Ikiwa ni kweli kuwa watu hujifunza kutokana na tajriba (uzoefu), na ikiwa idadi kubwa ya watu watashiriki katika maisha ya kisiasa – katika jamii za kidemokrasia na, bila kujali madhara ya kibinafsi, jamii zisizo za kidemokrasia – bila ya manufaa ya “elimu kwa raia”, hapo lazima pawe na njia zingine ambazo watu wanaelimishwa. Na kwa uhakika njia hizo zipo. Njia ya kimsingi ya kielimu ya kutoa elimu kwa raia imekuwa na itaendelea kuwa kupitia kwa maingiliano ya kijamii. Pale ambapo mchakato huu ni muhimu, na pale ambapo wale wanaohusika nao ni wanadhihirisha falsafa zinazoongoza juhudi zao na wanitekeleza, viongozi wanajitokeza, wananchi wanakuwa na bidii, na mashirika yanapata nguvu zaidi.
Waelimishaji huenda wasiweze kunakili hali za kijamii ambayo ina saidia katika uundaji wa muungano, muungano wa kijamii wa raia, na siasa ambazo zinaendeshwa kwa njia za kidemokrasia. Lakini wanaweza kutumia michakato hii ya kijamii katika hali ambazo zinaleta uwezekano kuwa watu watajifunza na kuendelea. Hili linaweza kufanyika tu ikiwa waelimishaji wameunganishwa kwa njia fulani na kelele za maisha ya kisiasa. Mashirika haya ambayo yanachanganya uhamashishaji wa kisiasa na huduma za kielimu, au mashirika ya kielimu ambayo yana uhusiano na wale ambao wanahusika na masuala ya kijamii, au hata waelimishaji ambao wameajiriwa kimsingi kama watoaji wa mafunzo katika mashirika, wananafasi zaidi ya kuhakikisha kuwa elimu kwa raia inafanyika katika na kupitia kwa kuhusisha masuala ya umma na mabadiliko ya kijamii ambayo ni muhimu miongoni mwa shule za demokrasia.
Inawezekana kuwa shule kama hizo zinaweza kuundwa kupitia kwa ukuzaji wa busara wa mabaraza ya umma, maisha ya ushirika, na shughuli za ujima. Wakati ambapo haya yanaweza kuibuka bila kupangwa, wale ambao wanahusika na shughuli ya elimu kwa wapigakura ambayo wanaweza kuyahusisha haya kama sehemu za mipango yao. Mijadala ya umma kuhusu masuala haya, kwa mfano, inaweza kutoa nafasi kwa watu kujifunza kuhusu uhuru wa kutoa maoni, kanuni zinazotawala mijadala, namna ya kuthibiti mabishano, na taratibu za kufanya maamuzi hata ingawa hakuna lengo la kielimu ambalo linatazamiwa na wale ambao wanahudhuria.
Kushiriki kama Elimu
Kwanza, waelimishaji watafurahia sababu kuwa wananchi wanashiriki katika maisha ya umma na ya kijamii, bila kujali ni suala gani linalowashawishi. Kushiriki pekee kunaweza kuboresha uelewa wa watu kuhusu maisha ya kisiasa, lakini bila ya kipengele cha kielimu na kuwazia uhamasishaji (wa kisiasa) wao, uelewa huu unaweza kuwa pungufu na hata husio sahihi. Jukumu la mwelimishaji kwa kulinganisha na kushiriki katika siasa na shughuli za raia lina sehemu mbili:
- kuongeza uwezo wa watu kushiriki katika shughuli hiyo ya kisiasa au ya kijamii.
- kuunda njia ambazo watu hawa hawa wanaweza kuwaza kuhusu na kujifunza kutokana na tajriba za shughuli za kisiasa na kiraia.
Bila shaka, hakuna hakikisho kuwa matokeo ya ushiriki wa wananchi utakuwa wa manufaa. Kunaonekana kuwa na hali kadhaa ambapo watu wamepoteza imani na wameamua kuchukua njia za kimabavu na zisizo za kidemokrasia za kutimiza mahitaji yao ya kisiasa. Katika hali zingine watu wamekubali hali iliyopo. Hata hivyo ushaidi hauonyeshi kuwa inawezekana kwa watu kukubali kanuni za demokrasia, na hata katika hali ambapo hakuna msaada kutoka kwa jamii kwa kujitolea huku, kuhusika katika shughuli ambazo zinazidisha ufaafu wao baada ya muda fulani.
