Jukumu la kutoa elimu kwa raia mara nyingi limepewa idara za elimu, tume za kusimamia uchaguzi na taasisi za kisheria. Taasisi za kitaifa kama hizo zinaweza kuwa na jukumu lililo sehemu ya jukumu la kijumla kuhusu haki za kibinadamu, masuala ya kikatiba, au ukuaji wa kijamii.
Pia kumekuwepo na mabaraza ya kitaifa yanayohusisha sekta mbalimbali yaliyoanzishwa kupitia kwa vipengele vya kisheria au muungano wa kujitolea.
Na hatimaye, kuna midhihiriko ya mashirika na miungano ya kimataifa katika nchi.
Kila mojawapo wa mashirika haya lina nguvu / uzuri wake na changamoto zake.
Kama nchi itahimiza na kuendeleza elimu kwa raia, itakuwa muhimu kuwa mjuzi wa katikati ambaye atawavutia washika dau wengine. Hii inahitaji kuwa na uwezo wa kutumia uwezo / nguvu fulani na ushawishi – kupitia kwa ubora wa kisheria, uzingatifu wa bajeti, au uongozi wa kiakili (bora). Pale ambapo ubora huu (wa kisheria) haupo, elimu kwa Wapigakura itasalia kuwa isiyo kamilifu hata kama itafuata muundo wa Kijerumani (tazama hapo chini). huenda hili lisionekane kama tatizo na hata inaweza kuonekana kuwa muafaka kwa jamii ya kidemokrasia na kuruhusu sauti nyingi na taasisi nyingi kuingiliana katika njia ambazo zinaimarisha jamii-lakini inaleta kiwango cha utepetevu wa kitaasisi ambao hutatiza ubunifu wakati wa mgogoro.
Muundo wa Kijerumani
Ujerumani imeanzisha taasisi ya kimajimbo ya poitische bildung ambayo hupata fedha za kijimbo ambazo hutumia kwa Mipango yake na ambazo husambaza kupitia kwa taasisi, vituo vya kimaeneo na mashirika yasio ya kiserikali. Kupitia kwa uundaji wa vifaa vya kielimu na kupitia kwa motisha na inayokubaliwa kisheria, Ujerumani ina mfumo wa elimu kwa raia ambao ni wa kidemokrasia, ni faafu na unaogharamiwa kitaifa na ambao elimu rasmi, elimu isiyo rasmi, taasisi za serikali na mashirika ya kijamii yanajukumu. Huu ni mfumo ambao umejikita kwa zaidi ya karne moja kiasi kuwa huzungumziwa tu katika nchi na haizungumziwi na wale wanaotengeneza vielelezo vya elimukwa raia. Mfumo huu unastahili uzingativu zaidi kuliko unavyopata.
Taasisi za kati / shirikishi
Chaguo la taasisi ya kati au shirikishi – idara ya serikali, taasisi ya kisheria kama vile tume ya kusimamia uchaguzi au tume ya kupigania haki za kijamii, chuo kikuu au kundi la vyuo vikuu au baraza la kitaifa kuhusu elimu kwa raia – itaamuliwa na nchi binafsi. Katika baadhi ya hali, taasisi kama hizo zinaweza kuibuka kutokana na seti ya hali fulani mahususi. Bila kujali namna itakavyoibuka, taasisi hiyo inahitaji raslimali ili kuweza kuwaleta pamoja washika dau wengine na kuunda Mpango wa kitaifa wa aina fulani.
Mabaraza ya kusimamia uchaguzi huenda yasiwe mashirika ndiyo mwafaka tu: yana shurutisho za uchaguzi, upungufu wa wafanyikazi wa kuendesha uchaguzi, na haja ya kutokuwa na mwegemeo au upendeleo wowote. Tume za kupigania haki za raia pia zinakabiliwa na baadhi ya matatizo sawa na hayo, ingawa yamezoea hali ya ‘kufanywa kuwa ya kisiasa’ na kuweza kuistahimili hali hii. Nchini Afrika Kusini Mahakama ya Kisheria inakuza amri ya kielimu na eneo lake limevutia na litaendelea kuvutia wale ambao wanahusika katika ukuzaji wa demokrasia na elimu kwa raia.
Kwa sababu ya umuhimu wa elimu kwa raia kutoonekana kuwa shughuli iliyoanziswa kulinda serikali na kunufaisha uongozi unaoshikilia mamlaka bali kuhimili / kusaidia mfumo wa kidemokrasia, mashirika shirikishi katika taifa huenda yakatiliwa shuku hata katika hali shwari zaidi. Ushirikiano wa kiwango fulani na serikali au kundi lisilo la kiserikali huenda ukafaa, na hivyo mabaraza ya kitaifa yanafaa kuzingatiwa.