Huku MMP ikiweka faida za usawazishaji za mifumo ya PR, pia huhakikisha kwamaba waliochaguliwa wameunganishwa na wilaya kijiografia. Hata hivyo, pale ambapo wapigaji kura wana kura mbili - moja ya chama na moja ya mwakilishi wa eneo lao - huwa haieleweki kila wakati kuwa kura ya uwakilishaji wa eneo lao huwa haina umuhimu kuliko kura ya chama katika kuamua utoaji wa kijumla wa viti bungeni. Zaidi ya hayo, MMP huweza kutoa makundi mawili ya wanabunge kundi moja likiwajibikia eneo bunge na lingine kutokana na orodha ya chama cha kitaifa bila mahusiano ya kijiografia na kushughulikia chama. Hili linaweza kuwa na athari katika mshikamano wa makundi ya wawakilishaji wa vyama waliochaguliwa.
Katika kufasiri kura kuwa viti, MMP huweza kuwa na usawazishaji wa mfumo wa uchaguzi kama ilivyo List PR iliyo safi, na hivyo, sababu moja ya kwa nini MMP wakati mwingine huchukuliwa kama usiopendelewa ikilinganishwa na List PR uliowekwa sawa ni kwamba unaweza kutoa matokeo yasiyo ya kawaida yanayotiwa ‘upigaji kura wenye mikakati’. Huko New Zealand mwaka wa 1996, katika eneo bunge la Wellington Central, baadhi ya mikakati ya National Party iliwahimiza wapigaji kura kutopigia kura mgombeaji wa National Party kwa sababu walikuwa wamepiga hesabu kwamba chini ya MMP, uchaguzi wake haungepatia National Party kiti kingine lakini kumbadilisha mwanabunge ambaye angechaguliwa kutokana na orodha yao ya chama. Basi ilikuwa afadhali kwa National Party kumuona mgombeaji akichaguliwa kutokana na chama kingine ikiwa mgombeaji huyo alikuwa ana upendeleo wa maoni na imani za National Party kuliko kwenye kura ‘zitakazo haribika’ ili kumuunga mkono mgombeaji wao.