Bila shaka hii imekuwa hali katika nchi ambapo miungano ya kijamii imeimarisha tamaduni za kidemokrasia na ushiriki wa umma ambao huwa unapendelewa. Tamaduni hizi, hata hivyo, si lazima ziweze kusafirishwa, na mafunzo yaliyopatikana kutoka jamii moja kuhusu namna ya kuafikia demokrasia huenda yasiafiki kwa njia rahisi katika nchi ambapo kuna katiba ya kidemokrasia lakini uongozi mzuri ndilo tatizo kuu.
Kanuni ya kuwahimiza watu kufanya kazi pamoja, kuimarisha usaidisi kwa matakwa yao wakiwa miongoni mwa kundi moja linaloleta pamoja watu tofauti lakini wanaoweza kushirikiana, kwa kundi hili jumuishi kuendeleza taratibu za kufanya maamuzi na tabia ambazo ni za kidemokrasia, na kisha kuwakabili wale ambao wanaweza kuunga mkono au kuhujumu uafikiaji wa malengo yao ya kijamii, ni jambo linaloendelea kuunda mienendo ya raia na uhamasishaji wa raia.
Nchi nyingi huendeleza kampeni za elimu kwa umma ambazo hushughulikia masuala ya kijinsia na kiafya, usalama na matumizi ya maji, masuala ya kimazingira, usafi wa miji, uvutaji, na mengine. Kampeni hizi kwa wakati mwingine hutumia kanuni zilizoorodheshwa katika Kanuni za Elimu kwa Umma.Lakini hazikusudii kuanzia mwanzoni kuendeleza elimu kwa raia pekee yake.
Kampeni za Elimu kwa Umma
Ni vigumu kuona, hata hivyo, jinsi kampeni ya elimu kwa umma isivyoweza kuhimili elimu kwa raia. Wakati ambapo inahusika katika kushirikisha na kuyaleta pamoja makundi makubwa ya wananchi, miungano ya mashirika ya kijamii, au waelimishaji, ni katika shughuli ya uendelezaji wa ujuzi wa kiraia. Wakati ambapo inatayarisha ujumbe wake, haiwezi kuepuka kushughulikia maswali yanayohusu maadili ya raia na wajibu wa wananchi. Wakati ambapo inaweka wazi matakwa yake, haiwezi kuepuka kushughulikia maswali ya kijamii na mpangilio wa kijamii.
Waelimishaji ambao wanatilia makini Mipango yao katika kuhimili demokrasia watatumia kampeni za elimu kwa umma kusambaza ujumbe kwa raia na kuhakikisha kwamba kampeni hizi hazichukui mtazamo mpana wa kazi yao. Mwishowe, watawahusisha ili kuhakikisha bajeti za Mipango hiyo inaweza kutengenezwa katika njia ambazo zitapunguza mzigo kwa bajeti iliyokusudiwa elimu kwa umma pekee.
Kwa hivyo waelimishaji watataka kutambua kampeni kama hizo na kujadiliana nao kuhusu njia ambazo wanaweza kufanya kazi ya utoaji elimu kwa raia. Ili kufanya haya, mitazamo ya mwelimishaji wa raia kuhusu umuhimu wa kushiriki kwa raia kwa ufanifu wa elimu kwa umma, na umuhimu wa uelewa wa kisiasa na ujuzi wa kisiasa kwa ukusaji wa mazingira ambamo kampeni inaweza kufaulu, utakuwa muhimu.
Kuna nyakati katika historia ya nchi wakati mabadiliko ni dhahiri. Katika nyakati hizi, watu wanakubali kwa wepesi kushiriki katika mazungumzo yanayohusu maisha ya umma na ushiriki wa kisiasa. Kuna uwezekano kuwa watahusika, au hata kujali, na wanaweza kuonyesha haja za elimu, ufahamu au habari. Nyakati kama hizo ni nadra, lakini zinapojitokeza, zinampa mwelimishaji nafasi mwafaka.
