Sheria za Kitaifa Huathiri Majukumu ya Wasimamizi wa Uchaguzi
Chaguzi hufanyika katika muktadha mahususi wa kisheria ambao unaweza kuendeleza au kudumiza malengo ya elimu kwa Wapigakura. Mamlaka ya kusimamia uchaguzi itataka kuzingatia, kwa hivyo, sio tu mipaka yao ya kisheria lakini pia mahitaji ya kisheria ambayo yataathiri uwezo wao kuwafahamisha na kuwaelimisha Wapigakura na kupata ushiriki wa watu wengi katika mchakato wa uchaguzi. Katika hali hii, ni muhimu kuelewa kuwa wasimamizi wa uchaguzi kwa kawaida watategemea serikali iliyochaguliwa (au katika hali ya jamii za kimpito, mamlaka ya kisheria).
Kinyume na miongozo mingine mingi ya kisheria, hata hivyo, sheria zinazohusiana na mifumo ya uchaguzi; maadili ya uchaguzi; uhuru wa kujieleza, habari, na kujumuika; fedha za kampeni; na shughuli za kisiasa, zinaweza kubadilishwa ili kunufaisha chama kilicho kwenye uongozi au serikali. Haya yanaweza kuathiri sio tu usimamizi wa kijumla wa uchaguzi, bali pia yanaweza kuathiri ufaafu wa juhudi za kuwafahamisha na kuwahamasisha Wapigakura.
Katika nafasi ya awali zaidi, kwa hivyo, wasimamizi wa uchaguzi watataka kuanzisha mbinu za kupunguza athari za hali mahususi za kisiasa kwa sheria zote ambazo zina athari za kiuchaguzi. Mbinu kama hizo zinaweza kuhusisha uingizaji wa taratibu fulani za kiuchaguzi katika katiba, zinazohitaji idadi maalum ya watu wengi, uidhinishaji na kamati mahususi, au taratibu za kujulisha umma na kushiriki kwa umma kabla ya kufanyiwa marekebisho.
Sheria nzuri ya Uchaguzi Huendeleza Elimu kwa Wapigakura
Mbali na haya, kuna mambo mengine muhimu ya kuzingatia kuhusiana na sheria za uchaguzi.
1) Habari kwa Wapigakura na shughuli za elimu zitakuwa rahisi zaidi ikiwa sheria na kanuni zitapunguza uchangamano na kuhimiza ushiriki wa kijumla.
Hasa, ufafanuzi wa kisheria wa, na desturi zinazohusiana na, karatasi za kupigia kura zilizoharibika na zisizofaa unaweza kuwa aidha zuivu (wenye vikwazo), na hivyo wa kuadhibu, au ukawa wazi. Vifungu vya sheria vinavyohusiana na muundo wa karatasi ya kupigia kura unaweza kuwa aidha changamano, na hivyo unaotatiza, au ukawa wa moja kwa moja. Mchakato wa kupiga kura unaweza kuendelezwa, kisaikolojia na kimwili, kupitia kwa nambari, uwezo wa kufikiwa, na maeneo ya vituo vya kupigia kura; ubora na utoaji wa mafunzo kwa maafisa; masaa ya kupiga kura; utoaji wa huduma maalum za upigaji kura; na wepesi wa kujisajili.
Huku kukiwa na uchukulio wa kijumla kuwa wale wanaotoa mswada wa sheria za uchaguzi hupendelea uwezo mkubwa wa wananchi kuweza kufikia uchaguzi, historia inapendekeza kuwa hii haijakuwa hali ya kawaida. Sheria inafaa kuwa ya kidemokrasia kikamilifu. Kama si ya kidemokrasia, inawezekana kwa makundi ya kutetea umma kushiriki katika shughuli za utoaji habari kwa Wapigakura, elimu, na uhamasishaji ili kubadilisha mfumo.
Uthabiti, ndani ya na baina ya sheria, pia utakuwa muhimu zaidi. Je, sheria na vifungu vyote vya sheria vinavyosimamia uchaguzi, kwa mfano zile zinazohusu haki za kupiga kura, chaguzi za mashinani, chaguzi za kitaifa, kura za maamuzi, fedha za kampeni, habari kwa umma na shughuli za kampeni, na adhabu za kiutawala na kigaidi ni thabiti? Si jambo geni kwa sheria za chaguzi za mashinani na za kitaifa kuwa na vifungu visivyo thabiti au vinavyojikanganya. Hii italeta matatizo makubwa ikiwa chaguzi za mashinani na za kitaifa zinafanyika wakati huo huo. Ikiwa kuna makataa ya usajili wa Wapigakura yanayohitilafiana, au taratibu zinazotofautiana za kujaza malalamishi, mkanganyo huenda ukatawala siku yote na jukumu la kuelimisha Wapigakura litakuwa changamano zaidi. Ili kuepuka matatizo ya aina hii, baadhi ya nchi zimeanzisha kanuni za ulimwenguni kuhusu uchaguzi.
2) Elimu si lazima iwe shughuli isiyo na mapendeleo.
Hofu inaweza kutokea kuwa kutoa mamlaka kamili kwa makundi ya kila aina katika jamii kuenda nyanjani na kutoa elimu kutasababisha propaganda dhidi ya serikali, kupigia debe baadhi ya vyama vya kisiasa kwa njia ya mapendeleo, na kusambaza habari zisizo sahihi. Kwa hivyo, sheria inaweza kuweka vizuizi kwa kuamua ni nani awezaye kutekeleza shughuli ya utoaji elimu na habari kwa Wapigakura. Kwa sasa, hata hivyo, sheria nyingi za uchaguzi hazizingatii kwa makini suala la elimu kwa Wapigakura. Huku haya yakiweza kuashiria kuwa wasimamizi wa uchaguzi wana uhuru wa kuhusisha tume zisizo za kisheria, mashirika, au watu binafsi, mamlaka (ya kusimamia uchaguzi) yaliyoteuliwa majuzi huwa yapata ugumu katika kutumia uhuru huu katika jamii ambapo haja ya habari na elimu ni kubwa lakini raslimali ni haba na ufahamu, ukubalifu na imani katika waelimishaji mbadala ni ndogo.
Kuna njia ambazo raslimali inaweza kufanywa kuwa nyingi iwapo sheria imefafanua elimu kwa Wapigakura kwa upana au angalau imeipa mamlaka ya kusimamia uchaguzi uwezo wa kuleta au kuhusisha mashirika mengine ya kitaifa au kimataifa na watu binafsi.