Je, Elimu kwa mpiga kura ni muhimu?
Chaguzi hushindaniwa na vyama vya kisiasa, na katika baadhi ya nchi, na wagombezi wanaowasilishwa na mashirika ya umma na makundi ya Wapigakura. Chaguzi hizo husimamiwa na wasimamizi wa uchaguzi. Wapigakura hujisajili na kisha hupiga kura.
Katika hali gani na kwa haki gani waelimishaji hujihusisha katika shughuli ambayo inaonekena kuwa ya moja kwa moja zaidi? Wengine wanaweza kuchukulia kwamba ni shughuli ambayo hutekelezwa na watu wazima ambao wanajua akili zao na wana ustarabu unaohitajika ili kuishi katika mazingira ya kjamii na kisiasa ambao huenda uchaguzi unafanyika.
Hata hivyo, hali sahili na ya kawaida inaweza kuibushwa kwa kusambaza habari kwa umma kuhusu namna uchaguzi utakavyoandaliwa. Hata katika demokrasia zilizo na utamaduni wa chaguzi za mara kwa mara, Wapigakura wanahitaji habari.
Wanaopiga kura kwa mara ya kwanza na wale wenye mahitaji maalum huenda wakawa miongoni mwa makundi mengi yanayofaa kuelimishwa. Mabadiliko katika istilahi za uchaguzi, kwa mfano uanzishaji wa tarakilishi zenye skrini ya kugusa, au katika tamaduni za kupiga kura kama vile kupiga kura kupitia kwa barua pepe, kutasababisha haja ya juhudi za kielimu za kijumla. Ongezeko katika idadi ya wagombezi au vyama vya kisiasa vinavyoshindana katika uchaguzi, na vilevile idadi ya juhudi za umma Wapigakura wanaulizwa kuamua, huenda kukaifanya karatasi ya kupigia kura kuwa changamano.
Mkanganyo wa hivi majuzi wa “upigakura wa kuhamahama” ambao ulitumika katika Palm Springs, Florida, wakati wa uchaguzi wa mwaka wa 2000 unadhihirisha haja ya kutekeleza elimu kwa Wapigakura ya kutosha hata katika hali ambazo huenda zikachukuliwa kuwa shwari zaidi.
Haja ya elimu kwa Wapigakura itakuwa hata ya juu zaidi katika mazingira ya mabadiliko / mpito na kipindi baada kinachofuatia hali ya mzozo ambayo yanapitia katika mabadiliko taratibu, ya kisheria, na yenye mpangilio na pale ambapo haki ya kupiga kura inaweza kuzidisha kwa wengi.
Lakini ni nini jukumu la elimu pana, katika kipindi cha uchaguzi na kama juhudi zinazoendelea, kuhusu thamani ya uchaguzi? Hili ni swali ngumu sana.
Hata kuna wale ambao wanapendekeza kuwa elimu kwa Wapigakura inaweza kuingiliwa na hata kutumiwa vibaya, na kuwa inafaa kutengwa kabisa na mchakato wa uchaguzi.
Ongezeko la Idadi ya wale Wanaoshughulikia Elimu kwa Wapigakura
Ongezeko la idadi ya wale wanaowajibikia elimu kwa Wapigakura inatokana na sababu mbalimbali. Kanuni za kimataifa zinazojitokeza kwa sasa zinaunga mkono kusambaa kwa demokrasia na kupanua kwa haki ya kupiga kura kwa watu wote. Chaguzi, bila shaka, ni sehemu muhimu sana ya muungano huu. Katika muktadha huu, elimu kwa Wapigakura inahakikisha kuwa wananchi wanaelewa na wanaweza kutekeleza haki zao za kiuchaguzi.
Pamoja na hayo, wajibu wa kisheria unaweka waziwazi majukumu yaliyoelezwa ya mamlaka ya kusimamia uchaguzi. Kuna imani inayoendelea kuongezeka kuwa mamlaka za kusimamia uchaguzi zinafaa kutoa sio tu habari lakini pia elimu kuwasaidia Wapigakura katika kutekeleza jukumu lao la kiraia la kupiga kura.
Majukumu Hufafanua Shughuli za Elimu kwa Wapigakura
Kuweka majukumu kunawezesha shirika kuangazia malengo na shughuli / matendo ambayo ni faafu kwa jamii fulani mahususi na mchakato wa kiuchaguzi ambamo unatumika.
Katika baadhi ya hali, wajibu wa kuelimisha Wapigakura unaweza kuanzishwa kupitia kwa sheria au amri ya serikali. Kwa kawaida, wajibu wa kisheria unapewa mamlaka ya kusimamia uchaguzi au makundi yanayopokea fedha za umma kwa kuendesha shughuli ya elimu kwa Wapigakura. Wajibu wa Tume Kuu ya Uchaguzi ya Shirikisho la Urusi kushiriki katika shughuli pana za utoaji elimu na mafunzo kwa Wapigakura, kwa mfano, ulitolewa na amri ya serikali ambayo ilihusisha shughuli hizo kwa utekelezaji na utoshelezaji wa haki za kupiga kura ambazo zilitungwa mwaka wa 1994.
Kuhusu mashirika ya kijamii, wajibu wa kuendeleza shughuli za elimu kwa Wapigakura imeanzishwa kikamilifu kupitia kwa nyaraka za kuhusishwa kwake, kanuni, na taarifa ya misheni. Taarifa ya misheni hasa, inaendeleza lengo la kuasisiwa kwa shirika, hutambulisha watu ambao shirika hilo linahudumia, na kwa ufupi huelezea jinsi ambavyo shirika linatekeleza wajibu huo.
Taasisi ya umma au shirika la kupigania haki za kijamii linaweza kuwa na wajibu finyu au mpana. Hivi ni kusema kwamba yanaweza kuwa yamebanwa uendelezaji wa shughuli za elimu kwa Wapigakura. Au, yanaweza kuendeleza shughuli za elimu kwa Wapigakura kama sehemu ya wajibu mpana katika elimu kwa raia au uhamasishaji wa umma.
Baada ya kuunda wajibu, aidha kutokana na utunzi wa sheria, au amri ya serikali, au kama taarifa ya misheni, itakuwa muhimu kuendeleza ufahamu wa umma kuuhusu na kuhusu haja ya kuunga mkono wajibu huo, na vilevile kuanzisha uhalaliwa, Mpango wa elimu kwa Wapigakura. Kuchukua hatua kama hizo huzidisha uwezekano wa kufaulu kwa juhudi za utoaji elimu kwa Wapigakura.
Utokeaji wa uchaguzi bila shaka utaibua masuala kadha ambayo watu watataka habari au elimu zaidi. Mara nyingi, waelimishaji hutumia uchaguzi kama jukwaa la kupanua uelewa wa watu kuhusu masuala kijamii, kiuchumi na kisiasa katika ujumla wake. Wanaweza hata kutumia nafasi hii kujaribu kuboresha ujuzi wa kimpangilio wa watu. Hizi ni sehemu muhimu za elimu kwa demokrasia inayofanya kazi.
Kwa wakati huo huo, hata hivyo, waelimishaji wanastahili kuwa makinifu. Wanafaa kufanya kazi katika mazingira wazi. Uendelezaji wa wajibu wa kitaasisi / kishirika na mipaka mahususi ya Mpango ni muhimu katika uelezeaji wa umakinifu huu.