Nyakati za Mabadiliko / Mpito
Labda kipindi cha wakati wa mabadiliko kinachojitokeza mara kwa mara katika demokrasia yoyote ni uchaguzi, hasa uchaguzi ambao unaonekana kuwa huenda kukawa na kubadilishwa kwa serikali. Nyakati kama hizo huenda ndiyo sababu muhimu ambayo inafanya elimu kwa Wapigakura kinyume na elimu kwa raia kuonekana kupata uzingatifu na usaidizi mkubwa kutoka nje na ndani ya nchi. Lakini kwa hakika, kinachofanyika ni kuwa uchaguzi unatoa kijisababu (ingawa iliyo nzuri) cha elimu kwa raia. Masuala ya uchaguzi na chaguo ambazo zinafaa kufanywa ziko wazi zaidi, diskosi ya umma ni kubwa zaidi, na nafasi za elimu, hasa katika kiwango kisicho rasmi, ni bayana zaidi.
Kuna nyakati zingine, hata hivyo, na waelimishaji watataka kutambua na kuzitumia nyakati hizi. Katika nchi kubwa, pale ambapo suala la kitaifa la demokrasia ya kikatiba limesuluhishwa, nyakati hizi huenda zikahitajika zaidi katika hali za kawaida. Na si jambo la kushangaza kuwa elimu kwa raia inaendelea kuhusishwa zaidi na masuala ya demokrasia ya kinyumbani (ki-nchi) na serikali ya nchi. Kwa upande mwingine huenda ikawa kuwa, pamoja na serikali ya nchi, serikali ya jimbo au mashirika ya kiuchumi yanatoa mwongozo wa mabadiliko kwa nchi nyingi.
Kuna ongezeko la idadi ya majaribio, hasa katika vyuo vikuu lakini tena katika mifumo kadha ya shule na shule binafsi, kuunda Mipango inayofunza huduma. Mipango hii kwa kawaida huundwa kama mkusanyiko wa mafunzo darasani na shughuli za kujitolea katika huduma iliyopo na mashirika ya kutoa misaada. Kwa sababu wale wanaohusika ni wanafunzi wa kudumu na wanasukumwa na mahitaji ya mwaka wa kielimu, huduma ambayo inatolewa na ambayo inatarajiwa kuwa mafunzo yatafunzwa yanaelekea kuwa ya mtawanyiko na ya kurudiarudia, na inaratibiwa sio na wanafunzi bali na taasisi ya elimu na taasisi inayopokea huduma hizi.
Kazi ya Umma
Kutokana na ongezeko la usafiri wa vijana, hasa katika mashariki, kujitolea kwa hiari wakati wa likizo kunazidi kuongezeka, na hii Mipango inayohusu ukufunzi, kujitolea na uanazuoni huenda zaidi na kuwaingiza vijana katika maendeleo na huduma iliyopo, mara nyingi na sio kila mara katika nchi inayoendelea.
Thamani ya mipango hii ni finyu katika upeo – watu wachache zaidi wanaweza kushiriki – na kiwango cha kujifunza kinategemea kujitolea kwa mtu binafsi na taasisi zinazotuma na zile zinazopokea.
Lakini muungano umeanza ambao unasajili vikundi vya vijana na mtu mzima ambaye ni mdhamini ili kushiriki katika kazi ya kuunda uchanganuzi wa kijamii, kuhamisha ujuzi wa kimpangilio na kisiasa wakati wa mchakato wa kusuluhisha tatizo, na kuwahimiza vijana kuchukua hatua zenye manufaa kwa kipindi cha wakati mahususi.
Mfano mzuri wa makundi kama hayo, ambayo sasa yanafanya kazi Marekani, Afrika Kusini na Ireland, hukutana wakati wa kujivinjari, huteua matatizo yaliyo katika jamii zao, kuzungumza na wale ambao wana malighafi na uwezo kama vile serikali za mitaa, na kuunda miungano na makundi mengine katika jamii ambao wana lengo sawa la kusuluhisha tatizo fulani mahususi. Sio tu kundi la kushughulikia tatizo fulani, kwa sababu wakiwa katika shughuli yao, vijana wanajifunza namna ulimwengu unavyofanya kazi na namna ya kuubadilisha; na katika wanapofanya hivyo, wanapata uelewa wa masuala yanayohusu raia ambao unaweza kuhamishiwa kwa nyanja zingine za maisha yao na ya jamii.