Kufafanua Mifumo ya Uchaguzi
Mifumo ya uchaguzi ni ubunifu wa wanadamu. Ni jambo linalotarajiwa kuwa mfumo wa uchaguzi wowote mahsusi, ambao umebuniwa katika hali fulani, kuafikia madhumuni fulani na kuimiza maadili fulani, sasa una athari kwa mifumo ya kisiasa ambamo wananchi wanaishi. Haikuteremshwa kutoka mbinguni ingawa inaweza kulindwa katika katiba, na hivyo ni jambo linalohusisha mjadala wa umma, na ikiwezekana, mabadiliko ya kisiasa.
Mpango wa elimu kwa raia utawapa wananchi baadhi ya maoni yanayounga mkono mifumo fulani na ubora na udhaifu wa mfumo wao. Hii itakuwa imefanyika bila ya ushawishi usiofaa kwa watu kuufuata mfumo mmoja au mwingine iwapo hatua hii inahujumu imani ya wananchi katika mfumo wao wa uchaguzi au unahatarisha na kukejeli wale wanaopigia debe uzuri wa mfumo mmoja au mwingine.
Bila ya elimu ya kijumla zaidi, mijadala ya umma kuhusu mifumo ya uchaguzi inaweza kupamba moto bila sababu, na kwa haraka inaweza kwenda nje ya muktadha ambamo uchaguzi unafaa kufanyika na mfumo unaofaa kwa wakati uliopo, na kuingia katika hali ya ugomvi unaokumbusha “bigendians” na “littleendians” wa Gulliver’s Travels.
Baada ya kuchaguliwa kwa mfumo wa uchaguzi, Wapigakura wapya watahitaji maelezo kuhusu namna unafanya kazi. Wakati ambapo mfumo unafanyiwa mabadiliko, waelimishaji watakuwa na changamoto mahsusi katika kuelezea mfumo mpya, hasa kwa kuzingatia ushikamano mkubwa ambao watu wanakuwa nao kwa mfumo wao na kutokuwa na nia ya mabadiliko. Mifumo ya uchaguzi pia inaonekana kuwa na ushikamano mkubwa sawa na ule unaopatikana kati ya fedha, uzito na vipimo – mabadiliko ya kizazi yanaonekana kuwa yenye manufaa kuliko elimu.
Waelimishaji mara nyingi huvutiwana siasa na chaguzi – ni wito na pia ni jambo la kupitisha la muda, na masuala yanayohusiana na mifumo ya uchaguzi yanaonekana kuwa na ushawishi mkubwa. Kuna ushawishi wa kubadili nafasi za kuwaelimisha watu kuhusu mfumo fulani wa uchaguzi na kuzifanya kuwa shughuli zilizojawa na mambo magumu au yanayokanganya kupitia kwa mambo madogo madogo yenye maelezo ya kina. Mahitaji ya hadhira yanapotelea tu katika mijadala inayohusu fomula, maelezo yanayohusu mipaka ya maeneo bunge, na mijadala baina ya vyama vya kisiasa na tume za kusimamia uchaguzi kuhusu uundaji wa orodha wakati kunapopatikana nafasi na kadhalika. Wakati ambapo makundi fulani ya watu wanafaa kujua mambo haya, waelimishaji ni lazima kwanza watambue mahitaji na viwango vya hadhira.
Mtego kwa Waelimishaji
Je, kuna mambo fulani ya kimsingi ambayo ni muhimu?
- Kwa nini mfumo wa sasa umechaguliwa?
Bila shaka sababu ya nchi kuwa na mfumo fulani wa uchaguzi
- Ni chaguo lipi ambalo watu watakabiliana nalo katika kibanda cha kupiga kura?
Mifumo tofauti ya uchaguzi ina athari tofauti kuhusiana na nini ambacho watu watakabiliana nacho katika kibanda cha kupigia kura. Je, wataona orodha ya vyama vya kisiasa? Au orodha ya majina ya wagombezi? Je, watapata nafasi (kama ilivyo Sweden) ya kuchagua chama cha kisiasa kupitia kwa chaguo la karatasi la kupigia kura na kasha waone orodha ya wagombezi wa chama hicho ili waweze kufanya uchaguzi wanaoupenda kutoka kwa wagombezi hao?
