Elimu kwa raia inaweza kufafanuliwa kwa mapana katika njia ambazo zinaifanya kwenda nje ya siasa za kiuchaguzi na usimamizi wa uchaguzi. Ni jambo linalowezekana kuwa mtu ambaye anawajibikia elimu kwa Wapigakura anaweza pia kuhusika katika shughuli pana ya elimu kwa raia. Kwa hakika, kuna kitu ambacho kinaashiria kuwa elimu kwa Wapigakura ni muungano kamili wa habari kwa Wapigakura na sehemu fulani za Mpango wa elimu kwa raia, yaani, wale ambao wanashughulika na uchaguzi.
Elimu kwa raia inaendeshwa kwa mapana katika miktadha isiyo rasmi ya elimu kwa watu wazima, ingawa kuna sehemu za elimu rasmi katika shule. Sehemu hii inapendekeza kuwa elimu kwa raia katika demokrasia (asasi, nchi na kadhalika) inasomwa na kufunzwa vizuri katika juhudi za harakati za kuanzisha kuhimili demokrasia.