Viwango vya juu ambavyo hufanikiwa zaidi huweza kutumika kubagua vyama vidogo – kwa hakika , katika hali nyingine hili ndilo lengo lake lakini katika hali nyingi ubaguzi wa aina hii dhidi ya vyama vidogo hutazamwa kama usio wa kupendelea, hasa pale ambapo vyama vidogo vyenye maeneo ya ufuasi yaliyo sawa ‘hugawa’ kura zao za pamoja na hivyo kupata kura chini ya viwango vya juu vilivyowekwa, wakati kundi moja lililopo lingepata kura za kutosha ili kushinda bungeni . Ili kutatua shida hii, baadhi ya nchi, huunda miungano yenye ukiritimba - au apparentement au stembusaccoord - ili kushindana katika uchaguzi. Hili humaanisha kwamba vyama vyenyewe husalia kuwa huru na huorodheshwa kwa njia tofauti katika karatasi ya kura, lakini kura ambazo kila chama hupata huhesabiwa kama zinavyomilikiwa na miungano mizima yenye ukiritimba, hivyo kuongezea nafasi ambapo idadi yote ya jumla itakuwa juu ya kiwango cha juu kilichowekwa na hivyo kuviwezesha kupata uwakilishaji zaidi. Chombo hiki huwa na sifa za idadi ya mifumo ya List ya PR katika maeneo ya Uropa, Latin America (ambapo vyama chini ya chama kikubwa huitwa Lema) na Israel. Vyama hivyo hata hivyo huwa haba kwenye mifumo ya PR Barani Afrika na Asia, na vilifutiliwa mbali huko Indonesia mwaka wa 1999 baada ya vyama vidogo kugundua kwamba, hata kama miungano yao yenye ukiritimba ilipata uwakilishaji kwa jumla, kwa ujumla walipoteza viti kama vyama.

