Kila mara kumekuwepo na mvutano baina ya michakato ya demokrasia ya uwakilishi na chaguzi zake za mara kwa mara – kutoa bunge ambazo wakati zinapochukua shughuli za kufanya maamuzi kwa kushirikiana na wananchi – na miundo ya kufanya maamuzi iliyo ya moja kwa moja zaidi. Kwa hivyo wakati ambapo nchi nyingi zina taratibu za kura za maamuzi na kura za maoni, mara nyingi kura hizi hutumiwa tu nyakati muhimu zaidi.
Hata hivyo kuna baadhi ya nchi ambapo demokrasia ya moja kwa moja – hufafanuliwa kama mchakato wa kufanya maamuzi, na michakato hii bila shaka si ya pekee ambayo hustawisha demokrasia – mara nyingi hutumiwa. Uswizi ni mojawapo wa nchi za aina hii. Mataifa fulani katika Marekani yanakubali mapendekezo ya wananchi kuonyeshwa kwenye karatasi za kupigia kura katika hali fulani.
Elimu kwa raia wakati wa kura za maamuzi au maoni zinaweza kuwa na miegemeo kwa njia rahisi. Ni vigumu sana kuendesha aina yoyote ile ya elimu ambayo haihitaji kulinganisha chaguo, na inatofauti ndogo sana na ile ya kulinganisha chaguo – hasa kwa kuwa maswali ya maamuzi mara nyingi huwa yametungwa ili kulazimisha chaguo rahisi kuhusu masuala changamano.
Bila shaka kuna masuala fulani ya kiutaratibu ambayo yanaweza kuwa sehemu ya Mpango waelimu – je, kura ya maamuzi ni nini? je, unashiriki namna gani? Scc aa, mn8k lipi?, kwa nini linaulizwa?, na, muhimu zaidi, athari za chaguo lolote lile zitakuwa gani? Na katika hali zingine haitawezekana na haitakuwa muhimu kuunda vifaa (vya kimaandishi) vya kielimu ambavyo vinatoa kauli za kutetea kila upande wa suala lenyewe. Pale ambapo taasisi inatoa vifaa vya kielimu ina heshima ya kutokuwa na miegemeo huenda ikawezekana kuunda vifaa kama hivyo. Badala ya hayo waelimishaji wanaweza tu kuhakikisha kuwa Wapigakura wamezuiliwa kupata na kuelewa vifaa (vya kimaandishi) ambavyo vina miegemeo zaidi ambayo inatolewa na kambi (makundi) mbalimbali.
Kwa sababu kura za maamuzi zinachukuliwa kuwa zinazojibu maswali kubwa yanayoathiri siku zijazo, na katika shughuli hiyo zinauwezo wa kukashirisha au kuaibisha sehemu kubwa za jamii iwapo zitashindwa, nyakati hizi huwa zenye hofu hata katika demokrasia zilizoimarika zaidi. Katika mataifa yasiyo imara kura hizi za maamuzi zinaweza kuwa chanzo cha mzozo.Waelimishaji watawajibika kwa kuwaanda watu kushinda au kushindwa, watatafuta njia mbadala za kuendelea mbele na wataendesha mipango ambayo itawahimiza uvumilianaji wa kisiasa.
Baada ya kukamilika kwa kura ya maamuzi, waelimishaji watataka kuanzisha mipango ambayo inashughulikia athari na maana ya maamuzi yaliyofanywa- ambayo huwa vigumu sana kuyatambua. Kura ya maamuzi iliyofaanyika nchini Ufaransa na Uholanzi zimedhihirisha kuwa matokeo yanaweza kuwa yasiyotarajiwa na kuwa mara nyingi huwa hakuna Mpango wa pili.
Katika Kolumbia ya Kiingereza jaribio la kiuvumbuzi katika aina tofauti ya demokrasia ya moja kwa moja (kutathminisuala changamano na lenye hisia kuu kuhusu mabadiliko katika mfumo wa uchaguzi) lilisababisha kuitwa kwa bunge la mwananchi kuwakilisha wananchi wote. Mwelekeo huu wa kisheria wa kufanya maamuzi kuhusu masuala ya umma unatoa mchakato wa kufanya maamuzi ambao ni tofauti na unaohusisha mashauriano, na kwa sababu ya haya unakubali mchakato wa kielimu kwa wale wanaoshiriki na wale ambao wanasubiri nje ya chumba cha bunge.