Eneo hili la mada linashughulikia habari kwa Wapigakura, elimu kwa Wapigakura na mada inayohusiana nayo ya elimu kwa raia. Katika hali nyingi, elimu kwa Wapigakura inaunda sehemu ya mtalaa wa elimu kwa raia. Kuwepo kwa Mpango wa elimu kwa raia unaoendelea bila shaka unaweza kuweka msingi na kuendeleza athari ya shughuli za elimu kwa Wapigakura.
Elimu kwa raia, hata hivyo, unaweza kuelezwa kwa mapana katika njia ambazo zinaipeleka nje ya shughuli za siasa za uchaguzi na msimamizi wa uchaguzi. Inawezekana kuwa mtu ambaye anawajibikia elimu kwa Wapigakura anaweza pia kuhusika katika shughuli pana ya elimu kwa raia. Kwa hakika, kuna kitu cha kuashiria kuwa elimu kwa Wapigakura ni muungano wa habari kwa Wapigakura na sehemu fulani za Mpango wa elimu kwa raia, hii ina maana kuwa, wale ambao wanahusika na uchaguzi. Elimu kwa raia inatekelezwa kwa undani katika miktadha isio rasmi ya elimu kwa watu wazima, ingawa kuna sehemu za elimu rasmi katika shule. Sehemu hii ya eneo la mada inatalii “Mielekeo Mbadala na Istilahi” na baadhi ya “Ujumbe Wastani wa Elimu kwa Raia” ambao waelimishaji wa raia wanachukulia kuwa muhimu.
Hali inayoendelea ya kutokuwa na uhakika
Kuna vishawishi viwili katika shughuli hii. Moja ni kuchukulia kila kitu kuwa elimu kwa raia, na ili iweze kuwekwa kama kanuni inayojumuisha na sharti la shughuli zote za kielimu. Nyingine ni kuitenga katika sehemu ndogo iliyotengwa kwa shughuli nyingine za kiusomi za maisha. Zote zinajaribiwa katika matendo, kama sio kufikiriwa tu katika nadharia. Zote ni muhimu. Usawazishaji unaohitajika kwa wananchi kuweza kuhisi wakiwa na nguvu na uwezo na kihalisi wakiwa na uwezo wa kushiriki katika uanzishaji, ujenzi, na udumishaji wa demokrasia ambazo zinaafiki miktadha yao ndiyo changamoto kwa wahamasishaji wa demokrasia na waelimishaji.
Istilahi
Weledi wa elimu kwa raia wamechagua dhana mbalimbali tofauti kuelezea kazi yao. Wanachagua majina kwa mielekeo ya kieleimu ambayo wanaamini inawasilisha shabaha ya elimu hiyo kwa njia iliyo sahihi. Kila mojawapo wa majina haya, au dhana, inayochaguliwa ina matatizo yake na michukulio yake ya kiutendaji. Lakini uchanganuzi wa dhana katika muktadha wa dhana zingine hakutoi utambuzi katika fikira za mwelimishaji wa raia.
Elimu kwa Demokrasia
Mipango inayojieleza yenyewe kama elimu kwa demokrasia inajishughulisha na kuwatayarisha watu kwa demokrasia kwa mchukulio kuwa inafaa kuanzishwa na kuimarishwa. Miongoni mwa yaliyomo ya Mpango wa elimu kama huo ni pamoja na maarifa na uelewaji ambao ni muhimu kwa uanzishaji na uimarishaji huu.
Waelimishaji wanaweza kuendesha mipango ya elimu kwa demokrasia katika jamii za kidemokrasia na kuiona shughuli hii kama hatua ya kijamii katika kuhakikisha kuwa wana demokrasia zaidi. Ufafanuzi huu wa demokrasia, kwa hivyo, unakuwa muhimu sana katika kuamua ni nini kinachofaa kufundishwa na vilevile Mpango wa elimu wenyewe. Ufafanuzi kama huo unaweza kuwa ulio bora: lakini unaweza kuwa wenye siasa kali, unaohusisha sehemu ya demokrasia ya kiviwanda, haki za watumizi, na haki za kijamii.
