Kwa ajili ya eneo ili la mada, dhana elimu kwa raia inatumika kusimamia jukumu pana la uelemishaji wa wananchi ili waweze kuwajibikia majukumu na wajibu wao katia mataifa ya kidemokrasia na waweze kutimiza haki zao kama wanadamu huru.
‘Elimu kwa Raia’
imepata uungwaji mkono kama ufafanuzi wa shughuli hii ya kuwapa watu uwezo na uhuru, lakini bado ina athari chache za kazi ya ustaarabishaji na uanzishaji wa miji ambayo waelimishaji stadi wanaofanya kazi katika miktadha mbalimbali wanashughulika nayo.
Ni mikitadha hii mbalimbali ambayo inaunda msingi wa sehemu zifuatazo za eneo la mada. Wakati ambapo kuna maudhui muhimu yanayohusika katika elimu kwa raia miktadha ambamo maudhui haya yanazingatiwa na kuendelezwa imekuwa ya aina mbalimbali. Na kama jukumu la elimu katika kuichunguza miktadha hii na kuifanya ya manufaaa kwa wananchi – na wananchi kuwa wa kufaa miktadha hii – imekuwa muhimu sana, kwa hivyo ni muhimu kwa waelimishaji kuzingatia tofauti na malengo yao.
Maudhui haya ni yale yanayohusu maono, maadili, tabia na mienendo.
Uchunguzi wa elimu kwa raia uanza kwa uchunguzi wa demokrasia na dhana zinazohusiana nayo za mwananchi na mashirika ya kijamii. Wale ambao wanajishughulisha katika elimu kwa raia wana maono ya kuwapa uwezo wananchi ambao wanajikusanya wenyewe kwa kujitegemea na kuleta athari katika jamii ambako demokrasia ya uwakilishi na ya moja kwa moja inaleta amani, maendeleo na uhuru wa kibinafsi. Dhana hizi zote ni za kushindaniwa. Hata hivyo, ingawa miaka ya 1990’s na imani zao katika kufana kwa demokrasia kama mfumo wa serikali, wakati ambapo elimu kwa umma ilipata nguvu mpya imeruhusu miaka yenye uangalifu mkubwa ambamo vita na ugaidi umejitokeza upya kama vyombo vya ujenzi wa taifa na uendelezaji wa uwezo (wa utawala ), Mpango wowote wa elimu kwa raia unafaa kutoa maono kwa waelimishaji na wanaoelimishwa.
Maono
Maadili ya raia yamekuwa madhumuni makuu katika mitalaa kadha na miradi ambayo imeundwa kwa kubadilisha kiini cha elimu kutoka kwa kitendo cha kushughulikia habari na elimu pekee – kujifunza kuhusu siasa za nchi fulani, au historia ya uundaji wa katiba na jinsi katiba hiyo imetumika au haijatumika vizuri – hadi kwa uzingatiaji wa wajibu wa kibinafsi wa yule anayeelimishwa wa kuweza kuwa na nidhamu njema katika jamii ya kidemokrasia ambamo anaishi. Orodha za maadili zimeundwa ambazo zimechukuliwa kuwa mwafaka zaidi kwa maisha ya aina hii. Maadili haya ni pamoja na heshima kwa wengine, wajibu wa pamoja kwa jamii, kuzingatia katiba na haki za kibinadamu, amani na urafiki katika masuala ya mashinani na ya kitaifa.
Maadili
Katika baadhi ya taipolojia (maandishi yaliyopigwa chapa) za kutoa mafunzo, maadili na tabia yanaingiliana yenyewe kwa yenyewe na vilevile yanaingiliana na ujuzi kuhusu masuala ya kiraia. Hata hivyo wote wanakubali kuwa elimu kwa raia inafaa kufunza tabia ambazo zonawawezesha watu kuunda maisha ya kidemokrasia, bila kujali mfumo mahususi ambamo wanajikuta. Miongoni mwa tabia hizi ni zile ambazo ni rahisi zinazohusu ukabilianaji na mizozo isiyo ya kivita; kuipa mwelekeo, kuwasilisha na kukuza matamanio na mahitaji ili kwamba matamanio yanayong’ang’ania nafasi na mahitaji yaweze kutambuliwa na kusuluhishwa; kupiga kura; kama umma, mtu binafsi na kadhalika.
Tabia
Kila mara jamii ni changamano – na jamii za kidemokrasia zinafaa kuanzisha, kwa misingi ya historia zao mahususi na usawazishaji wa mivutano, tamaduni ambazo zinawawezesha kuafikia vigezo vya chini vinavyohitajika kwa jamii kama hiyo (tazama Maana ya Demokrasia). Baada ya kuanzisha tamaduni na taratibu hizi – na katika harakati za kuibadili upya na kuifanyia mabadiliko ili kufikia mahitaji ya sasa – jamii hutaka kuwaelimisha wananchi wao katika matumizi ya na kushiriki katika tamaduni na taratibu hizi.
Tamaduni
Kufikia hapa hivyo, elimu kwa raia inalenga kuwapa watu nguvu na uwezo wa kushiriki kikamilifu katika jamii ya kidemokrasia au kuunda jamii ya kidemokrasia lakini miktadha hutofautiana, na changamoto zinazowakabili waelimishaji hivyo hutofautiana. Ni muhimu kuwa maamuzi katika uundaji wa mipango, utafutaji wa vielelezo na vifaa (vya kimaandishi), utafutaji wa usaidizi kwa wataalamu wengine na uwezeshaji watu kufikiria kuhusu tofauti hizi. Je, mwelimishaji wa raia anahusika katika uhifadhi na wendelezaji taifa la demokrasia (tazama Elimu kwa Raia katika Demokrasia zilizohimarika), ujenzi au ujenzi mpya baada ya vita au mzozo wa wenyewe kwa wenyewe (tazama Ujenzi upya Baada ya Vita), utunzaji wa demokrasia inayochipuza (tazama Elimu kwa Umma katika Demokrasia zinazochipuza), au kuzibadilisha jamii (tazama Mifumo ya Serikali za Kimabavu na Mataifa Dhaifu)? au mwelimishaji ni sehemu ya kundi ambalo linashughulikia mzozo usio imara ambapo dhana ya taifa haina maana kwa dharura iliyopo (tazama Elimu kwa Raia Wakati wa Dharura [hali ya hatari).
Picha:
OSCE Timu ya Uangalizi wa Uchaguzi katika Chaguzi za Urais katika Kyrgyzstan,2009 na mcaton imeidhinishwa chini ya Creative Commons Attribution-Noncommercial-No Derivative Works 2.0 Generic License.