Kote ulimwenguni, miungano ya kuendeleza elimu kwa umma ambayo inahusishwa na demokrasia au maisha ya kijamii imeanzishwa pamoja na mitalaa yao ya kienyeji na inayojisimamia / tenge. Mara nyingi miungano hii imeendeshwa katika misingi ya mwalimu-mwanafunzi, pale ambapo walimu ni watu wenye ushawishi / ukuu fulani katika jamii. Mifano ya miungano hii ni pamoja na ile ambayo inajulikana kama ‘shule za jandoni’ katika sehemu mbalimbali barani Afrika, shule za kidini ambazo zinaonekana mara nyingi katika jamii za Kiyahudi na Kiislamu, na vilevile shule zinazohusishwa na miugano ya wafanyikazi na makundi mbalimbali ya kijamii na kisiasa. Hivi maajuzi, mashirika ya kupigania haki za kijamii yamebuni njia za kuunganisha Mipango yao ya muda ya kielimu katika muundo mmoja mpana kutokana na imani yao kuwa kuna athari ya kudumu kutoka kwa uwekezaji wa aina hiyo.
Baadhi ya matukio haya ya hapo awali yana chimbuko lake katika muungano fulani mahususi ambao waanzilishi wake asilia wanauona kuwa uliokuwa na athari kubwa katika ukuzaji wa demokrasia katika nchi za Scandanavia. Kuna uendeleaji wa kukuza mawazo haya na taasisi za elimu kwa umma ambazo zinaisaidia katika nchi zinazoendelea. Kwa hivyo ni muhimu kuangalia labda vielelezo vya elimu kwa umma ambavyo vimetaasisishwa zaidi na vina historia ndefu zaidi na ambavyo vinahusishwa moja kwa moja na demokrasia.
Shule ya kwanza ya jadi ilifunguliwa nchini Denmark katika mwaka wa 1844 kutokana na ushawishi wa Nikolaj Grundtvig, na ‘shule hizi za maisha’ zilizokuwa na mwalimu mmoja, boma na jamii ndogo ya wanafunzi walioishi humo mara moja zilikuja kuwa sehemu ya maisha ya kidemokrasia ya jamii za Kinodiki (Nordic).
Sasa hivi kuna shule ambazo zina misingi yake katika kanuni za Grundtvigian katika nchi nyingi, na zingine ambazo, huku zikihifadhi au kuendelea kutumia jina la shule ya jadi au shule ya upili ya jadi, zimebadilika na kwa kiwango kikubwa kuwa taasisi za kiufundi ambazo zinazingatia kwa kiasi fulani hali ya kisiasa na uhusiano dhabiti na serikali iliyo katika mji au eneo ambako shule hizo ziko.
Katika midhihiriko yao ya kwanza kulikuwa na uhusiano wa moja kwa moja baina ya harakati za kuzifanya jamii za Kinodiki (Nordic) kuwa za kidemokrasia na shule ya kijadi. Zilidhamiriwa “kuchangamsha na kuzindua, lakini kwanza na muhimu zaidi kuchangamsha” (Christen Kold, 1866), na zilisisitiza kuendeleza mtalaa wao wenyewe katika wakati ambapo elimu rasmi ya kijumla ilikuwa ikieneza umbali wake polepole bila ya athari za moja kwa moja kwajamii za wafanyikazi na wakulima.
Baada ya muda, shule ya upili ya jadi iliendeleza manufaa mahususi ya kijamii wakati ambapo watu binafsi walikuwa wakitafuta nafasi yao, wakitafuta jukumu lipya katika jamii, wakitaka kukuza ujuzi mpya, au wakiingia kipindi kipya cha maisha. Kuna haja maalum katika watu wenye mahitaji maalum ya kielimu na katika jamii ya kuhamahama. Shule mbalimbali za kijadi zina haja maalum na mapendeleo tofauti, lakini zote zinafanya kazi kulingana na maadili mbalimbali ambayo yalielezwa maajuzi na mkuu wa Shule ya Upili ya Alma Folk huko Uswidi kama:
- elimu huru (bila mapendeleo) na bila malipo kwa watu wazima
- (elimu) ya kujitolea na isiyo rasmi ingawa inayotolewa kupitia kwa taasisi rasmi
- taasisi ambazo hufanya kazi kwa imani kuwa wananchi wako huru na wana haki ya kushiriki katika sehemu zote za jamii ya kidemokrasia
- kutengeneza hali ambapo watu wanaendelea kutafuta maarifa kwa njia huru
- kuchochea hali ya kutaka kujua na uwazaji makinifu
Shule za jadi zilihimiza uimbaji, matumizi ya lugha moja (sawa), na uelewaji wa siasa na maisha ya umma. Elimu hii ni muhimu katika ujumla wake, lakini isiyozingatia manufaa kutokana na sababu kuwa inazingatia tu ujuzi wa kikazi au kufaulu katika mitihani. Baada ya muda mfupi, wakuu hawa walichukuliwa pia na shule za miungano ya wafanyikazi, na muungano wa shule za jadi hivi leo bado zina ukubalifu na uungwaji mkono kwa upana na jamii licha ya elimu rasmi kwa wote.
Muungano huu umeunganishwa na muungano wa kundi la kiusomi, ambalo hutumia makundi yenye mpangilio na inayotoa elimu ya wenyewe kwa wenyewe kwa watu wazima ambao hukutana mara kwa mara kujifunza ujuzi fulani au kusoma suala au somo fulani. Makundi haya ya kiusomi huhimiza kujisimamia, mafunzo ya kudumu na mafunzo (ya muda) mahususi kutoka kwa wengine na katika ushirikiano na uhusiano sawa. Makundi ya kiusomi kwa hivyo yanatoa nafasi zenye manufaa mengi na gharama za chini kwa elimu kwa watu wazima na ukuzaji wa raslimali ya kijamii.
Baadhi ya nchi zinazoendelea (ambazo ni pamoja na Tanzania na Afrika Kusini) zinafanyia majaribio makundi ya kiusomi na shule za kijadi kwa sababu ya athari zionekenazo ambazo makundi na shule hizi zimekuwa nazo kwenye ubora wa maisha na demokrasia katika nchi za Kinodiki (Nordic).