Wapigakura hawafai kushangaa wakati wanapoingia katika kibanda cha kupigia kura. Wanafaa kujua uchaguzi wao ulizwa kufanya, hasa wanapohitajika kufanya uamuzi wa zaidi ya moja, ikiwa kwenye karatasi moja la kupigia kura lililo changamano au kutoka kwa msururu wa karatasi za kupigia kura kadha kama inavyoweza kufanyika katika mifumo mseto, au katika uchaguzi unaohusisha chaguzi zaidi ya moja zinazofanyika siku hiyo hiyo.
Kwa kujua chaguzi wanazofaa kufanya siku ya kupiga kura kunampa mpiga kura mwongozo wa ni nini cha kushughulikia wakati wa kampeni. Je, watahitajika kufanya uamuzi wa kuwili – chama hiki au kile, mgombezi huyu au yule – au watakuwa wakionyesha mapendeleo mbalimbali. Katika hali ya kwanza wanaweza kujitokeza na utaratibu wa kufanya maamuzi unaozingatia kutohusisha. Na katika hali ya pili wanaweza kujishughulisha na sehemu tofauti za manifesto za vyama ambazo zinawapendeza. Bila kujali namna Wapigakura watakavyo afikia mapendeleo yao, watajitokeza na mikakati inayozingatia jinsi mfumo wa uchaguzi unavyowakabili na maamuzi.
- Je, kura zao zitabadilishwa namna gani kuwa viti (nyadhifa)?
Baada ya waelimishaji kuelewa taratibu zinazotumiwa kubadilisha kura kuwa viti, ambazo zinatatiza sana kwa mifumo ya PR na STV lakini ambazo pia zinaweza kuwa na matatizo kwa mifumo ya FPTP kuhusiana na kura usawa wa idadi ya kura, kwa mfano, au katika chaguzi za urais za moja kwa moja kuhusiana kura za marudio, wanafaa kutafuta njia za kuelezea haya kupitia kwa uhusishaji wa sitiari na mielekeo. Mifumo ya PR mara nyingihuelezwa kwa kulinganisha na jinsi washindi katika michezo wanavyotuzwakwa kuzingatia mshindi wa kwanza, wa pili au wa tatu na kadhalika. Waelemishaji uzungumzia kuhusu washindi na washindwa katika mifumo ya FPTP. Wakati wa kujitokeza sitiari zifaazo, uangalifu unafaa kuhakikishwa kuwa hakuna kulimbikiza sifa kwa wale wanaofaulu – kwa kuwa watahitajika kuwawakilisha hata wale ambao waliamua kutowapigia kura – na kutafuta njia ambazo wale walioshindwa katika uchaguzi wanaweza kuhifadhi heshima na kufahamu kuwa yote hajapotea, la sivyo uwezekano wa mambo kuharibika unaweza kuongezeka.
Mpangilio wa matukio unachukua mifano kutoka kwa hali halisi au kutoka kwa hali bandia – ambazo huwa salama – na zinaonyesha jinsi idadi tofauti ya kura hubadilika na kuwa idadi tofauti ya viti (nyadhifa). Mifumo ya PR hasahunufaika kutoka kwa mifano kama hiyo, lakini mifumo mseto, ambayo inaendelea kuwa maarufu, pia mara nyingi huelezwa vizuri kupitia kwa njia hii – ambapo kuongezea juu hili kuweza kupata usawazishaji unaweza kuwa na athari tofauti kwa kutegemea idadi ya viti vilivyoshindwa na FPTP.
- Je, ni nini ambacho Wapigakura wanaweza kutarajia kutoka kwa vyama wakati wa kampeni na ni nani ambaye wanaweza kukutana naye au kumwona?