Elimu ya Kiraia
Mara jamii inapoundwa kanuni ambazo zinawekea msingi uraia, waelimishaji wanaweza kufikiria kuwa watu wanahitaji elimu ambayo inawawezesha kuwa kama raia wa kawaida. Haki, majukumu na wajibu wa uraia utasisitizwa, na hatua hii ya kielimu inaweza kuhusishwa na mchakato wa kuwafanya wahamiaji kuwa raia halisi wa nchi. Kwa haya, inaweza kuanzisha mjadala mkali kuhusu msimamo wa kisheria wa raia na namna ambavyo utambulisho na uhusiano wao na taifa unaelezwa. Mwelekeo wa kijumla unaweza kuwa wa usimilishaji, lakini pia kutakuwa na mipango ile ambayo itahisika na mambo kama yale yaliyoelezwa katika aya ifuatayo na yaliyoendelezwa kivyake kwa sababu za mjadala huu pekee.
Elimu kwa Uraia
Uraia unaweza kufasiliwa sio tu katika mitizamo ya kisheria lakini katika mitizamo ya jinsi watu wanatekeleza majukumu yao kwa watu wengine au kwa taifa, au pale ambapo taifa halipo, kwa maisha ya kijamii. Elimu katika kuhimili uraia, ambayo inajitokeza kama seti ya mahusiano na majukumu ya kila mtu na uitikiaji wa serikali kwa mtu huyu na watu wa jamii yake, itazingatia ujuzi wa uraia. Ujuzi kama huo, wakati ambapo unatambulishwa, unafanya mtu kuwa raia. Kabla ya hapo wao ni watawaliwa.
Ujuzi huo unaweza kuhusisha ule ambao ni muhimu katika kushiriki katika uchaguzi, au kufanya maamuzi ya kijamii, au kushiriki katika mjadala wa umma. Unaweza vilevile kuhusisha ule ambao ni muhimu katika kuhakikisha kuwepo na taifa linalofanya kazi au wa kushirki katika ujenzi wake. Ujuzi huu unaweza kuhusisha utetezi, uandaaji, na uhamasishaji wa sera ya umma. Mipango ya elimu inayohusika na uraia inajengwa kwenye mchukulio kuwa uraia unawezekana. Katika maneno mengine, yawezekana kufanyika katika jamii ambapo dhana ya uraia imeimarishwa na pale ambapo utendaji wa uraia unawezekana. Jamii kama hizi zina, iwewazi au isiyo wazi, taratibu ya kikatiba inayotambua watu binafsi na mchango wao kwa uongozi na uhusiano wao kama wahusika huru katika nchi na kuhusiana na taifa.
Elimu ya Kisiasa
Wale ambao wanachukulia miendo ya maisha ya umma katika serikali, bila kujali ilivyoimarishwa, kuwa muhimu wanaweza kueleza kazi yao kuwa elimu ya kisiasa. Pale ambapo siasa zipo, watu binafsi wanahitaji kukuza elimu (uwezo wa kusoma na kuelewa maisha ya kisiasa yaliyo karibu nao ) na wanahitaji kujifunza njia za kushiriki katika maisha ya kisiasa.
Uchanganuzi wa kijamii, uchunguzi wa diskosi na mawasiliano, uelewaji wa njia ambazo mifumo ya kisiasa na ya kijamii inaingiliana na namna ambavyo zinahusiana na kugawa uongozi pia itakuwa sehemu ya Mpango wa elimu kama huo.
Mafunzo ya Uongozi
Muundo wa mwisho wa elimu kwa raia unaelezwa vizuri kama mafunzo kwa uongozi. Mafunzo kama hayo yanachukulia kuwa uongozi unaweza na unafaa kufunzwa na kisha kutumiwa na wanadamu. Mpango utazingatia maarifa na mahusiano mbalimbali ya uongozi. Huenda wakazingatia masuala ya uongozi wa kibinafsi na wa kisiasa na mwelekeo dhabiti wa manufaa na kimaadili kwa uongozi. Kuna aina mbili za elimu kwa Wapigakura. Wakati ambapo zina mambo mawili sawa, na kihistoria zinaonekana kushinikizwa na haja matamanio sawa, zinajidhihirisha zenyewe katika jamii tofauti au matabaka tofauti katika jamii.
