Kimuundo, List PR huhusu kila chama kikiwakilisha orodha ya wagombeaji kwenye tume ya uchaguzi kutoka kwa kila wilaya yenye uanachama zaidi ya mmoja. Wapigaji kura huchagua chama na vyama hupokea viti kulingana na mgao wake wa kura katika wilaya ya uchaguzi. Wagombeaji wanaoshinda hutolewa kwenye orodha kulingana na nafasi zao kwenye orodha . Uteuzi wa List PR hauelezi bayana mfumo wa uchaguzi: habari zaidi lazima zielezewe. Mfumo unaotumIwa kuhesabu utoaji wa viti baada ya kura kuhesabiwa huweza kuwa ya mbinu ya Highest Average au Largest Remainder. Fomula inayochaguliwa huwa na athari ndogo lakini wakati mwingine huwa muhimu kwenye matokeo ya uchaguzi chini ya PR. Huko Cambodia mwaka wa 1998, badiliko kwenye fomula wiki chache kabla ya siku ya uchaguzi lilikuwa na athari ya kupatia chama kikubwa viti 64, badala ya 59 kwenye bunge la wawakilishaji 121. Badiliko hili halikuwa limetangaziwa umma ilivyohitajika, na upinzani ulikubali matokeo shingo upande. Mfano huu hueleza kwa uwazi umuhimu wa wapangaji wa mfumo wa uchaguzi kudhihirisha maelezo yote hata yale madogo.

Karatasi ya Kura ya List PR iliyo Funge huko Cambodia
Kuna masuala mengine muhimu ambayo yanahitaji kushughulikiwa katika kueleza kwa uwazi jinsi mfumo wa list PR utakavyofanya kazi. Kiwango cha juu rasmi huhitajika kwa uwakilishaji bungeni: kiwango cha juu (kwa mfano asilimia10 kama inavyotumika Turkey) huweza kutenga vyama vidogo, huku kiwango cha chini (kwa mfano asilimia 1.5, kama inavyotumika Israel) huweza kuimarisha uwakilishaji wao. Huko Afrika Kusini, hakuna kiwango cha juu rasmi na katika mwaka wa 2004 chama cha African Christian Democratic Party kilishinda viti sita kutokana na viti 400 kikiwa tu na asilimia1.6 ya kura za taifa. Mfumo wa list PR pia hutofautiana kutegemea jinsi na vile mpigaji kura huweza kuchagua wagombeaji pamoja na vyama yaani ikiwa orodha ni funge au wazi, uteuzi huu huwa na athari kwenye uchangamano wa karatasi ya kura.
Teuzi zingine hujumlisha mipango rasmi au isorasmi ya ‘uletaji pamoja wa kura’; upana wa makubaliano kati ya vyama, kama ule unaotolewa na mifumo yenye kutumia uwazi: na kuweka wazi mipaka ya wilaya.

