Karatasi ya kura inastahili kuwa yenye kueleweka kwa urahisi kwa wapigaji kura wote ili kuhakikisha idadi kubwa ya wapigaji kura imeshiriki na kupunguza idadi ya kura zitakazoharibiwa au zisizo halali. Karatasi za kura za mfumo wa FPTP na AV huwa rahisi kuchapisha na katika hali nyingi huwa na idadi chache ya majina. Karatasi za kura za mfumo wa TRS huwa sahili pia lakini katika hali nyingi karatasi mpya za kura huhitaji kuchapishwa ili zitumike katika awamu ya pili ya upigaji kura hivyo basi kupandisha mara mbili gharama ya utoaji wa karatasi za kura; na nafasi hutengwa ili kuhakikisha kuwa karatasi za kura zimetolewa kwa uchaguzi wa pili. Mifumo sambamba na wa MMP kawaida huhitaji uchapishaji wa karatasi mbili za kura ili zitumike katika uchaguzi wa siku moja na hutumia mifumo miwili tofauti (au zaidi) yakiwemo matokeo ya upangaji wa mafundisho kwa maofisa wa uchaguzi na jinsi ambavyo watu wanastahili kupiga kura. Karatasi za kura za mifumo ya SNTV, BV, BC na STV huwa na ishara na picha zaidi (ikiwa zitatumika). Mwisho, karatasi za kura za mfumo wa orodha ya PR huweza kuvuka mwendeleo wa uchangamano. Huweza kuwa sahili kama ilivyo katika mfumo wa orodha funge au kuwa changamano zaidi kwenye mfumo wa orodha wazi kama ilivyo huko Switzerland.