Vyama vya kisiasa vinaendelea kuwa tata katika usimamizi wao wa kampeni na wanatumia uchunguzi na demografia (data ya takwimu ya kima cha uzazi, vifo, maradhi na kadhalika) kupanga jinsi watakavyoingiliana na Wapigakura watarajiwa. Hata hivyo mifumo ya FPTP inaweza kubainishwa na kampeni za mashinani ambapo wagombezi wanatambulishwa na kuelezwa, na ambapo uwezo wao unazingatiwa sawa na maelezo kuhusu vyama vyao vya kisiasa. Katika mwisho wa uchaguzi, mpiga kura ataweza kumtambua mmoja au wengine wa wagombezi hao ambao wanachukua nyadhifa za viongozi waliochaguliwa. Wanaweza kuona tofauti katika vyombo vya habari vya mashinani – vikiangazia mgombezi wao, na vyombo vya habari vya kitaifa – vikiangazia viongozi wa chama na manifesto vya vyama au viti ambapo mgombezi anamshinda mpinzani wake kwa kura chache. Mifumo ya PR huvipa vyama alama, na katika nchi ambapo karatasi za kupigia kura zinahusisha picha ya kiongozi wa chama, picha ya kiongozi huyo pia hupewa alama. Utoaji wa maelezo kuhusu chama ni kila kitu, na wakati ambapo orodha za wagombezi zinaweza na zinafaa kutathminiwa, mara nyingi hupewa nafasi ya mwisho.
Wapigakura watataka kujua ikiwa kuna maana yoyote kuchukua wakati mwingi kumdadisi mgombezi kuhusiana na siasa zao za kibinafsi, na iwapo shughuli za chama zitakuwa na nguvu sana. Kwa upande mwingine, wanaweza kutaka pia kutafuta mgombezi mpinzani ikiwa wanahisi kuwa kufaulu kwake, bila kujali ikiwa ni mgombezi huru au wa chama kunaenda kutishia serikali.
- Je, bunge linaonekanaje baada ya uchaguzi?
Uzingativu mdogo sana hupewa matokeo ya uchaguzi wakati wa elimu kwa Wapigakura, sio tu katika usawazishaji wa madaraka pekee bali pia kwa maana ya utawala. Katika mifumo ya PR chaguo la vyama vingi vidogo linaweza kusababisha ugumu katika uundaji wa serikali thabiti. Katika mifumo ya FPTP, jukumu la mgombezi anayeibuka mshindi katika kuendelea kuwakilisha eneo bunge katika uhusiano wake na serikali linaweza kuwa jambo muhimu linaloamua jinsi mpiga kura anavyochagua. Wapigakura wanafaa kujua jinsi bunge litafanya kazi, mamlaka gani ambayo bunge na wawakilishi kibinafsi waliyonayo, na uhusiano wake kwa wenye mamlaka wengine waliochaguliwa kivyao.
Kalenda na ratiba ya uchaguzi
Kila uchaguzi bila shaka una ratiba. Wakati ambapo uelimishaji wa Wapigakura unaweza kuwa shughuli inayoendelea kila mara, kutakuwa na wakati ambapo uchaguzi unatangazwa na tarehe kuwekwa. Waelimishaji wanafaa kuwa na kalenda ya matukio muhimu katika uchaguzi na waunde Mpango wao ili kuhusisha tarehe hizi. Kwa kuzingatia haya, Mpango wa kina wa utekelezaji wa Mpango wa elimu kwa mpiga kura unafaa kuandaliwa na kuambatanishwa na kalenda ya uchaguzi. Kusema ukweli, kalenda ya uchaguzi inafaa kukamilishwa kabla kuanza kuanzishwa kwa Mpango wa elimu kwa mpiga kura. Hata hivyo, katika baadhi ya nchi zinazoendelea na jamii ambazo zinatekeleza mabadiliko, hii huenda isiwezekane. Katika hali hizi, waelimishaji nchi ya wasimamizi wa uchaguzi watataka kuhifadhi mawasiliano wazi na ya mara kwa mara na maafisa wa uchaguzi ili kubakia mbele ya makataa mapya au mabadiliko kwa ratiba ambazo zimewekwa kabla.