Utumizi mzuri wa Mamlaka:
Kanisa nyingi, miungano, miungano ya vijana (muungano wa maskauti ni mfano mmoja), na mashirika ya kutoa msaada kama vile Klabu ya Rotary (ya kibiashara) hutoa mafunzo ya uongozi ambayo inaangazia ukuwaji wa ujuzi, maadili, matendo mema ya kijamii, na kadhalika katika mfumo wao wa utenda kazi.
Kupata uongozi:
Kwa upande mwingine, miungano isiyo na uwezo wa kupata uongozi katika jamii hutumia mipango ya mafunzo kwa uongozi ambayo ni ya kimajaribio katika methodolojia, na, labda ni ya kushangaza, huendeshwa na wale ambao wamenyimwa uongozi katika jamii.
Kiini cha mjadala kuhusu istilahi mwafaka ni mjadala kuhusu haja ya elimu kama hiyo. Lengo lake ni kutoa mafunzo ya nidhamu na ujuzi ambayo humwandaa mtu kwa jamii ambayo inatarajiwa, au je, ina jukumu muhimu katika kuwawezesha watu kushughulikia na kubadilisha mazingira yao? Desturi hutofautiana kwa kiwango kikubwa. Kwa bahati nzuri, katika jamii ambazo hazijazongwa na vita, kuwepo kwa habari ya mara kwa mara na makubaliano ya kijumla ya kimataifa yanayoruhusu demokrasia yamemaanisha kuwa watu wengi wamenyimwa nafasi na wengi wa watangulizi wao. Wanaweza kuamua mstakabali wao iwapo tu wanania, ujuzi na uhuru wa kiwango fulani dhidi ya mahitaji na woga.
Ujumbe Wastani wa Elimu kwa Raia
Hapa kuna angalau ujumbe wastani tano (au maudhui) ambao unafaa kushughulikiwa kwa Mpango wa elimu kwa raia.
- maana ya demokrasia
- jukumu, wajibu na haki za wananchi
- uongozi bora
- kanuni na taratibu za kidemokrasia
- taasisi na sheria za kidemokrasia
Utangulizi
Sababu ya elimu kwa raia ni kuwahimiza wananchi kushiriki kikamailifu katika maisha ya kisiasa ya kijamii na nchi ambayo inazingatia maadili na kanuni ya demokrasia. Kwa kutumia maelezo haya kama lengo la kimsingi, wale ambao wanatayarisha na kuendesha mipango ya elimu kwa raia wameunda aina mbalimbali katika silabasi au mitalaa yao.
Katika kiwango cha shule, taasisi katika Australia na Marekani wameweka viwango au mahitaji yanayoeleza kwa uwazi yale ambayo yanafaa kuzingatiwa katika Mpango wa elimu. Utaratibu kama huo hauonekani kuwa katika nchi zingine, au hupo kwa hatua sisizo rasmi za watu wazima. Japo elimu kwa raia, ikiwa itatekelezwa katika shule pekee, inauwezo wa kujibadilisha na kuwa katika kiwango sawa na masomo mengine na hivyo kupoteza maana baada shule au hata wakati wa kipindi cha shule kwa sababu ya nafasi adimu (chache) kwa watoto kushiriki katika maisha ya kisiasa.
Kuna makubaliano kadha kuhusu aina za ujumbe ambao umetengenezwa katika taarifa za kinadharia ambazo zina unda msingi wa mtalaa wastani wa elimu kwa raia kwawatu wazima. Ujumbe huu utajalizwa na vifaa (vya kimaandishi) zaidi ambavyo vinazingatia kwa makini historia ya kila jamii na jinsi ambavyo inashughulikia dhana idhini isiyotarajiwa na utohakika wenye mipaka, na kanuni na taratibu za demokrasia zao mahususi. Ujumbe huu wastani utahusu mada zifuatazo:
Maana ya demokrasia – ufafanuzi, aina, na changamoto
Kama mfano wa kile ambacho waelimishaji wanaweza kuandaa kuwaongoza katika mjadala wao wa eneo hili la mada na kutengeneza vifaa (vya kimaandishi) vya elimu, nyaraka imetengenezwa ambayo ina shughulikia ufafanuzi wa demokrasia tazama Maana ya Demokrasia. Nyaraka hiyo hiyo pia inapendekeza njia ambazo suala la mada linaweza @@@@kutumika shughuli za kielimu na kuwashilishwa kwa makundi ya wale wanaojifunza.
