Kuna sababu mbili ni kwa nini maeneo ya uchaguzi yanafaa kutumika kama nafasi ya kwanza kwa elimu na habari kwa Wapigakura.
- Habari na elimu inaweza kutolewa kwa gharama ya chini
Usambazaji wa vifaa unaweza kujumuishwa na vifaa vingine vya uchaguzi. Matangazo yanaweza kubandikwa bila malipo. Vifaa vinavyotolewa kwa Wapigakura kuenda navyo vinaweza kusambazwa na wafanyikazi waliopo. Na wafanyikazi hao hao wanaweza kutimiza jukumu la habari kwa wakati huo huo wakati wanaposhirikishwa katika shughuli zingine.
- Vifaa vya habari na elimu kwa Wapigakura vinavyoonyeshwa katika maeneo ya uchaguzi vinatambulisha eneo na kulifanya liweze kuonekana vizuri zaidi
Wapigakura wanakaribishwa katika eneo na hivyo mojawapo wa sababu za kimsingi za habari kwa mpiga kura ni kuhakikisha kuwa watu wanajua mahali pa kuenda. Na mojawapo wa sababu za kimsingi za elimu kwa Wapigakura ni kuhakikisha kuwepo kwa imani katika mchakato na usimamizi. Sababu hizi zinashughulikiwa na wakati huo huo malengo mengine yanatimizwa.
Labda ni wazi kuwa maeneo ya kupigia kura yanaweza kuwa maeneo ya habari na elimu (Tazama Elimu kwa Wapigakura katika Maeneo ya Kupigia kura). Labda si wazi sana kuwa afisi za kiutawala za serikali, vituo vya usajili, au vituo vya kuhesabia na kupangia matokeo vinaweza kutumika kwa sababu sawa na hizo (Tazama Afisi za Wasimamizi wa Uchaguzi na Elimu kwa Wapigakura katika Vituo vya Kuhesabia). Pia huenda isiwe wazi kuwa watafanya hivyo hata kama wasimamizi wa uchaguzi wanatarajia au hawatarajii hivyo. Mahali palipo na afisi na vituo, uwezo wake wa kufikiwa na umma, huduma ambazo zinatolewa, na fahari ambayo afisi imetengenezwa au imetengenezwa tu ovyo ovyo kunaweza kutoa kuashiria fulani kwa umma unaopiga kura. Kwa kiasi kwamba afisi hizo zinaweza kuonekana na zinajieleza zenyewe na kueleweka hata kwa wasiopiga kura, pia zinasaidia kuongeza uhamasishaji, na hivyo, kuongeza idadi ya Wapigakura watarajiwa katika chaguzi za baadaye.