Kalenda ya uchaguzi inafaa kuhusisha tarehe zote ambazo zimewekwa katika sharia au kupitia kwa kanuni. Waelimishaji kisha watahitaji kuzingatia matukio haya muhimu ili kuamua ni yapi yanayowaathiri Wapigakura moja kwa moja na kukadiria mahitaji muhimu ya kielimu na maana yake.
Mpango wa elimu unafaa kuandaa watu kushiriki katika mchakato wa uchaguzi.Watu tofauti wanashiriki kwa wakati tofauti na, katika hali zingine, kupitia kwa njia tofauti. Kinadharia hata hivyo, Mpango wa elimu unaweza kuzungumzia maandalizi haya yote. Wakati ambapo elimu na habari kwa mpiga kura kimsingi zinalenga Wapigakura ujumla ( Tazama Wapigakura kwa ujumla), ni muhimu kuwa pia ilenge makundi yenye athari kuu (Tazama Makundi yenye Athari Kubwa) na katika kusaidia makundi madogo yanayolengwa katika ushiriki wao (Tazama Wapigakura Waliotengwa na Makundi Yenye Mahitaji Maalumu).
Matakwa ya Elimu
Miongoni mwa nyakati ambazo zinaweza kuwa za manufaa kwa Wapigakura na zinaweza kuhitaji kushiriki kwao zitakuwa:
- uundaji au usajili wa vyama vya kisiasa
- uteuzi wa wagombezi na orodha ya vyama, ambazo zinaweza kuhitaji shughuli za umma kama vile uchaguzi wa mwanzo na ukusanyaji wa sahihi
- uwekaji wa mipaka ya maeneo uchaguzi
- usajili wa Wapigakura na ukaguzi na uidhinishaji wa orodha ya Wapigakura
- uwekaji wa vituo vya kupigia kura
- muda wa kutuma maombi ya huduma maalum za kupiga kura kama vile upigaji kura na mpiga kura bila ya kufika katika kituo cha kupigia kura au katika vituo vya kutanga
- muda wa kupiga kura, ambao unaweza kuhusisha nafasi kwa upigaji kura mapema (kabla ya siku rasmi ya kupiga kura) na vilevile katika siku ya uchaguzi
- mchakato wa kutoa malalamishi, labda kupitia kwa tume za uchaguzi au mahakama
Inawezekana kwa waelimishaji kutumia wakati wa umma katika uchaguzi ili kuzidisha ufanifu wa Mpango wao. Kwa kuongeza nyakati hizi wanapata upeperushaji wa habari, mjadala wa umma, na pia kuwafanya Wapigakura kutambua mahitaji yao wao wenyewe ya kielimu.
Maana ya Elimu
Ya kwanza miongoni mwa hizi bila shaka ni kutangazwa kwa tarehe ya uchaguzi. Kama inavyotarajiwa, utangazaji huu huchochea shughuli za msukosuko na vyama, huongeza ufahamu wa umma kuhusu uchaguzi, na huanzisha mjadala kuhusu kinyang’anyiro katika vyombo vya habari na katika sehemu za kutangamana kwa wanajamii. Tangazo kama hilo, hasa katika hali ambapo inatarajiwa kuwa Mpango imara wa elimu kwa mpiga kura utahitajika, unaweza kuunganishwa na vifaa vya kutandaza na kutangaza kwa kuweka mahitaji ya kumruhusu mtu kupiga kura ikiwemo mchakato wa usajili.
Kutoka wakati huo na kuendelea, kutakuwa na nyakati sawa na hizo, kama sio yenye umuhimu wa chini kidogo. Kama nyakati hizi zimehusishwa katika kalenda, itawezekana kwa timu ya uchaguzi kutengeneza shughuli za kimpango zinawezesha kupata uenezi (hali ya kusambaa na kujulikana kwa habari), kuongeza athari za Mpango, na kujenga athari kubwa ambayo inahitajika ili kuzidisha athari ya shughuli hiyo, kupunguza juhudi na kupunguza gharama.