Jukumu, Wajibu na Haki za Wananchi
Tazama Elimu ya Kimsingi kwa Wapigakura kwa mjadala unaohusu mada hii na umuhimu wa kushughulikia haki na wajibu. Wananchi binafsi wanauwezo mdogo kwa kulinganisha na serikali isipokuwa serikali hiyo iheshimu na kulinda haki za wananchi, Bila ya ulinzi huo ni vigumu kuzungumza kuhusu wajibu. Kwa uhakika, wajibu wa mtu huenda ukawa wa kulazimisha serikali kutambua haki za kibinadamu na demokrasia.
Uongozi /Utawala bora
Mwananchi amepewa uwezo ikiwa tu anaweza kuelewa jinsi serikali inafanya kazi na ana vigezo vya kupimia utendakazi wa serikali hiyo. Kwa kuwa serikali imeendelea kuonekana kama mchakato ambamo taifa, maafisa waliochaguliwa na watu binafsi wakishirikiana kwa pamoja hutawala kwa ushirikiano, imeitwa uongozi/utawala. Uongozi/utawala hauhitaji tu kushiriki kwa wananchi lakini pia kuwaelimisha wananchi hao kuhusu demokrasia na ushiriki.
Hata hivyo uongozi/utawala bora unafaa kutimiza vigezo fulani, kama vile uwazi, uhalali, uwajibikaji, uitikiaji na utendakazi.
Kanuni na Taratibu za Demokrasia
Demokrasia ina maadili. Muhimu zaidi, demokrasia inahusu tamaduni, tambiko, na taratibu ambazo zinakubali wananchi kufanya uamuzi, kuakikisha kuwepo kwa serikali wakilishi, na katika vipindi maalum kutoa nafasi ya kupimia utendakazi ya serikali hiyo.
Maadili au kanuni hizi zinadhihirishwa katika matendo. Kwa hivyo, wananchi ni lazima waelewe kanuni, ambazo zinaweza kuwa bia (za kilimwengu), na jinsi ambavyo jamii tofauti zimejengwa ili kuhakikisha kuwa kanuni hizi zinadhihirishwa. Wananchi pia watataka kuangazia jinsi tamaduni za nchi yao zinavyoendeleza au kuhujumu kanuni za demokrasia.
Ni muhimu kutofautisha kati ya kanuni na tamaduni za demokrasia, kwani kufanya hivyo kunaweza kuzuia nchi kuiga (kutoka mataifa ya kigeni) tamaduni ambazo zinaweza kuchukuliwa tu (bila kujua) kuwa muhimu kwa demokrasia. Badala yake, nchi zinaweza kuchunguza ufaafu wa tamaduni kama hizo na kama kanuni hizo zinaweza kudhihirishwa katika miundo ya kiutamaduni inayofaa zaidi.
Taasisi na sheria za Kidemokrasia
Kila nchi uenda ikawa na mkusanyiko wake wa taasisi na sheria za kidemokrasia. Taasisi na sheria hizi za kidemokrasia zinafaa kukubaliwa na kueleweka ikiwa watu wanatarajiwa kuzitumia, kusaidia katika kuziboresha au kuzirekebisha, na kuzibadilisha au kuzifutilia mbali.
Waelimishaji wanafaa kutafuta njia kuhakikisha kuwa vifaa (vya kimaandishi) vinavyostahili kwa nchi yao vinaandaliwa ili kuzingatia mada hizi. Inawezekana kupata habari za kijumla na za kiulinganishi. Wakati ambapo haya ni muhimu, ni pale tu ambapo habari hizi za kijumla na linganishi zinaposhughulikia moja kwa moja matamanio ya kundi linalojifunza ndipo zinapopata umuhimu. Kwa hakika, waelimishaji wanafaa kuwa tayari mara kwa mara kupata mifano mpya kutoka sehemu mbalimbali na kwa wakati tofauti ili kufananisha na hali zao.
CIVICS