi Wengi
»
The Two-Round system (TRS)
»
Umuhimu na Udhaifu wa Two Round System (TRS)
face
Practitioner Login
العربية
Encyclopaedia
Info
النظم الانتخابية
Topic Index
Umuhimu na Udhaifu wa Two Round System (TRS)
Umuhimu wa TRS
Kwanza kabisa, TRS huwaruhusu wapigaji kura kuwa na nafasi ya pili ya kupigia kura mgombeaji wanayempenda au hata kubadilisha nia kati ya awamu ya kwanza au ya pili. Huwa na sifa sawa na zile za mifumo ya upendeleo ya Alternative Vote ambapo wapigaji kura hutakiwa kuorodhesha wapigaji kura ili kufanya uamuzi mpya kabisa katika awamu ya pili ikiwa watataka.
TRS ni mfumo unaoweza kuhimiza mielekeo tofauti kuungana ili kufanikisha ushindi wa wagombeaji waliotangulia katika awamu ya kwanza ambao huweza kuongoza baada ya uchaguzi wa awamu ya pili, hivyo basi kuhimiza mijadala ya kuuza nafasi kati ya vyama na wagombeaji. Pia huwezesha vyama na wapigaji kura kuonyesha hisia kuhusu mabadiliko katika uwanja wa kisiasa ambayo hutokea kati ya uchaguzi wa awamu ya kwanza na ya pili.
TRS hupunguza matatizo ya ‘kugawa kura’, hali iliyo ya kawaida katika mifumo ya walio wengi ambapo vyama viwili vinavyofanana au wagombeaji hugawana kura zao zilizowekwa pamoja, na hivyo kumruhusu mgombeaji asiye na ufuasi mkubwa kushinda. Pia kwa sababu wapigaji kura hawana orodha ya kuwapanga wagombeaji ili kudhihirisha uteuzi wao wa pili, TRS huweza kufaa zaidi katika nchi ambapo hali ya kutojua kusoma imeenea kuliko katika mifumo ambayo hutumia hesabu ya upendeleo kama vile Alternative Vote au Single Transferable Vote.
Udhaifu wa TRS
TRS huweka shinikizo kwenye uongozi wa uchaguzi kwa kuutaka kufanya uchaguzi wa pili muda mfupi tu baada ya ule wa kwanza, hivyo kuongeza kwa kiwango kikubwa gharama ya mchakato wa uchaguzi kwa jumla pamoja na muda unaopita kati ya kufanyika kwa uchaguzi hadi wakati wa kutangaza matokeo. Hili huweza kusababisha ukosefu wa udhabiti pamoja na wa uhakika. TRS pia huweka mzigo wa ziada kwa mpigaji kura kuhusiana na muda na uwezo unaotakikana kupiga kura kwa kuwa inambidi kufika kwenye kituo cha kupigia kura mara mbili, na wakati mwingine huwa kuna upungufu mkubwa wa wanaofika kati ya awamu ya kwanza na ya pili.
TRS huwa na udhaifu sawa na ule wa FPTP. Utafiti unaonyesha kwamba huko France mfumo huu unatoa matokeo yaliyokosa usawa zaidi katika demokrasia yoyote ya kimagharibi, na kuwa hupelekea kugawa mifumo ya chama katika demokrasia mpya.
Mojawapo ya matatizo makubwa ya TRS ni athari zake za kuwa na jamii zilizogawika zaidi. Huko Angola mwaka wa 1992, katika yale yaliyotazamiwa kuwa uchaguzi wa kuleta amani, kiongozi wa uasi Jonas Savimbi alichukua nafasi ya pili katika awamu ya kwanza ya uchaguzi wa urais wa TRS baada ya Jose dos Santos akiwa na asilimia 40 ya kura ikilinganishwa na dos Santos asilimia 49. Kwa kuwa ilikuwa wazi kwamba angeshindwa katika uchaguzi wa awamu ya pili, alikuwa na kichocheo hafifu cha kuchukua nafasi ya harakati za Demokrasia ya upinzani na moja kwa moja akaanza upya vita vya kuvizia huko Angola, ambavyo vilichukua miaka kumi. Katika Jamhuri ya Congo mwaka wa 1993, matarajio ya ushindi mkubwa wa serikali katika awamu ya pili ya uchaguzi wa TRS uliufanya upinzani kusuzia awamu ya pili na kutangaza vita. Katika hali hizi mbili, ishara wazi ya kushindwa kwa upande mmoja ni ile inayosababisha vurugu. Nchini Algeria mwaka wa 1992, mgombeaji wa Islamic Salvation (Front Islamique du Salut, FIS) aliongoza katika awamu ya kwanza na wanajeshi waliingilia kati katika kufutilia mbali awamu ya pili.
Mifumo ya Uchaguzi
Contributors to Electoral Systems
Electoral Systems Glossary
Bibliography
جهة اتصال
نهج الخصوصية
شروط الاستخدام
إتاحة
خريطة الموقع
حق المؤلف وتنويه
©
1998-2025 ACE project